Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili MDAs & LGAs Kada ya Afya December 2025

Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili MDAs & LGAs Kada ya Afya December 2025

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya MDAs & LGAs ametangaza rasmi orodha ya Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili MDAs & LGAs Kada ya Afya December 2025, ambapo mchakato wa usaili umepangwa kuanza tarehe 16 Desemba 2025 hadi 22 Desemba 2025 nchini kote. Tangazo hili limeeleza kuwa washiriki watakaofaulu hatua hii wataendelea kupangiwa vituo vya kazi kulingana na taratibu za Serikali.

Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili MDAs & LGAs Kada ya Afya December 2025

Maelezo ya Msingi Kuhusu Usaili

Ratiba ya usaili imeainishwa kwa kila kada, ikionyesha tarehe na maeneo ya kufanyia usaili kwa wasailiwa wote. Kwa kada zote za afya, usaili utafanyika katika mikoa yote ya Tanzania Bara pamoja na vituo maalumu visiwani Unguja na Pemba, kulingana na mahali alipo msailiwa kwa sasa (current resident region). Vituo vya usaili vimeambatanishwa katika tangazo easmi lililotolewa na Utumishi kupitia tovuti ya PSRS: www.ajira.go.tz

Kwa mfano, usaili wa Afisa Muuguzi Msaidizi II umewekwa tarehe 16 Desemba 2025, wakati kada kama Mfamasia Daraja II, Afisa Muuguzi Daraja II, Daktari Daraja II, na Mhandisi wa Vifaa Tiba zimepangwa kufanyiwa usaili tarehe 17 Desemba 2025.

Kada nyingine za afya, kama Fiziotherapist Daraja II, Tabibu wa Kinywa na Meno, na Afisa Afya Mazingira, zimepangiwa tarehe 18 Desemba 2025, huku usaili wa Tabibu Daraja II ukifanyika 19 Desemba 2025. Kundi la mwisho linalojumuisha kada kama Afisa Afya Mazingira Msaidizi II, Dobi Daraja II, na Mtoa Tiba kwa Vitendo Daraja II, limepangiwa usaili 22 Desemba 2025.

Vitu Vinavyohitajika

Kwa mujibu wa maelekezo ya PSRS, waliotwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia taratibu zote zilizopangwa:

1. Kuleta Vyeti Halisi

Wasailiwa wanalazimika kuwasilisha vyeti halisi pekee, vikiwemo:

  • Cheti cha kuzaliwa
  • Vyeti vya Kidato cha IV na VI
  • Astashahada, Stashahada au Shahada (kulingana na nafasi)

Imesisitizwa kuwa Testimonials, Provisional Results, Statement of Results au results slips za Form IV na VI hazitakubalika, na msailiwa hataruhusiwa kuendelea na usaili endapo atawasilisha nyaraka hizo.

2. Kitambulisho kwa Ajili ya Utambuzi

Kila msailiwa anapaswa kuja na kitambulisho halali kama:

  • Kitambulisho cha Mkazi
  • Kitambulisho cha Mpiga Kura
  • Kitambulisho cha Uraia
  • Leseni ya Udereva
  • Hati ya Kusafiria

Au barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji

3. Maagizo ya Usajili wa Bodi

Kwa kada zinazohitaji usajili wa kitaaluma, wasailiwa wanapaswa kuleta:

  • Vyeti halisi vya usajili
  • Leseni za kufanyia kazi

4. Mavazi, Usafiri na Muda

Waliotwa wanapaswa kufika kwenye eneo la usaili kwa wakati na kwa mavazi yenye staha kulingana na waraka wa mavazi. Gharama za usafiri, chakula na malazi ni jukumu la msailiwa mwenyewe. Pia kuvaa barakoa ni lazima kwa mujibu wa maelekezo.

5. Waliyosomea Nje ya Nchi

Wanapaswa kuhakikisha vyeti vyao vimehakikiwa na TCU, NACTVET au NECTA. Kwa kada zinazohitaji GPA, msailiwa analazimika kuleta cheti cha ukokotozi wa GPA kutoka TCU.

6. Akaunti ya Ajira Portal

Waliotwa wanapaswa kuingia kwenye akaunti zao za Ajira Portal ili kunakili namba ya usaili na kuhakikisha wanakumbuka email na password zao, hasa kwa usaili wa mtandaoni.

7. Tofauti ya Majina

Wasailiwa wenye tofauti za majina kwenye nyaraka zao wanapaswa kuleta Hati ya Kiapo cha Kubadili Jina (Deed Poll) iliyosajiliwa na Wizara ya Ardhi

Kuangalia Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili MDAs & LGAs Kada ya Afya December 2025

Kupata orodha kamili ya majina, tarehe za usaili, na maelezo ya kina kwa kila kada:

👉 Pakua PDF Rasmi la “Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Kada za Afya – December 2025

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Ualimu 2025 (Mikoa Mbalimbali)
  2. Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga na Mafunzo Jeshi la Magereza Desemba 2025
  3. Mfumo wa Maombi ya Ajira Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (Zimamoto Ajira Portal)
  4. Mfano wa Barua Ya Maombi ya Kazi Jeshi la Zimamoto 2025
  5. Nafasi za Kazi Jeshi la Zimamoto November 2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo