Seleman Mwalimu ‘Gomez’ Asajiliwa Fountain Gate

Seleman Mwalimu ‘Gomez’ Asajiliwa Fountain Gate

Klabu ya Fountain Gate imekamilisha usajili wa aliyekuwa mshambuliaji wa KVZ ya Zanzibar na mfungaji bora wa ligi kuu ya Zanzibar (PBZ Premier league) msimu wa 2023/2024, Seleman Mwalimu ‘Gomez’.

Seleman Mwalimu ‘Gomez’ aliyewahi kuzichezea timu mbalimbali ikiwemo FGA Talents inayoshiriki Ligi ya Championship amejiunga na kikosi hicho kwa mkopo ili apate nafasi ya kucheza akitokea Singida Black Stars ambayo imemsajili kwa mkataba wa miaka mitatu.

“Ni kweli tumemtoa kwa mkopo kwa sababu bado ni mchezaji mdogo na anayehitaji muda zaidi wa kucheza ili kulinda kipaji chake, tuliangalia timu itakayompa nafasi ya kucheza na Fountain tukaona ni sehemu sahihi kwake,” kilisema chanzo hicho.

Uhamisho wa Gomez ni sehemu ya mpango mkubwa wa Fountain Gate kujenga timu imara yenye uwezo wa kushindana na vigogo Ligi Kuu Bara. Klabu hiyo imeahidi kuendelea kuimarisha kikosi chake kwa kusajili wachezaji wenye viwango vya juu kutoka ndani na nje ya nchi.

Seleman Mwalimu 'Gomez' Asajiliwa Fountain Gate

Rekodi za Gomez Katika Ligi ya Zanzibar

Msimu uliopita akiwa na KVZ, Gomez alionyesha kiwango cha juu sana. Aliibuka mfungaji bora wa Ligi ya Zanzibar (ZPL) baada ya kufunga mabao 20 na kutoa pasi za mabao saba (assists) katika michezo 27 aliyocheza kati ya 30. Huu ni ushahidi wa uwezo wake mkubwa na matarajio ni kwamba ataendelea kufanya vizuri akiwa na Fountain Gate.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. TETESI ZA USAJILI: Dodoma Jiji FC Katika Mazungumzo ya Kumrejesha Wazir Jr
  2. Tetesi za Usajili simba 2024/2025
  3. Tetesi za Usajili Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/2025
  4. FIFA Yaiondolea Yanga Adhabu ya Kufungiwa Kusajili
  5. Dirisha la Usajili Ligi Kuu Tanzania kufunguliwa Juni 15 hadi Agosti 15, 2024
  6. Tetesi za Usajili Yanga: Okrah Kwenye Rada za Kuondoka Yanga? Habari Kamili
  7. Jinsi Ya Kuangalia Usajili Wa Namba ya Simu
  8. Tetesi za Usajili Real Madrid 2024/2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo