Fomu za Kujiunga Kidato cha Kwanza 2026 – TAMISEMI Form One Joining Instructions

Fomu za Kujiunga Kidato cha Kwanza 2026 – Form One Joining Instructions

TAMISEMI imetangaza kuwa wanafunzi 937,581 waliokuwa na sifa za kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2026 wamepangiwa shule, sawa na asilimia 100 ya watahiniwa waliofaulu mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2025. Kundi hili linajumuisha wasichana 508,477 na wavulana 429,104, wakiwemo wanafunzi 3,228 wenye mahitaji maalum.

Akitoa taarifa hiyo jijini Dar es Salaam, Desemba 4, 2025, Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Profesa Riziki Shemdoe, alisema kuwa kila mwanafunzi aliyepata alama 121 hadi 300 katika mtihani wa darasa la saba amechaguliwa bila kupitwa hata mmoja.
Katika maelezo yake, Prof. Shemdoe alibainisha:

“Uchaguzi wa wanafunzi umezingatia kigezo cha ufaulu wa mtahiniwa, na kila mwenye sifa amepangiwa shule ya serikali. Hii inahakikisha usawa na upatikanaji wa nafasi kwa wanafunzi wote waliofaulu.”

Pia alisisitiza wajibu wa wazazi kuhakikisha watoto wanaripoti shuleni kwa wakati na kuendelea na masomo hadi kukamilisha kidato cha nne.

Muundo wa Upangaji wa Wanafunzi – Shule za Bweni na Shule za Kutwa

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wanafunzi wamepangiwa katika shule 5,230 za sekondari za serikali nchi nzima. Upangaji umezingatia makundi mawili makuu:

1. Shule za Bweni

Shule hizi zimegawanywa katika makundi matatu:

(a) Shule za Bweni kwa Wanafunzi Wenye Ufaulu wa Juu

Zinapatikana katika kila mkoa, na nafasi zimegawanywa kitaifa kwa kuzingatia idadi ya watahiniwa.
Wanafunzi 815 (wasichana 335, wavulana 480) wamechaguliwa kujiunga na shule za kitaifa za ufaulu wa juu kama:

  1. Ilboru
  2. Kibaha
  3. Msalato
  4. Kilakala
  5. Mzumbe
  6. Tabora Boys
  7. Tabora Girls

(b) Shule za Bweni za Amali

Hapa, nafasi zimegawanywa kwa kila mkoa kulingana na idadi ya watahiniwa waliotahiniwa, kisha kugawanywa sawa kwa kila halmashauri.

(c) Shule za Bweni za Kitaifa

Upangaji umefanywa kwa kuzingatia idadi ya watahiniwa wa halmashauri husika, kwa kutumia kanuni za kugawa nafasi kitaifa.

2. Shule za Kutwa

Watahiniwa wengi zaidi wamesambazwa kwenye shule hizi, ambazo zimeandaliwa kupokea idadi kubwa ya wanafunzi.

Kuhusu tarehe za kuripoti:

  • Shule za Bweni: Januari 12, 2026
  • Shule za Kutwa: Januari 13, 2026

Fomu za Kujiunga Kidato cha Kwanza 2026 – Nini Kinaonekana Ndani ya Joining Instructions?

Fomu za kujiunga kidato cha kwanza (Form One Joining Instructions) hutolewa na TAMISEMI kwa kila mwanafunzi baada ya kutangazwa kwa shule aliyopewa. Fomu hizi ni nyaraka muhimu kwa maandalizi ya mwanafunzi kabla ya kuanza masomo.

Kwa kawaida, Fomu za Kujiunga Kidato cha Kwanza 2026 zitakuwa na maudhui yafuatayo:

  1. Shule Uliyopangiwa
  2. Tarehe ya Kuripoti Shuleni
  3. Nyaraka Muhimu za Kuwasilisha
  4. Michango ya Shule na Ada ya Uendeshaji
  5. Mahitaji ya Sare za Shule
  6. Vifaa Vinavyohitajika wakati wa kuripoti shule hususani kwa waliochaguliwa shule za Bweni
  7. Vifaa vya Kitaaluma
  8. Maelekezo Mengine Muhimu kama vile kanuni za nidhamu, Taratibu za afya na usafi na Ratiba ya masomo na malazi

Jinsi ya Kupata Fomu za Kujiunga Kidato cha Kwanza 2026

Mara tu matokeo ya uchaguzi wa shule yanapotangazwa, wanafunzi wanaweza kupakua Fomu za Kujiunga Kidato cha Kwanza 2026 kupitia hatua hizi rahisi:

1. Tembelea Tovuti Rasmi ya TAMISEMI

👉 https://selform.tamisemi.go.tz

2. Fungua Sehemu ya “Form One Selection 2026”

Chagua mkoa na halmashauri ili kupata jina lako.

3. Tafuta Jina Lako au Namba ya Mtihani

Orodha ya watahiniwa inaonekana kwa mpangilio wa shule.

4. Pakua Fomu za Kujiunga (PDF)

Bofya kwenye jina la shule uliyochaguliwa kupakua Joining Instruction.

Fomu za Kujiunga Kidato cha Kwanza 2026 – TAMISEMI Form One Joining Instructions

5. Hifadhi na Kuchapisha Fomu

Hakikisha umehifadhi nakala na kuichapisha kwa ajili ya maandalizi.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Majina ya Wanafunzi na Shule Walizopangiwa Kidato cha Kwanza 2026
  2. Wanafunzi Waliochaguliwa Kidato Cha Kwanza 2026
  3. Matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba 2025/2026 NECTA
  4. NECTA Standard Seven Results 2025 Released: 81.8% of Candidates Pass the PSLE Examination
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo