Simba vs Azam Leo 07/12/2025 Saa Ngapi?

Simba vs Azam Leo 07/12/2025 Saa Ngapi?

Leo Mnyama Simba atashuka dimbani kuwakabili wana-rambaramba Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC ambao kwa miaka mingi umebeba ushindani na heshima kubwa ndani ya soka la Tanzania. Baada ya kusogezwa mara kadhaa kutokana na sababu mbalimbali, hatimaye pambano hili linaloitwa Mzizima Derby litapigwa jioni ya leo kuanzia saa 11:00 jioni kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Simba vs Azam Leo 07/12/2025 Saa Ngapi?

Mara ya mwisho timu hizi zilipokutana kwenye ligi, zilishindwa kutambiana na kutoka sare ya mabao 2-2, katika mchezo uliokuwa na presha ya mbio za ubingwa. Rekodi zinaonyesha kuwa tangu Azam ipande Ligi Kuu mwaka 2008, mpaka sasa zimekutana mara 34, na Simba akibeba ubabe kwa ushindi 15, huku Azam ikipata 6, na sare 13. Kwa jumla, mabao 77 yamefungwa katika mikutano yao, Simba akiongoza kwa 48 dhidi ya 31 ya Azam.

Kocha kaimu wa Simba, Seleman Matola, anayekiongoza kikosi chake kwa mara ya kwanza kwenye Mzizima Derby, ataendelea kutegemea nyota walio katika kiwango cha juu akiwamo kipa Yacoub Suleiman, Jean Ahoua, Rushine de Reuck, Neo Maema, Jonathan Sowah na Kibu Denis. Sowah anaongoza orodha ya mabao ya Simba hadi sasa akiwa ametupia matatu, huku Rushine akiwa na mawili na Ahoua akichangia mabao na asisti muhimu.

Kwa upande mwingine, Azam ya Florent Ibenge imeonyesha upinzani licha ya mfululizo wa sare kwenye mechi nne za Ligi Kuu. Wataendelea kumtegemea Feisal Salum Fei Toto aliye na rekodi nzuri dhidi ya Simba, pamoja na Yahya Zayd, James Akaminko, Sadio Kanoute na mshambuliaji Japhte Kitambala. Fei Toto anaongoza mabao ndani ya kikosi hicho akiwa amefunga mawili.

Historia ya Mzizima Derby imejaa matukio ya kukumbukwa. Simba na Azam zimewahi kutoa matokeo ya mabao mengi, ikiwamo mechi za 3-2 mwaka 2011 na 2020. Pia Bocco ndiye kinara wa mabao katika hii derby akiwa ametupia nane, akifuatiwa na Meddie Kagere mwenye tano.

Kwa muktadha wa msimu huu, mchezo wa leo unakuwa muhimu zaidi kwa sababu zote zimeanza hatua ya makundi ya CAF kwa matokeo magumu, na ushindi unaweza kurejesha morali kwa vikosi vyote. Matola na Ibenge wanahitaji mwanzo mzuri kwenye derby yao ya kwanza msimu huu, jambo linaloongeza ukubwa wa presha kwa wachezaji.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Makundi ya Kombe la Dunia 2026
  2. Msimamo wa Ligi kuu NBC Tanzania 2025/2026
  3. TFF Yatangaza Kikosi cha Awali cha Taifa Stars kwaajili ya Fainali za AFCON 2025 Morocco
  4. Ratiba ya Kombe la Shirikisho CRDB Federation Cup 2025/2026
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo