Ratiba ya Mechi za Taifa Stars AFCON 2025
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imewasili nchini Morocco tayari kwa ajili ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025), michuano mikubwa zaidi ya soka barani Afrika inayotarajiwa kuanza rasmi Jumapili, Desemba 21.
Ujio huo unakuja baada ya Stars kuweka kambi ya maandalizi kwa takribani wiki mbili jijini Cairo, Misri, ambako ilicheza mechi za kirafiki kama sehemu ya kujiandaa kikamilifu kwa changamoto za mashindano hayo.
Katika AFCON 2025, Taifa Stars imepangwa Kundi C, kundi linaloonekana kuwa na ushindani mkubwa likiwa na mataifa yenye uzoefu mkubwa wa soka la kimataifa. Safari ya Tanzania katika hatua ya makundi itachukua siku saba pekee, kuanzia Desemba 23 hadi Desemba 30, kipindi ambacho kitaamua hatma ya Stars katika michuano hiyo.
Ratiba ya Mechi za Taifa Stars Hatua ya Makundi AFCON 2025
Nigeria vs Tanzania
- Tarehe: Desemba 23, 2025
- Muda: Saa 20:30
Hii itakuwa mechi ya kwanza kwa Taifa Stars katika AFCON 2025, ikiwakutanisha na Nigeria ‘Super Eagles’. Pambano hili bila shaka litakua ndio mtihani mkubwa wa mwanzo dhidi ya moja ya vigogo wa soka barani Afrika. Pamoja na ugumu wake, mchezo huu unaonekana pia kama fursa ya Stars kuonyesha mapema kuwa haijaja kushiriki bali kushindana.
Uganda vs Tanzania
- Tarehe: Desemba 27, 2025
- Muda: Saa 20:30
Mechi ya pili ni derby ya Afrika Mashariki dhidi ya Uganda. Huu ni mchezo wenye presha kubwa kutokana na ushindani wa kihistoria kati ya mataifa haya mawili. Ushindi katika mechi hii unaweza kuipa Tanzania nafasi nzuri ya kusonga mbele kutoka hatua ya makundi.
Tanzania vs Tunisia
- Tarehe: Desemba 30, 2025
- Muda: Saa 19:00
Mechi ya mwisho ya kundi itakuwa dhidi ya Tunisia, taifa linalojulikana kwa nidhamu na uzoefu mkubwa katika michuano ya AFCON. Kwa mujibu wa muktadha wa kundi, huu unaweza kuwa mchezo wa maamuzi kwa Taifa Stars katika kupigania nafasi ya kufuzu hatua inayofuata.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Bei ya Tiketi za Kombe la Dunia 2026 Yazua Mjadala Mkubwa Duniani
- Mchango Mkubwa wa Salah Waipa Liverpool Ushindi Mnono Dhidi ya Brighton
- Timu Nane Zathibitishwa Kushiriki Kombe la Mapinduzi 2026 Zanzibar
- Ratiba Ya AFCON 2025 Hatua Ya Makundi
- Kikosi cha Taifa Stars AFCON 2025
- Matokeo ya Coastal Union vs Yanga Leo 07/12/2025








Leave a Reply