Fomu za Kujiunga Vyuo Vya VETA 2026
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imetangaza rasmi orodha ya waombaji waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya ufundi stadi pamoja na Fomu za Kujiunga Vyuo Vya VETA 2026 kwa mwaka wa masomo 2026.
Tangazo hilo linahusisha waombaji 14,433 kati ya waombaji 18,875 waliowasilisha maombi, likionesha ongezeko la mwitikio na umuhimu unaozidi kupewa elimu ya ufundi stadi nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Anthony Kasore, amesema kuwa mchakato wa uchaguzi umefanyika kwa kuzingatia kikamilifu miongozo na mifumo rasmi ya serikali, huku ukilenga kutoa fursa sawa za elimu kwa Watanzania wote.
“Jumla ya waombaji 14,433 wamepangiwa kujiunga na mafunzo ya ufundi stadi katika vyuo vya VETA kwa ngazi ya kwanza kwa mwaka wa masomo 2026,” amesema Kasore.
Takwimu Muhimu za Waliochaguliwa VETA 2026
Kwa mujibu wa VETA, kati ya waombaji waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya mwaka 2026:
- Wanaume ni 8,776
- Wanawake ni 5,657
Aidha, mgawanyo wa muda wa masomo unaonesha kuwa:
- Waombaji 12,942 wamechaguliwa kwa masomo ya asubuhi
- Waombaji 1,491 wamepangiwa masomo ya jioni
Kasore ameongeza kuwa waombaji 4,511 wanasubiri kupangiwa vyuo na fani kutokana na kuchagua fani moja pekee wakati wa maombi.
Orodha ya Vyuo na Fomu za Kujiunga Vyuo Vya VETA 2026
Waombaji waliochaguliwa wanaweza kupata Fomu za Kujiunga Vyuo Vya VETA 2026 kwa kubonyeza jina la chuo husika kwenye jedwali la vyuo lililotolewa na VETA. Orodha hiyo inajumuisha vyuo vingi vya VETA katika mikoa mbalimbali nchini, vikiwemo:
Mapendekezo ya Mhariri:
- Matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba 2025/2026 NECTA
- Ratiba ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2026
- Wanafunzi Waliochaguliwa Kidato Cha Kwanza 2026
- Form One Selection 2026 | Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Kwanza 2026
- Matokeo ya Kidato cha Nne 2024/2025 (NECTA Form Four Results)
- Botswana PSLE Results 2025 Released: 52,766 Candidates Sit Examination as Pass Rate Reaches 99.91%









Leave a Reply