Timu Zilizofuzu Hatua Ya 16 Bora AFCON 2025

Timu Zilizofuzu Hatua Ya 16 Bora AFCON 2025

Mechi za Hatua ya Makundi ya michuano ya AFCON 2025 zinaelekea tamati huku ushindani ukiwa mkubwa katika makundi yote. Mataifa mbalimbali yamekuwa yakipambana vikali kutafuta tiketi ya kufuzu, na hadi sasa baadhi ya timu tayari zimejihakikishia nafasi zao katika hatua ya 16 bora. Michuano hiyo inayofanyika Morocco inaendelea kuvutia hisia za mashabiki barani Afrika, huku kila bao na kila pointi likiwa na uzito mkubwa katika maamuzi ya nani anaendelea na nani anaondoka.

Timu Zilizofuzu Hatua Ya 16 Bora AFCON 2025

Mfumo wa Kufuzu Hatua ya 16 Bora AFCON 2025

Katika AFCON 2025, timu zitakazofuzu hatua ya 16 bora ni zile zitakazomaliza katika nafasi mbili za juu kwenye kila kundi, pamoja na timu nne bora zitakazomaliza nafasi ya tatu zikiwa na matokeo mazuri zaidi. Mfumo huu umeongeza ushindani mkubwa hadi dakika za mwisho za mechi za makundi, kwani hata timu zilizo nafasi ya tatu bado zina nafasi ya kuendelea kulingana na matokeo.

Timu Timu Zilizofuzu Hatua Ya 16 Bora AFCON 2025

Hadi kufikia hatua hii ya mashindano, timu tatu tayari zimejihakikishia kufuzu raundi ya 16 bora baada ya kushinda mechi zao mbili za mwanzo. Timu hizo ni:

  1. Misri
  2. Nigeria
  3. Algeria
  4. South Africa

Misri imeonyesha ubora mkubwa tangu mwanzo wa michuano, ikikusanya alama sita mapema na kujihakikishia tiketi ya kuendelea. Nigeria nayo imefanya vyema katika Kundi C na tayari imehakikisha nafasi yake kabla ya mechi za mwisho. Algeria, kutoka Kundi E, pia imefuzu mapema na bado ina nafasi ya kuathiri ni timu ipi itakayomfuata katika kundi lake.

Ratiba ya Hatua ya Mtoano AFCON 2025

Baada ya kukamilika kwa hatua ya makundi, michuano itaingia rasmi kwenye awamu ya mtoano. Mechi za hatua ya 16 bora zitachezwa kuanzia 3 hadi 6 Januari 2026. Robo fainali zitafuatia tarehe 9 na 10 Januari, kabla ya nusu fainali kupigwa 13 Januari. Fainali ya michuano imepangwa kufanyika 18 Januari mjini Rabat, ambapo bingwa wa AFCON 2025 atatajwa rasmi.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Msimamo wa Kundi C La Tanzania AFCON 2025
  2. Kikosi cha Tanzania Taifa Stars vs Uganda Leo 27/12/2025
  3. Matokeo ya Uganda Vs Tanzania Taifa Stars Leo 27/12/2025
  4. Uganda vs Tanzania Taifa Stars Leo 27/12/2025 Saa Ngapi?
  5. Ratiba ya Mechi za AFCON Leo 27/12/2025
  6. Msimamo wa Makundi AFCON 2025
  7. Bao la Dakika za Mwisho la Patson Daka Lainusuru Zambia Dhidi ya Mali, Mechi Ikiisha 1-1
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo