Matokeo ya Kidato Cha Pili 2025/2026 (NECTA FTNA Results)

Matokeo ya Kidato Cha Pili 2025/2026 (NECTA FTNA Results)

Leo 10/01/2026 NECTA imetangaza Matokeo ya Kidato Cha Pili 2025/2026 yanayojulikana rasmi kama Form Two National Assessment (FTNA), yakihusisha wanafunzi wote waliofanya upimaji wa kitaifa wa Kidato cha Pili katika shule za sekondari nchini Tanzania. Tangazo hili limeidhinishwa rasmi na Baraza la Mitihani la Tanzania kufuatia upimaji uliofanyika kati ya tarehe 10 hadi 19 Novemba 2025, na linatoa taswira ya kina kuhusu hali ya ufaulu, mahudhurio, ulinganifu wa kijinsia, pamoja na ubora wa elimu katika ngazi ya sekondari ya chini.

Kwa mujibu wa takwimu rasmi za Baraza la Mitihani la Tanzania, mahudhurio katika FTNA 2025 yalifikia asilimia 91.3, sawa na wanafunzi 811,575 kutoka shule za sekondari 6,223. Ufaulu wa jumla umefikia asilimia 86.93, ukiwa ni ongezeko la asilimia 1.52 ikilinganishwa na mwaka 2024, jambo linaloashiria kuendelea kuimarika kwa kiwango cha elimu katika ngazi ya Kidato cha Pili.

Kati ya wanafunzi waliofaulu, wasichana wanachangia asilimia 56 huku wavulana wakiwa asilimia 44, na wanafunzi 78,309 (9.65%) wakipata Daraja la Kwanza (Division I).

Matokeo ya Kidato Cha Pili 2025/2026 ni sehemu muhimu ya mfumo wa tathmini ya kitaaluma nchini, yakilenga kupima kiwango cha uelewa wa wanafunzi baada ya miaka miwili ya masomo ya sekondari. Aidha, matokeo haya hutumika kama nyenzo ya msingi kwa wanafunzi, walimu, wazazi, wasimamizi wa shule na wadau wengine wa elimu katika kupanga mikakati ya kuboresha ufundishaji na ujifunzaji, sambamba na kutoa mwelekeo wa maendeleo ya kielimu kabla ya kuendelea na Kidato cha Tatu.

Matokeo ya Kidato Cha Pili 2025/2026 (NECTA FTNA Results)

Mtihani wa Upimaji wa Kidato Cha Pili (FTNA) ni Nini?

Mtihani wa Upimaji wa Kidato cha Pili, maarufu kama FTNA, ni mtihani wa kitaifa unaosimamiwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) kwa wanafunzi wa shule zote za sekondari nchini. Mtihani huu hufanyika kila mwaka na hutumika kama chombo muhimu cha tathmini ya kielimu kinachopima kiwango cha maarifa na uelewa wa mwanafunzi katika masomo ya msingi ya sekondari.

Kwa mwaka 2025, mtihani wa upimaji wa Kidato cha Pili ulifanyika katika shule zote za sekondari nchini Tanzania kuanzia tarehe 10 Novemba 2025 hadi 20 Novemba 2025. Kipindi hiki kilihusisha tathmini ya kina ya masomo mbalimbali yaliyomo kwenye mtaala wa elimu ya sekondari, kwa lengo la kufuatilia maendeleo ya ujifunzaji wa wanafunzi baada ya miaka miwili ya masomo.

Mtihani wa Upimaji wa kidato cha pili (FTNA) ni tathmini endelevu inayolenga kutoa mrejesho unaoweza kutumika na walimu kuboresha mbinu za ufundishaji, wanafunzi kuongeza juhudi katika maeneo yenye changamoto, pamoja na wazazi na walezi kufuatilia maendeleo ya kitaaluma ya watoto wao kabla ya kuendelea na Kidato cha Tatu.

Soma Pia

  1. Wanafunzi Waliochaguliwa Kidato Cha Kwanza 2026
  2. Ratiba ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2026
  3. Matokeo ya Kidato cha Nne 2024/2025 (NECTA Form Four Results)
  4. Majina ya Wanafunzi na Shule Walizopangiwa Kidato cha Kwanza 2026
  5. Siku ya Kuripoti Shule Kidato cha Kwanza 2026

Masomo Yaliousika Katika Mtihani wa Kidato Cha Pili 2025

Mtihani wa Kidato Cha Pili unahusisha masomo mbalimbali yanayolenga kukuza maarifa ya kinadharia pamoja na ujuzi wa vitendo. Masomo hayo ni pamoja na:

  • Kiswahili
  • Basic Mathematics
  • English Language
  • Biolojia
  • Fizikia
  • Kemia
  • Jiografia
  • Historia
  • Uraia
  • Elimu ya Dini ya Kiislamu
  • Bible Knowledge
  • Masomo ya Ufundi kama Building Construction, Mechanical Engineering na Electrical Engineering
  • Masomo ya Biashara kama Book-Keeping na Commerce
  • Lugha za Kigeni kama Kifaransa na Kichina

Mchanganyiko huu wa masomo unaakisi malengo ya elimu ya sekondari nchini Tanzania katika kujenga wanafunzi wenye maarifa mapana na ujuzi unaoendana na mtaala wa taifa.

Je, NECTA Imeshatangaza Matokeo ya Kidato Cha Pili 2025/2026?

Ndiyo. Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza rasmi Matokeo ya Kidato Cha Pili 2025/2026 (Form Two National Assessment – FTNA) baada ya kukamilika kwa taratibu zote za uchakataji, uhakiki na uidhinishaji wa matokeo hayo. Tangazo hili linahusu wanafunzi wote waliofanya upimaji wa kitaifa wa Kidato cha Pili uliofanyika kati ya tarehe 10 hadi 19 Novemba 2025 katika shule za sekondari nchini.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi, matokeo hayo yanaonyesha hali ya ufaulu, mahudhurio, ulinganifu wa kijinsia, pamoja na ubora wa matokeo kwa shule na masomo mbalimbali, ikiwa ni sehemu ya tathmini muhimu ya maendeleo ya wanafunzi baada ya miaka miwili ya elimu ya sekondari. Hatua hii inaweka msingi wa kitaaluma kwa wanafunzi kabla ya kuendelea na Kidato cha Tatu.

Wanafunzi, wazazi, walezi na wadau wa elimu wanashauriwa kupata na kuhakiki matokeo ya Kidato Cha Pili 2025/2026 kupitia tovuti rasmi ya NECTA ambayo ni https://necta.go.tz, na kuepuka kutegemea taarifa zisizo rasmi ambazo zinaweza kupotosha.

NECTA FTNA Results 2025/2026: Nini Kinaonyeshwa Kwenye Matokeo?

Matokeo ya Kidato Cha Pili 2025/2026 (NECTA FTNA Results) huonesha kiwango cha ufaulu wa mwanafunzi kwa kila somo pamoja na daraja la jumla (Division). Aidha, matokeo haya huwasilishwa kwa kuzingatia mgawanyo wa kijinsia, jambo linalosaidia kutoa picha ya hali ya elimu kitaifa kwa mwaka husika.

Muonekano wa Ukurasa wa Matokeo ya Kidato Cha Pili

Maana ya Neno “Referred” Kwenye Matokeo ya NECTA

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetoa ufafanuzi leo 08/01/2026 kuhusu matumizi ya neno “Referred” linaloonekana kwenye Matokeo ya Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne (SFNA) na Matokeo ya Kidato cha Pili (FTNA).

Kwa mujibu wa NECTA, neno Referred linamaanisha kuwa mwanafunzi husika hajafaulu upimaji huo kwa kiwango kinachomruhusu kuendelea na darasa au kidato kinachofuata.

NECTA imeeleza kuwa mwanafunzi aliyepata matokeo ya Referred anatakiwa kurudia Darasa la Nne au Kidato cha Pili, kulingana na upimaji alioufanya, ili kupata fursa ya kuimarisha uelewa wake katika masomo yaliyobainika kuwa na changamoto. Uamuzi huu unalenga kuhakikisha mwanafunzi anapata msingi imara wa kielimu kabla ya kuendelea na hatua inayofuata ya masomo.

Ufafanuzi huu wa NECTA ni muhimu kwa wanafunzi, wazazi na walezi katika kuelewa vyema maana ya matokeo yanayotolewa na kuchukua hatua sahihi za kitaaluma kwa maendeleo ya mwanafunzi.

Kwa wanafunzi na wazazi, taarifa hizi ni muhimu katika kufanya maamuzi ya kitaaluma, hususan wakati wa kuchagua mwelekeo wa masomo pindi mwanafunzi anapoendelea na Kidato cha Tatu.

Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Kidato Cha Pili 2025/2026 Mtandaoni

Baada ya Matokeo ya Kidato Cha Pili 2025/2026 (NECTA FTNA Results) kutangazwa rasmi na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), wanafunzi, wazazi na walezi wanaweza kuyapata kwa urahisi kupitia mtandao. NECTA hutoa matokeo haya kupitia tovuti yake rasmi, hatua inayolenga kuhakikisha uwazi na upatikanaji wa taarifa sahihi kwa wakati.

Ili kusaidia kuelewa kwa vitendo mchakato wa kuangalia matokeo, video ifuatayo inaonesha hatua za kufuata wakati wa kuangalia NECTA FTNA Results 2025/2026 mtandaoni.

Hatua za Kuangalia Matokeo ya Kidato Cha Pili 2025/2026

Tembelea Tovuti Rasmi ya NECTA
Fungua kivinjari cha intaneti na nenda kwenye tovuti rasmi ya NECTA. Hakikisha una muunganisho mzuri wa intaneti ili kurahisisha upakiaji wa ukurasa wa matokeo.

Bofya Sehemu ya “Results”
Baada ya kufungua tovuti, bofya menyu ya Results ambapo mitihani yote ya kitaifa huorodheshwa.

Chagua FTNA (Form Two National Assessment)
Tafuta na ubofye kipengele cha FTNA ili kufungua ukurasa wa Matokeo ya Kidato Cha Pili.

Chagua Mwaka wa Mtihani 2025
Chagua mwaka husika ili kupata Matokeo ya Kidato Cha Pili 2025/2026 (NECTA FTNA Results).

Tafuta Jina la Shule
Orodha ya shule zote zilizoshiriki mtihani itaonekana. Tafuta jina la shule unayotaka kuangalia matokeo yake.

Tafuta Namba ya Mtihani ya mwanafunzi
Ndani ya ukurasa wa shule, unaweza kutafuta jina la mwanafunzi au namba ya mtihani ili kuona matokeo yake binafsi, ikiwemo alama za masomo, jumla ya alama na daraja la ufaulu.

Angalia Matokeo ya Kidato cha Pili 2025 kwa Shule Zote (NECTA FTNA)

Takwimu Muhimu za Matokeo ya Kidato Cha Pili 2025/2026 (FTNA)

Matokeo ya Kidato Cha Pili 2025/2026 yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) yanaonyesha mwenendo chanya wa ufaulu na ushiriki wa wanafunzi katika upimaji wa kitaifa wa Form Two National Assessment (FTNA).

Takwimu hizi zinatoa picha halisi ya hali ya elimu ya sekondari ya chini nchini, kwa kuzingatia usajili, mahudhurio, ufaulu wa jumla, ulinganifu wa kijinsia, pamoja na ubora wa matokeo kwa shule na masomo.

Kwa mwaka 2025, jumla ya wanafunzi 889,264 walisajiliwa kufanya upimaji wa Kidato cha Pili, wakiwemo wasichana 492,856 (55%) na wavulana 396,408 (45%). Kati yao, wanafunzi 811,575 walihudhuria mtihani sawa na asilimia 91.3, kutoka katika shule za sekondari 6,223 nchini kote. Wanafunzi 77,689 (8.7%) hawakuhudhuria licha ya kusajiliwa, sababu zikitajwa kuwa ni pamoja na utoro na changamoto za kiafya.

Kwa upande wa ufaulu, wanafunzi 759,091 wamefaulu upimaji wa FTNA 2025 sawa na asilimia 86.93, kiwango ambacho ni ongezeko la asilimia 1.52 ikilinganishwa na mwaka 2024. Katika ulinganifu wa kijinsia, wavulana waliofaulu ni asilimia 88.28 ya waliofanya mtihani, huku wasichana wakiwa asilimia 85.89. Kati ya wanafunzi wote waliofaulu, wasichana wanawakilisha asilimia 56 na wavulana asilimia 44.

Kwa kuzingatia ubora wa ufaulu, jumla ya wanafunzi 240,469 (29.64%) wamepata madaraja ya kwanza hadi ya tatu, hali inayoonyesha kuimarika kwa ubora wa matokeo ikilinganishwa na miaka ya nyuma. Aidha, wanafunzi 78,309 (9.65%) wamepata Daraja la Kwanza (Division I).

Kwa upande wa ufaulu kishule, asilimia 99.6 ya shule zenye matokeo zimepata wastani wa daraja la A hadi D, huku idadi ya shule zilizopata daraja A ikiongezeka na zile zenye daraja F zikiendelea kupungua.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Matokeo ya Darasa la Nne 2025/2026 (NECTA SFNA Results)
  2. NECTA Yatangaza Usajili wa Watahiniwa wa Kujitegemea CSEE na FTNA 2026
  3. Matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba 2025/2026 NECTA
  4. Fomu za Kujiunga Vyuo Vya VETA 2026
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo