Azam VS Simba Leo 08/01/2026 Saa Ngapi?

Azam VS Simba Leo 08/01/2026 Saa Ngapi?

Wana rambaramba wa Azam FC leo wanashuka dimbani kuivaa Simba SC katika pambano kubwa la nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi 2026, mchezo unaosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini. Dabi hii ya Mzizima inapigwa leo Alhamisi tarehe 08 Januari 2026, katika Uwanja wa New Amaan Complex, Unguja, kuanzia saa 2:15 usiku.

Taarifa Muhimu za Mchezo

  • Mchezo: Azam FC vs Simba SC
  • Mashindano: Nusu Fainali – NMB Mapinduzi Cup 2026
  • Tarehe: 08 Januari 2026
  • Muda: Saa 2:15 usiku
  • Uwanja: New Amaan Complex, Unguja

Viingilio

  • Orbit & Saa: 3,000/=
  • Urusi: 5,000/=
  • VIP: 10,000/=

Azam VS Simba Leo 08/01/2026 Saa Ngapi?

Dabi ya Mzizima Yarejea Mapinduzi Cup

Ni takribani mwezi mmoja umepita tangu timu hizi zikutanishe nguvu kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, ambapo Azam FC iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Simba SC. Leo usiku, dabi hiyo inarudi tena, safari hii ikiwa na uzito mkubwa zaidi kwani ni hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi 2026.

Mashindano ya mwaka huu yamebeba simulizi za kisasi, kwani mechi zote za nusu fainali zinawakutanisha wapinzani waliokutana kwenye hatua muhimu hapo awali. Kwa Simba, huu ni mtihani wa kurejesha heshima mbele ya Azam, huku Azam ikilenga kuendelea kudhihirisha ubabe wake kwenye michuano hii.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Timu Zilizofuzu Robo Fainali AFCON 2025
  2. Msimamo wa Kundi C La Tanzania AFCON 2025
  3. Haaland Aipiku Rekodi ya Magoli ya Cristiano Ronaldo EPL
  4. Bingwa wa AFCON 2025 Kubeba Zaidi ya Bilioni 24 za Kitanzania
  5. Chelsea Yanusurika Kupigika Nyumbani Kwa Newcastle United
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo