Matokeo ya Kidato cha Pili na Darasa la Nne 2025 Yatangazwa Rasmi na NECTA

Matokeo ya Kidato cha Pili na Darasa la Nne 2025 Yatangazwa Rasmi na NECTA

Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) leo Jumamosi, tarehe 10 Januari 2026, limetangaza rasmi Matokeo ya Kidato cha Pili na Darasa la Nne 2025, yanayotokana na upimaji wa kitaifa uliofanyika mwezi Oktoba na Novemba 2025. Tangazo hili linaainisha kwa kina hali ya ufaulu, kiwango cha usajili na mahudhurio ya watahiniwa, pamoja na taswira ya ubora wa elimu katika ngazi za elimu ya msingi na sekondari nchini, kwa mujibu wa takwimu rasmi zilizothibitishwa na Baraza la Mitihani Tanzania.

Matokeo ya Kidato cha Pili na Darasa la Nne 2025

Matokeo ya Mtihani wa Darasa la Nne 2025

Mtihani wa kitaifa wa upimaji wa Darasa la Nne ulifanyika tarehe 22 na 23 Oktoba 2025. Jumla ya wanafunzi 1,583,686 walisajiliwa kushiriki upimaji huu, wakiwemo wasichana 818,673 sawa na asilimia 52, na wavulana 765,013 sawa na asilimia 48.

Mahudhurio yalifikia asilimia 94, yakihusisha wanafunzi 1,487,377 kutoka shule za msingi 20,508. Hata hivyo, wanafunzi 93,309 sawa na asilimia 6 hawakufanya upimaji licha ya kusajiliwa.

Kwa upande wa matokeo, ufaulu wa jumla umefikia asilimia 88.91, sawa na wanafunzi 1,249,970 waliopata madaraja ya ufaulu A, B, C na D. Hii ni ongezeko la asilimia 2.67 ikilinganishwa na ufaulu wa mwaka 2024 ambao ulikuwa asilimia 86.24, na mwaka 2023 uliokuwa asilimia 83.34. Takwimu hizi zinaashiria kuimarika kwa ubora wa elimu katika ngazi ya Darasa la Nne.

Kwa kuzingatia jinsia, wasichana waliofaulu ni 733,287 sawa na asilimia 90.1 ya wasichana wote waliofanya upimaji, huku wavulana waliofaulu wakiwa 621,683 sawa na asilimia 87.59. Kati ya wanafunzi wote waliofaulu, wasichana ni asilimia 53 na wavulana asilimia 47.

Ufaulu kwa Ngazi ya Shule na Masomo – Darasa la Nne

Kati ya shule 20,508 zilizoshiriki, shule 20,364 sawa na asilimia 99.3 zilipata wastani wa madaraja ya ufaulu A hadi D. Shule 144 zilipata wastani wa daraja E, idadi iliyopungua ikilinganishwa na shule 197 mwaka 2024 na 325 mwaka 2023.

Kwa masomo, upimaji wa mwaka 2025 ulizingatia mtaala ulioboreshwa unaojumuisha masomo tisa. Kwa masomo ya lugha, ufaulu wa Kiswahili umefikia asilimia 92.1, ukipanda kutoka asilimia 84.52 ya mwaka 2024.

Ufaulu wa English Language umefikia asilimia 72.71 kutoka asilimia 68.86 mwaka 2024. Kwa lugha za chaguo, French Language ilipata asilimia 95.73, Arabic Language asilimia 80.45, na Chinese Language asilimia 93.16.

Kwa masomo ya sayansi, ufaulu wa sayansi ni asilimia 87.93 na hisabati asilimia 81.44. Somo la hisabati limeendelea kuimarika, ambapo wanafunzi waliopata daraja E wamepungua kwa asilimia 10 na waliopata daraja A wameongezeka kwa asilimia 10 ikilinganishwa na mwaka 2024. Kwa masomo ya sayansi ya jamii, jografia na mazingira ya sanaa na michezo limepata asilimia 83.22, huku historia ya Tanzania na maadili ikipata asilimia 82.99.

Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Pili 2025

Upimaji wa kitaifa wa Kidato cha Pili ulifanyika kuanzia tarehe 10 hadi 19 Novemba 2025. Jumla ya wanafunzi 889,264 walisajiliwa, wakiwemo wasichana 492,856 sawa na asilimia 55 na wavulana 396,408 sawa na asilimia 45.

Mahudhurio yalikuwa asilimia 91.3, yakihusisha wanafunzi 811,575 kutoka shule za sekondari 6,223. Wanafunzi 77,689 sawa na asilimia 8.7 hawakufanya upimaji licha ya kusajiliwa.

Ufaulu wa jumla kwa watahiniwa wa shule umefikia asilimia 86.93 sawa na wanafunzi 759,151. Kati yao, wavulana waliofaulu ni asilimia 88.28 na wasichana asilimia 85.89. Kwa jumla ya waliofaulu, wavulana ni asilimia 44 na wasichana asilimia 56. Ufaulu huu umeongezeka kwa asilimia 1.52 ikilinganishwa na mwaka 2024 na unaonyesha mwenendo chanya pia ikilinganishwa na mwaka 2023.

Kwa kuzingatia mitaala, wanafunzi waliosoma mtaala ulioboreshwa wamefaulu kwa asilimia 89.85, huku waliosoma mtaala wa awali wakifaulu kwa asilimia 86.93. Kwa ubora wa ufaulu, watahiniwa 240,469 sawa na asilimia 29.64 walipata madaraja ya kwanza hadi ya tatu, ikilinganishwa na asilimia 30.08 mwaka 2024 na asilimia 27.73 mwaka 2023.

Idadi ya wanafunzi waliopata daraja la kwanza (Division I) mwaka 2025 ni 78,309 sawa na asilimia 9.65. Mwaka 2024 idadi ilikuwa 77,772 sawa na asilimia 9.76, na mwaka 2023 ilikuwa 58,180 sawa na asilimia 8.37.

Ufaulu wa Shule na Masomo – Kidato cha Pili

Kwa ufaulu wa shule, shule 6,198 sawa na asilimia 99.6 ya shule zote zenye matokeo zilipata wastani wa daraja A hadi D. Shule zilizopata daraja A zimeongezeka na kufikia 177 mwaka 2025, kutoka 155 mwaka 2024 na 96 mwaka 2023. Shule zilizopata daraja F ni 25 mwaka 2025, ikilinganishwa na 27 mwaka 2024 na 30 mwaka 2023.

Kwa masomo ya sayansi jamii, history ilipata ufaulu wa asilimia 56.29 na geography asilimia 57.52. Ufaulu wa somo la civics ni asilimia 35.1, ikiwa ni ongezeko la asilimia 2 ikilinganishwa na mwaka 2024.

Kwa masomo ya lugha, Kiswahili kimepata asilimia 94.31, huku English Language ikipata asilimia 73.16. Takwimu zinaonyesha kuwa ufaulu wa English Language umeendelea kuimarika kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo.

Kwa upande wa sayansi asilia, physics, chemistry, biology na basic mathematics zimeendelea kuwa na ufaulu chini ya wastani, kati ya asilimia 22.71 na 41.84. Hata hivyo, basic mathematics imeonyesha kuimarika kwa kufikia asilimia 22.87 mwaka 2025 kutoka asilimia 18.85 mwaka 2024.

Upatikanaji wa Matokeo ya Kidato cha Pili na Darasa la Nne 2025

Matokeo ya Kidato cha Pili na Darasa la Nne 2025 yanapatikana rasmi kupitia tovuti ya Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA). Wazazi, wanafunzi na wadau wa elimu wanashauriwa kuyatazama matokeo kupitia njia rasmi pekee ili kuepuka taarifa zisizo sahihi.

ANGALIA HAPA CHINI MATOKEO YA DARASA LA NNE 2025

ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA
GEITA IRINGA KAGERA
KATAVI KIGOMA KILIMANJARO
LINDI MANYARA MARA
MBEYA MOROGORO MTWARA
MWANZA NJOMBE PWANI
RUKWA RUVUMA SHINYANGA
SIMIYU SINGIDA SONGWE
TABORA TANGA

ANGALIA HAPA CHINI MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2025

Angalia Matokeo ya Kidato cha Pili 2025 kwa Shule Zote (NECTA FTNA)

Kwa ujumla, Matokeo ya Kidato cha Pili na Darasa la Nne 2025 yanaonesha mwenendo wa kuimarika kwa ufaulu katika ngazi zote mbili, huku yakibainisha maeneo yanayohitaji kuendelea kuimarishwa, hususan katika masomo ya sayansi asilia na nidhamu ya mitihani.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Fomu za Kujiunga Vyuo Vya VETA 2026
  2. Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga na Vyuo vya VETA 2026
  3. When will 2025 Matric Results Released Online?
  4. Matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba 2025/2026 NECTA
  5. Ratiba ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2026
  6. Wanafunzi Waliochaguliwa Kidato Cha Kwanza 2026
  7. Form One Selection 2026 | Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Kwanza 2026
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo