Kombe la Toyota Cup 2024: Ratiba, Tarehe na Matokeo
Wakati msimu wa soka wa 2024/2025 barani Afrika ukikaribia kushika kasi, Julai hii inawapa mashabiki wa soka sababu ya kusherehekea. Toyota South Africa Motors (TSAM), kwa ushirikiano na Klabu ya Soka ya Kaizer Chiefs, wamezindua rasmi Kombe la Toyota Cup, mashindano ya kila mwaka ambayo yatawakutanisha mabingwa wa soka Afrika. Kombe hili jipya si tu onyesho la ushindani wa hali ya juu, bali pia ni jukwaa la kuunganisha mashabiki wa soka na chapa kubwa ya magari, huku likikuza mchezo pendwa barani Afrika.
Kombe la Toyota Cup 2024: Ratiba, Tarehe na Matokeo
Msimu wa kwanza wa Kombe la Toyota Cup utafanyika katika uwanja wa Toyota Stadium jijini Bloemfontein mnamo Jumapili, tarehe 28 Julai, saa 3 jioni kwa masaa ya Afrika Kusini na Saa 10 kwa masaa ya Tanzania. Mechi hii ya kihistoria itawakutanisha Kaizer Chiefs, mabingwa wa soka nchini Afrika Kusini, dhidi ya Young Africans Sports Club, klabu yenye mafanikio makubwa kutoka Tanzania.
Kabla ya mechi kuu ambayo itakutanisha mabingwa wa soka Tanzania Yanga Sc na Kaizer Chiefs, kutakuwa na mechi kati ya wakongwe wa Kaizer Chiefs na Bloemfontein Celtic itakayo anza saa 12:30 jioni (Masaa ya Afrika Kusini).
Mechi hii, imetajwa kua maalum kwa heshima ya marehemu Ntate Petrus Molemela, Rais wa Maisha wa Bloemfontein Celtic, na wakazi wapenda soka wa Mangaung. Lakini burudani haishii hapo! Wasanii mashuhuri watapamba jukwaa, na mmoja wa mashabiki mwenye bahati ataondoka na gari jipya kabisa aina ya Toyota Corolla Cross XI CVT!
Kaizer Chiefs | 0-4 | Young Africans Sports Club |
Angalia Hapa >> Matokeo ya Kaizer chiefs Vs Yanga Leo 28/07/2024 – Toyota Cup
Mapendekezo Ya Mhariri:
- Majina ya Wachezaji Wapya Simba 2024/2025
- Picha za Wachezaji Wapya wa Simba 2024/2025
- Hii apa CV ya Omary Abdallah Kiungo Mpya Wa Simba 2024/2025
- CV ya Fadlu Davids: Kocha Mpya wa Simba SC (2024/2025)
- Cv ya Valentino Mashaka Mshambuliaji Mpya wa Simba Sc 2024
- Kundi la Tanzania Kufuzu AFCON 2025
- Mishahara ya Wachezaji wa Yanga sc 2024
- CV Ya Abdulrazak Hamza Beki Mpya Wa Simba 2024/2025
Weka Komenti