Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Uhamiaji 2026
Idara ya Uhamiaji Tanzania imetangaza rasmi kutangazwa kwa majina ya walioitwa kwenye usaili Uhamiaji 2026 kwa waombaji wote walioomba ajira kupitia Mfumo wa e-Ajira wa Uhamiaji. Tangazo hilo limetolewa na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji likiwaelekeza waombaji waliochaguliwa kuchukua hatua muhimu ili kupata taarifa kamili za usaili wao.
Kwa mujibu wa tangazo hilo, waombaji wanapaswa kutembelea akaunti zao za maombi ya ajira kupitia tovuti rasmi ya Idara ya Uhamiaji Tanzania pamoja na barua pepe walizotumia wakati wa kuomba ajira, ili kupata taarifa na maelekezo ya tarehe na eneo la kufanya usaili.
Jinsi ya Kuangalia Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Uhamiaji 2026
Waombaji wote walioomba ajira wanatakiwa kuingia kwenye akaunti zao za maombi kupitia tovuti ya Uhamiaji na kukagua ujumbe uliotumwa. Taarifa hizi pia zinatumwa moja kwa moja kwenye barua pepe ya mwombaji, zikionyesha kama amechaguliwa kushiriki usaili pamoja na maelekezo husika. Ni muhimu kwa kila mwombaji kuhakikisha anatumia taarifa sahihi za kuingia kwenye akaunti yake, kwani taarifa zote muhimu kuhusu majina ya walioitwa kwenye usaili Uhamiaji 2026 zinapatikana kupitia njia hizo rasmi pekee.
Mahitaji Muhimu kwa Walioitwa Kwenye Usaili
Wasailiwa wote waliochaguliwa wanapaswa kufika kwenye usaili wakiwa na mahitaji yafuatayo:
Namba ya Ombi la Ajira (Application ID) kama ilivyotumwa kwenye akaunti na barua pepe ya mwombaji
Kitambulisho chenye picha ya mwombaji
Mfano: Kitambulisho cha Taifa, Kitambulisho cha Mkazi, Kadi ya Mpiga Kura, Pasipoti au kitambulisho kingine chochote kinachomtambulisha kwa sasa
Kalamu ya wino wa bluu
Mahitaji haya ni ya lazima kwa kila mshiriki wa usaili, na kutokuyakamilisha kunaweza kuathiri ushiriki wa mwombaji katika zoezi hilo.
Usaili wa Vitendo kwa Fani Maalum
Kwa waombaji waliochaguliwa katika fani za TEHAMA, udereva pamoja na ufundi magari, wanatakiwa kujiandaa kwa usaili wa vitendo (Practical Examination). Usaili huu utahusisha tathmini ya ujuzi wa moja kwa moja kulingana na fani husika.
Waombaji wa fani hizi wanashauriwa kuhakikisha wako tayari kwa usaili wa nadharia na vitendo kulingana na maelekezo watakayopokea kupitia akaunti zao na barua pepe.
Mawasiliano kwa Changamoto au Maulizo
Kwa waombaji watakaokutana na changamoto au kuwa na maulizo kuhusiana na majina ya walioitwa kwenye usaili Uhamiaji 2026, wametakiwa kuwasilisha maswali yao kupitia barua pepe rasmi ya Idara ya Uhamiaji:
📧 [email protected]
Bofya Hapa Kupakua Tangazo la Usaili Uhamiaji
Mapendekezo ya Mhariri:









Leave a Reply