Yanga SC VS JS Kabylie Leo 15/02/2026 Saa Ngapi?

Yanga SC VS JS Kabylie Leo 15/02/2026 Saa Ngapi?

Timu ya wananchi Yanga SC leo inashuka dimbani ikiwa na kibarua kizito cha kusaka ushindi muhimu mbele ya JS Kabylie katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Pambano hilo linabeba matumaini ya kuiwezesha klabu hiyo kuendelea kusalia kwenye michuano na kuipa Tanzania mwakilishi katika robo fainali.

Yanga SC VS JS Kabylie Leo Saa Ngapi?

  • Tarehe: Jumapili, 15 Februari 2026
  • Uwanja: New Amaan Complex, Zanzibar
  • Muda wa kuanza: Saa 1:00 usiku (19:00)
  • Matangazo ya moja kwa moja: Azam Sports 2 HD

Huu ni mchezo wa sita na wa mwisho wa makundi kwa Yanga, ukiwa na uzito mkubwa katika hatma ya Kundi B.

Yanga SC VS JS Kabylie Leo 15/02/2026 Saa Ngapi?

Hesabu za Kufuzu Robo Fainali

Katika Kundi B hali ya msimamo imeifanya Yanga kulazimika kushinda ili kubaki kwenye mashindano.

  1. Al Ahly – pointi 9
  2. AS FAR Rabat – pointi 8
  3. Yanga SC – pointi 5
  4. JS Kabylie – pointi 3

Ili kufuzu, Yanga inahitaji:

  • Kushinda mechi dhidi ya JS Kabylie
  • Kutegemea AS FAR Rabat ipoteze dhidi ya Al Ahly

Ushindi wa kawaida unaweza usitoshe. Timu hiyo inahitaji ushindi wa mabao mengi ili kuboresha uwiano wa mabao iwapo pointi zitafanana.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Viingilio vya Mechi ya Simba vs Stade Malien 14/02/2026
  2. Timu Zilizofuzu Robo Fainali Klabu Bingwa Afrika 2025/2026 CAF
  3. Al Nasr Yafikia Makubaliano Rasmi na Simba SC Kumnunua Kibu Denis
  4. Mechi ya Yanga vs Kabylie CAF ni Lini? Tarehe, Saa na Mahali
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo