Kikosi cha Yanga VS JS Kabylie Leo 15/02/2026

Kikosi cha Yanga VS JS Kabylie Leo 15/02/2026

Timu ya wananchi Yanga SC leo itashuka dimbani visiwani Zanzibar katika pambano la maamuzi likisaka ushindi muhimu dhidi ya JS Kabylie ya Algeria kwenye mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mchezo huo utapigwa katika Uwanja wa New Amaan Complex kuanzia saa 1:00 usiku na utaonyeshwa moja kwa moja kupitia AzamSports2HD. Ni mechi inayobeba hatma ya mabingwa hao wa Tanzania katika mbio za kufuzu hatua ya robo fainali huku macho na masikio ya wadau wa soka nchini yakielekezwa pia kwenye matokeo ya mchezo mwingine wa kundi hilo.

Kikosi cha Yanga VS JS Kabylie Leo 15/02/2026

Hesabu za Kufuzu kwa Yanga

Yanga inaingia kwenye mchezo huu ikiwa kwenye mazingira magumu ya kufuzu. Baada ya kupoteza ugenini mabao 1-0 dhidi ya AS FAR Rabat ya Morocco, matumaini yaliyobaki ni kushinda dhidi ya JS Kabylie huku ikiombea matokeo mazuri kutoka mchezo wa Al Ahly dhidi ya AS FAR.

Msimamo wa Kundi B

  1. Al Ahly – pointi 9
  2. AS FAR Rabat – pointi 8
  3. Yanga – pointi 5
  4. JS Kabylie – pointi 3

Ikiifunga JS Kabylie itafikisha pointi 8, lakini haitatosha pekee. Ili kufuzu rasmi, Yanga inahitaji:

  • Kushinda kwa mabao mengi (zaidi ya 2-0 au hata 3-0 kutengeneza uwiano mzuri)
  • AS FAR Rabat kupoteza dhidi ya Al Ahly

Ushindi mdogo unaweza kuifanya ibaki nafasi ya tatu kutokana na tofauti ya mabao.

Presha ya Historia

Mashabiki wa Yanga hawataki kurudia yaliyotokea msimu uliopita (2024/2025) ambapo walihitaji ushindi mechi ya mwisho lakini wakatoka sare 0-0 dhidi ya MC Alger na kumaliza wa tatu wakiwa na pointi nane.

Katika misimu mitatu iliyopita dhidi ya timu za Algeria kwenye mechi za maamuzi:

  1. Walifanikiwa mara moja dhidi ya CR Belouizdad
  2. Wakashindwa dhidi ya USM Alger
  3. Wakakwama pia mbele ya MC Alger

Mchezo huu unakuwa mtihani mwingine muhimu dhidi ya JS Kabylie.

Changamoto Ndani ya Kikosi

Licha ya kuwa na washambuliaji kama: Prince Dube, Laurindo Dilson Maria “Depu” na viungo wabunifu akiwemo Pacome Zouzoua, bado timu imekuwa na tatizo la umaliziaji.

Katika mechi tano za makundi:

  • Mabao ya kufunga: 2
  • Mabao ya kuruhusu: 4

Hali hii inaonyesha ukosefu wa uwiano kati ya safu ya ushambuliaji na ulinzi hata chini ya nahodha Bakari Mwamnyeto.

Kikosi cha Yanga VS JS Kabylie Leo 15/02/2026

Mashabiki wa Wananchi wanasubiria kwa hamu kuona orodha ya wachezaji ambao benchi la ufundi la Yanga litawaamini katika mchezo wa leo. Kwa kawaida katika michezo ya CAF, vikosi vya kwanza hutangazwa rasmi takribani saa moja kabla ya kuanza kwa pambano.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Viingilio vya Mechi ya Simba vs Stade Malien 14/02/2026
  2. Timu Zilizofuzu Robo Fainali Klabu Bingwa Afrika 2025/2026 CAF
  3. Al Nasr Yafikia Makubaliano Rasmi na Simba SC Kumnunua Kibu Denis
  4. Mechi ya Yanga vs Kabylie CAF ni Lini? Tarehe, Saa na Mahali
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo