Simba Yafuzu 32 Bora CRDB Federation Cup Baada ya Kuifunga Greenland 3-0
Wekundu wa Msimbazi Simba SC wamefanikiwa kukata tiketi ya kushiriki hatua ya raundi ya 32 bora ya michuano ya Kombe la FA maarufu kama Kombe la Shirikisho la CRDB, kufuatia ushindi wa mabao 3-0 walioupata dhidi ya Greenland katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam. Ushindi huo unaifanya Simba SC kuendelea na safari ya michuano hiyo ya msimu huu huku ikionyesha ubora wake mapema katika hatua za awali za mashindano.
Mabao Yaliyoipa Simba SC Ushindi
Katika mchezo huo, Simba SC ilianza kwa kasi na kupata bao la mapema kupitia kwa Baraka Mwangosi aliyefunga dakika ya 12 na kuiweka timu yake mbele.
Kabla ya mapumziko, katika dakika za nyongeza za kipindi cha kwanza, Anthony Mligo aliifungia Simba bao la pili na kuipa timu yake utulivu mkubwa kuelekea kipindi cha pili.
Dakika za mwisho za mchezo zilishuhudia Neo Maema akiandika bao la tatu na la mwisho, akihitimisha ushindi wa 3-0 dhidi ya Greenland.
Kwa ushindi huo, rasmi Simba SC yafuzu raundi ya 32 bora CRDB Federation Cup kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya Greenland.
Matokeo Mengine ya Kombe la Shirikisho la CRDB
Mbali na ushindi wa Simba SC, michezo mingine ya mashindano hayo ilichezwa katika viwanja mbalimbali nchini:
- Coastal Union 3-1 Nyumbu FC
- Transit Camp 4-0 Chama la Wana
- Dodoma Jiji 3-1 Kilimanjaro Wonders
- Fountain Gate 1-0 Mapinduzi
Katika mchezo uliovutia zaidi, KMC iliondolewa mashindanoni baada ya kufungwa kwa mikwaju ya penalti 3-2 na Bandari Tanzania, kufuatia sare ya mabao 3-3 ndani ya dakika 90 kwenye Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.
Bandari Tanzania ni timu inayoshiriki Ligi ya Kwanza.
Mkoani Mbeya, Mbeya City imepata ushindi wa mezani baada ya Biashara United kutotokea uwanjani katika mchezo uliopangwa kuchezwa Uwanja wa Halmashauri Chunya.
Mapendekezo ya Mhariri:









Leave a Reply