Matokeo TS Galaxy Vs Yanga Leo 24 July 2024- Mechi Ya Kirafiki

Kikosi cha Yanga Vs TS Galaxy 22 July 2024 Mechi Ya Kirafiki

Matokeo TS Galaxy Vs Yanga Leo 24 July 2024 – Matokeo ya Yanga Dhidi ya TS Galaxy Leo Mechi Ya Kirafiki

Mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania mara tatu mfululizo Yanga Sc leo watashuka dimbani kukabiliana na wakali wa kwa madiba Afrka kusini TS Galaxy katika mchezo wa pili wa michuano ya Mpumalanga Premier International Cup 2024. Mchezo huu utaanza majira ya saa 15:00 jioni kwa saa za Afrika Kusini na saa 16:00 jioni kwa saa za Tanzania katika uwanja wa Kanyamazane Afrika Kusini.

Mechi hii ni sehemu ya muendelezo wa maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu na michuano ya kimataifa ya CAF. Kwa Yanga SC, ni fursa muhimu ya kujipima nguvu dhidi ya timu zinazoshiriki michuano ya kimataifa, kuimarisha kikosi na kujaribu mbinu mbalimbali za kiufundi kutoka kwa kocha wao. Kwa TS Galaxy, ni nafasi ya kuthibitisha uwezo wao dhidi ya mabingwa wa Tanzania na kujipatia uzoefu zaidi.

Katika mchezo wao wa kwanza wa Mpumalanga Cup 2024, Yanga SC walikutana na FC Augsburg kutoka Ujerumani. Mchezo huo ulimalizika kwa Yanga SC kufungwa 2-1, licha ya jitihada zao za kupambana kwa nguvu zote. FC Augsburg waliweza kuonesha uwezo wao na kuibuka na ushindi huo muhimu. Kwa upande wa TS Galaxy, walikutana na Mbabane Swallows FC kutoka Eswatini katika mechi yao ya kwanza. Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya 2-2, huku timu zote zikionesha uwezo mkubwa na ushindani wa hali ya juu

Matokeo TS Galaxy Vs Yanga Leo 24 July 2024- Mechi Ya Kirafiki

TS Galaxy Fc 0-1 FT Yanga Sc
  • HT: Ts Galaxy Fc 0-0 Yanga
  • 55’—⚽️ Prince Dube

Angalia Hapa Kikosi cha Yanga Vs TS Galaxy 24 July 2024- Mechi Ya Kirafiki

Taarifa Kuhusu Mechi ya TS Galaxy Vs Yanga

🏆 Mpumalanga Premier International Cup 2024
⚽️ TS Galaxy FC vs Young Africans FC
📆 24.07.2024
🏟 Kanyamazane Stadium
🕖 15H00🇿🇦 16H00🇹🇿

Matokeo TS Galaxy Vs Yanga Leo 24 July 2024- Mechi Ya Kirafiki

Jinsi Ya Kuangali Mechi ya TS Galaxy Vs Yanga Leo 24 July 2024 Live

Azam Sports 1 HD imethibitisha kuwa itaonyesha moja kwa moja mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya Young Africans SC ya Tanzania na TS Galaxy ya Afrika Kusini. Mchezo huu uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu kubwa utafanyika leo Jumanne, tarehe 24 Julai 2024, kuanzia saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Baada ya mazungumzo ya kina baina ya klabu hizo mbili, TS Galaxy ilikubali ombi la Yanga SC kuuruhusu mchezo huo kuonyeshwa moja kwa moja katika televisheni, na hivyo kuwapa mashabiki wa soka kote Afrika Mashariki fursa ya kushuhudia mtanange huu wa kusisimua.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Hii apa Ratiba ya Mechi za Azam Fc Pre season
  2. Wiki ya Mwananchi 2024 (Yanga Day): Tarehe, Matukio na Bei ya Tiketi
  3. Jezi Mpya za Simba 2024/25
  4. Novatus Miroshi Ajiunga na Goztepe ya Uturuki
  5. Simba SC Yatoa Tamko Rasmi Kuhusu Kibu Mkandaji
  6. Vilabu Bora Afrika 2023/2024 (IFFHS Club Ranking)
  7. Matokeo Simba Vs El-Qanah Egypt (22 July 2024) Mechi Ya Kirafiki
  8. Washindi wa Tuzo Dar Port Kagame Cup 2024, Hawa Apa
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo