Simba Yalazimishwa Sare ya 1-1 na Pamba Jiji Kirumba
Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, wameshindwa kuendeleza matokeo chanya baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Pamba Jiji katika mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Matokeo hayo yamekuja siku moja tu baada ya mashabiki wao kufurahia sare ya watani wao, Yanga, dhidi ya TRA Unitedhali iliyoongeza ushindani na presha katika mbio za ligi.
Simba Yaanza Kwa Kasi, Oura Afungua Akaunti
Simba iliingia uwanjani ikiwa na dhamira ya kusaka ushindi mapema, huku kocha wake, Steve Barker, akifanya maamuzi ya kimkakati kwa kuwaanzisha pamoja Elie Mpanzu, Anicent Oura, na Libasse Gueye kwa mara ya kwanza katika ligi.
Mpanzu alipewa jukumu la kuongoza safu ya ushambuliaji, akisaidiwa na Oura na Gueye waliocheza pembeni, huku kiungo Clatous Chama akiratibu mashambulizi kutoka nyuma yao.
Mbinu hiyo ilionekana kuzaa matunda dakika ya 33, ambapo shambulizi la kushtukiza lililoanzishwa na Mpanzu lilimkuta Oura, aliyefanikiwa kufunga bao na kuipa Simba uongozi. Bao hilo liliwapa matumaini mashabiki wa Simba waliokuwa uwanjani wakiamini ushindi ulikuwa karibu.
Pamba Jiji Yasawazisha Haraka Kupitia Mwashinga
Hata hivyo, furaha ya Simba haikudumu kwa muda mrefu. Dakika tatu tu baada ya kufungwa, Pamba Jiji ilisawazisha kupitia James Mwashinga, aliyepiga mpira wa faulo uliomshinda kipa wa Simba, Mahamadou Kassali. Bao hilo lilirejesha ushindani na kufanya timu hizo kwenda mapumziko zikiwa sare ya 1-1.
Kipindi cha Pili: Simba Yakosa Majibu
Kipindi cha pili kilianza kwa Simba kujaribu kuongeza kasi ya mashambulizi kutafuta bao la ushindi, lakini Pamba Jiji ilionyesha uimara mkubwa katika safu ya ulinzi. Wenyeji walijipanga kwa idadi kubwa ya wachezaji nyuma, jambo lililowafanya Simba kushindwa kupenya kwa urahisi.
Dakika ya 74, Simba ilifanya mabadiliko kwa kumuingiza Morice Abraham kuchukua nafasi ya Alassane Kante kwa lengo la kuongeza nguvu katikati ya uwanja. Licha ya juhudi hizo, Simba haikufanikiwa kupata bao la pili, na mchezo huo ukamalizika kwa sare ya 1-1.
Matokeo Yaiathiri Simba Kwenye Msimamo
Sare hiyo imekuwa ya tatu kwa Simba katika mechi nne zilizopita, na kuifanya kufikisha pointi 28, ikishika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi. Wekundu hao wako nyuma kwa pointi moja tu dhidi ya Azam FC yenye pointi 29, ambayo nayo imetoa sare katika mechi yake dhidi ya Mashujaa.
Pamba Jiji Yaendelea Kung’ara Nyumbani
Kwa upande wa Pamba Jiji, matokeo hayo yanaendeleza rekodi yao nzuri wakiwa nyumbani. Timu hiyo imekuwa ngumu kufungika katika Uwanja wa CCM Kirumba, ikiwa imekusanya pointi 19 nyumbani ikiwa ni ya pili nyuma ya Yanga.
Katika mechi tisa za nyumbani, Pamba Jiji imeshinda tano dhidi ya Namungo, Coastal Union, KMC, Fountain Gate, na Mashujaa. Pia imetoa sare dhidi ya TRA United, Singida Black Stars, Azam, na sasa Simba. Jumla ya mabao yaliyofungwa ni 14 huku wakiruhusu matano pekee.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Senegal Yapokonywa Ubingwa wa AFCON 2025 Baada ya CAF Kubadili Matokeo ya Fainali
- Senegal Kupeleka Kesi CAS Kupinga Kupokonywa Taji la AFCON
- Kikosi cha Taifa Stars Kitakacho Ingia Kambini Machi 23, 2026 Kwa Ajili ya FIFA Series Rwanda
- Matokeo ya TRA United Vs Yanga Leo 18/03/2026
- Ratiba ya Ligi Kuu ya NBC Leo 18/03/2026









Leave a Reply