Tangazo la Nafasi za Kazi za Ualimu: Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia May 24 2024
Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma inakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 147 za ualimu kama ilivyoainishwa katika lililotolewa na Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) tareh 24 May 2024.
Tangazo la Nafasi za Kazi za Ualimu May 2024
Kama wewe ni muhitimu wa mafunzo ya elimu ngazi ya cheti, astashahada, shahada au zaidi na ungependa kutuma maombi ya kazi kwa nafasi zilizotangazwa na TAMISEMI, fursa imewadia. Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma inakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 147 za ualimu kama ilivyoainishwa katika tangazo hili.
Nafasi za Kazi Mwalimu Daraja la IIIA: Nafasi 100
- Sumbawanga MC – 12
- Ngara DC – 4
- Bariadi TC – 8
- Kyerwa DC – 14
- Mtwara DC – 4
- Mkuranga D – 11
- Geita DC – 13
- Kondoa DC – 6
- Chemba DC – 7
- Handeni DC – 5
- Shinyanga DC – 7
- Momba DC – 5
- Meatu DC – 4
Majukumu Ya Kazi
- Kuandaa azimio la kazi, maandalio ya masomo, nukuu za masomo na Mpango wa Kazi wa majukumu mengine aliyokabidhiwa;
- Kutengeneza na Kufaraghua zana za kufandishia na kujifunzia;
- Kufundisha, kufanya Tathmini na kutunza kumbukumbu za Maendeleo ya Wanafunzi;
- Kusimamia na kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi Shuleni na Darasani;
- Kusimamia malezi ya wanafunzi Kiakili, Kimwili, Kiroho na kutoa ushauri nasaha na unasihi;
- Kutoa ushauri wa kitaalamu na kitaaluma kuhusu maendeleo ya Elimu;
- Kusimamia utunzaji wa Vifaa na mali za Shule;
- Kufundisha na kusimamia Elimu ya Watu Wazima;
Sifa: Cheti cha Kidato cha Nne na mafunzo ya Ualimu ya miaka miwili.
Mshahara: TGTS-B
Nafasi za Kazi Mwalimu Daraja la IIIB (Hisabati): Nafasi 3
- Kondoa DC – 1
- Ilemela MC – 1
- Meatu DC – 1
Majukumu: Kama ilivyoainishwa kwa Mwalimu Daraja la IIIA.
Sifa: Cheti cha Kidato cha Sita/Nne na Stashahada ya Ualimu ya miaka miwili/mitatu yenye Hisabati.
Mshahara: TGTS-C
Nafasi za Kazi Mwalimu Daraja la IIIB (Fizikia): Nafasi 12
- Sumbawanga MC – 1
- Geita DC – 4
- Rombo DC – 5
- Shinyanga DC – 1
- Meatu DC – 1
Majukumu: Kama ilivyoainishwa kwa Mwalimu Daraja la IIIA.
Sifa: Cheti cha Kidato cha Sita/Nne na Stashahada ya Ualimu ya miaka miwili/mitatu yenye Fizikia.
Mshahara: TGTS-C
Nafasi za Kazi Mwalimu Daraja la IIIB (Kemia): Nafasi 3
- Ilemela MC – 1
- Shinyanga DC – 1
- Handeni – 1
Majukumu: Kama ilivyoainishwa kwa Mwalimu Daraja la IIIA.
Sifa: Cheti cha Kidato cha Sita/Nne na Stashahada ya Ualimu ya miaka miwili/mitatu yenye Kemia.
Mshahara: TGTS-C
Nafasi za Kazi Mwalimu Daraja la IIIB (Baiolojia): Nafasi 2
- Ilemela MC – 1
- Handeni – 1
Majukumu: Kama ilivyoainishwa kwa Mwalimu Daraja la IIIA.
Sifa: Cheti cha Kidato cha Sita/Nne na Stashahada ya Ualimu ya miaka miwili/mitatu yenye Baiolojia.
Mshahara: TGTS-C
Nafasi za Kazi Mwalimu Daraja la IIIC (Hisabati): Nafasi 9
- Sumbawanga MC – 1
- Ngara DC – 1
- Bariadi TC – 2
- Mkuranga DC – 2
- Ilemela MC – 2
- Shinyanga DC – 1
Majukumu: Kama ilivyoainishwa kwa Mwalimu Daraja la IIIA.
Sifa: Shahada ya Elimu/Ualimu yenye Hisabati au Shahada isiyo ya Ualimu/Elimu yenye Hisabati na Stashahada ya Uzamili ya Elimu.
Mshahara: TGTS-D
Nafasi za Kazi Mwalimu Daraja la IIIC (Fizikia): Nafasi 6
- Ngara DC – 1
- Bariadi TC – 1
- Mkuranga DC – 2
- Rombo DC – 1
- Handeni – 1
Majukumu: Kama ilivyoainishwa kwa Mwalimu Daraja la IIIA.
Sifa: Shahada ya Elimu/Ualimu yenye Fizikia au Shahada isiyo ya Ualimu/Elimu yenye Fizikia na Stashahada ya Uzamili ya Elimu.
Mshahara: TGTS-D
Nafasi za Kazi Mwalimu Daraja la IIIC (Kemia): Nafasi 8
- Ngara DC – 1
- Bariadi TC – 1
- Mkuranga DC – 2
- Sengrema DC – 1
- Ilemela MC – 2
- Wizara ya Elimu – 1
Majukumu: Kama ilivyoainishwa kwa Mwalimu Daraja la IIIA.
Sifa: Shahada ya Elimu/Ualimu yenye Kemia au Shahada isiyo ya Ualimu/Elimu yenye Kemia na Stashahada ya Uzamili ya Elimu.
Mshahara: TGTS-D
Nafasi za Kazi Mwalimu Daraja la IIIC (Baiolojia): Nafasi 2
- Bariadi TC – 1
- Ilemela MC – 1
Majukumu: Kama ilivyoainishwa kwa Mwalimu Daraja la IIIA.
Sifa: Shahada ya Elimu/Ualimu yenye Baiolojia au Shahada isiyo ya Ualimu/Elimu yenye Baiolojia na Stashahada ya Uzamili ya Elimu.
Mshahara: TGTS-D
Nafasi za Kazi Mwalimu IIIB (Kiingereza): Nafasi 2 (Wizara ya Elimu)
Majukumu: Kama ilivyoainishwa kwa Mwalimu Daraja la IIIA, lakini kwa wanafunzi wa Chuo.
Sifa: Cheti cha Kidato cha Nne na Stashahada ya Ualimu wa Elimu ya Awali/Msingi katika Kiingereza (miaka miwili/mitatu).
Mshahara: TGTS-C
Masharti ya Jumla Ya Nafasi za Kazi za Ualimu: Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia May 24
- Raia wa Tanzania mwenye umri usiozidi miaka 45 (isipokuwa kwa watumishi wa serikali).
- Ambatisha cheti cha kuzaliwa, CV, vyeti vya taaluma, na barua ya maombi.
- Maombi yatumwe kwa Katibu, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma, S.L.P. 2320, Dodoma.
Mwisho wa kutuma maombi: 6 Juni 2024
Kwa maelezo zaidi na kuomba, tembelea tovuti ya Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma au pakua Tangazo la kazi hapa chini
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA UALIMU WIZARA YA ELIMU NA LGA’s 24-05-2024
Mapendekezo Ya Mhariri:
Weka Komenti