Matokeo ya Yanga Vs Muembe Makumbi Leo 21/04/2026
Kikosi cha Young Africans SC kinashuka dimbani leo Jumanne kuikabili Muembe Makumbi City katika mchezo wa Kombe la Muungano utakaopigwa Uwanja wa New Amaan Complex kuanzia saa 1:15 usiku. Mchezo huu wa Matokeo ya Yanga Vs Muembe Makumbi Leo 21/04/2026 unasubiriwa kwa hamu huku ukiwa hatua ya kwanza kwa mabingwa watetezi katika safari ya kulinda taji lao.
Yanga imewasili Unguja ikiwa na lengo la kushinda mechi zote tatu za mashindano hayo ili kufikia fainali na kutetea ubingwa waliouchukua msimu uliopita. Kocha mkuu Pedro Goncalves ameweka wazi dhamira hiyo, akisisitiza kuwa kikosi chake kimekuja kuendeleza mafanikio ya msimu uliopita.
Akizungumza kuelekea mchezo huo, Pedro alisema timu yake haitadharau mpinzani yeyote licha ya ubora wao. Alibainisha kuwa anaifahamu changamoto ya kucheza dhidi ya timu za Zanzibar baada ya kushiriki Kombe la Mapinduzi 2026, ambapo aliiongoza Yanga kutwaa ubingwa.
Pedro alisema: “Tumefika hapa, kama ilivyo kawaida hii ni timu ambayo wakati wote inahitaji mafanikio, tumekuja kama bingwa mtetezi, tunataka kuendeleza yale ambayo tuliyafanya msimu uliopita.”
Aliongeza kuwa: “Najua namna ilivyo ngumu kushinda dhidi ya timu za hapa, hatuwezi kuchukulia rahisi timu ya Mwembe Makumbi.”
Kwa mujibu wa benchi la ufundi, Yanga imefika na kikosi kamili kwa ajili ya mashindano hayo, isipokuwa baadhi ya wachezaji waliobaki kutokana na sababu za kiufundi. Kocha huyo alisisitiza kuwa wachezaji waliopo wana uzoefu wa kucheza mechi za presha na wataingia uwanjani kwa umakini mkubwa.
| Yanga Sc | 4-0 | Maembe Makumbi |
- 🏆 #muunganocup
- Yanga 🆚 M/Makumbi
- 🗓️ 21 April 2026
- 🏟️ Amaan Complex
- ⏱️ 01:15 Usiku
17’ Prince Dube (Assisted by Okello)
34’ Frank Assinki (assisted by Shekhan)
38 Shekhan Khamis
57’ Prince Dube (assisted by Edmund)
Goli La Kwanza la Yanga Sc
View this post on Instagram
Katika muktadha wa Matokeo ya Yanga Vs Muembe Makumbi Leo 21/04/2026, mshindi wa mchezo huo atapewa nafasi ya kusonga mbele na kukutana na mshindi kati ya KVZ FC na Azam FC, ambao wanatarajiwa kucheza kesho Jumatano.
Hiki Apa Kikosi cha Yanga Kilichotangazwa Kuanza leo Dhidi ya Muembe Makumbi
Starting XI
- 39. Diarra (GK)
- 21. Yao
- 23. Boka
- 36. Assinki
- 4. Bacca
- 25. Damaro
- 26. Edmund
- 27. Mudathir
- 29. Dube
- 20. Okello
- 22. Sheikhan
Benchi: Masalanga, Abubakar, Kibwana, Abdulnasir, Andabwile, Faridi, Maxi, Pacome, Depu
Umuhimu wa mchezo huu ni mkubwa kwa Yanga, kwani ushindi leo utafungua njia ya kuelekea nusu fainali na hatimaye fainali. Ili kutetea ubingwa wao, wanahitaji ushindi katika kila hatua kuanzia mchezo huu wa kwanza.
Mashabiki wanatarajiwa kufuatilia kwa karibu Matokeo ya Yanga Vs Muembe Makumbi Leo 21/04/2026, ambao utaashiria mwanzo wa safari ya mabingwa watetezi katika Kombe la Muungano.
Kwa kumalizia, Yanga inaingia katika mchezo huu ikiwa na ari ya ushindi na malengo makubwa, huku Muembe Makumbi wakitarajiwa kutoa ushindani mkali katika uwanja wao wa nyumbani.
Mapendekezo ya Mhariri:








Leave a Reply