Kikosi cha Yanga Vs Muembe Makumbi Leo 21/04/2026
Kikosi cha Young Africans SC kinatarajiwa kushuka dimbani leo Jumanne kumenyana na Muembe Makumbi City katika mchezo wa Kombe la Muungano utakaopigwa Uwanja wa New Amaan Complex kuanzia saa 1:15 usiku. Mchezo huu wa Yanga Vs Muembe Makumbi ni sehemu ya safari ya mabingwa hao watetezi katika kulinda taji lao walilolitwaa msimu uliopita.
Yanga imewasili Unguja ikiwa na malengo makubwa ya kushinda mechi zote tatu za mashindano hayo ili kufikia hatua ya kutwaa ubingwa tena. Kocha mkuu Pedro Goncalves ameeleza wazi kuwa kikosi chake kipo tayari kwa changamoto hiyo, licha ya kukiri ugumu wa kucheza dhidi ya timu za Zanzibar.
Katika maandalizi ya Kikosi cha Yanga Vs Muembe Makumbi Leo 21/04/2026, Pedro amesema timu yake imefika ikiwa kamili isipokuwa baadhi ya wachezaji waliobaki kutokana na sababu za kiufundi. Ameongeza kuwa wachezaji waliopo wana uzoefu wa mechi za presha na wataingia uwanjani kwa umakini mkubwa kulingana na ubora wa mpinzani.
Hiki Apa Kikosi cha Yanga Kilichotangazwa Kuanza leo Dhidi ya Muembe Makumbi
Starting XI
- 39. Diarra (GK)
- 21. Yao
- 23. Boka
- 36. Assinki
- 4. Bacca
- 25. Damaro
- 26. Edmund
- 27. Mudathir
- 29. Dube
- 20. Okello
- 22. Sheikhan
Benchi: Masalanga, Abubakar, Kibwana, Abdulnasir, Andabwile, Faridi, Maxi, Pacome, Depu
Yanga inaingia kwenye mechi hiyo ikiwa juu ya msimamo wa Ligi Kuu Bara kwa tofauti ya pointi tano, hali inayoongeza morali ya kikosi hicho. Kocha huyo pia ana kumbukumbu nzuri ya mashindano ya visiwani, baada ya kushinda Kombe la Mapinduzi 2026 alipoiadhibu Azam FC katika fainali iliyochezwa Gombani Stadium Januari 13, 2026.
Hata hivyo, Yanga itamkosa kiungo Mudathir Yahya ambaye amefungiwa mechi tatu na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kufuatia tukio la kumpiga kiwiko mchezaji wa Pamba Jiji FC, Ibrahim Abraham, katika mchezo uliochezwa CCM Kirumba Stadium. Adhabu hiyo pia imeambatana na faini ya Sh1 milioni.
Mudathir amekuwa katika kiwango bora hivi karibuni akiwa na mabao saba kwenye ligi, akikaribia vinara wa ufungaji ambao ni Prince Dube na Fabrice Ngoy wenye mabao manane kila mmoja.
Kwa mujibu wa ratiba ya mashindano, mshindi wa mchezo huu wa Yanga Vs Muembe Makumbi Leo 21/04/2026 atakutana na mshindi wa pambano kati ya KVZ FC na Azam FC litakalopigwa kesho Jumatano.
Umuhimu wa mchezo huu ni mkubwa kwa Yanga, kwani inahitaji kushinda michezo mitatu mfululizo ili kufikia lengo la kutetea ubingwa wa Kombe la Muungano. Hii inaifanya mechi ya leo kuwa hatua ya kwanza muhimu katika safari hiyo.
Mashabiki wa soka wanapaswa kufuatilia kwa karibu mchezo huu wa Yanga Vs Muembe Makumbi Leo ili kushuhudia mwanzo wa mapambano ya ubingwa kwa mabingwa watetezi.
Kwa ujumla, Yanga inaingia uwanjani ikiwa na ari ya ushindi na dhamira ya kuendeleza mafanikio yao ya msimu uliopita, huku Muembe Makumbi wakitarajiwa kutoa upinzani mkali nyumbani.
Mapendekezo ya Mhariri:








Leave a Reply