Ajira Mpya za Walimu MDAs & LGAs 2025: Nafasi 3018 Zatangazwa October 16
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, kwa niaba ya Wizara, Idara, Wakala na Serikali za Mitaa (MDAs & LGAs), ametangaza rasmi tarehe 16 Oktoba 2025 jumla ya nafasi mpya 17,710 za ajira katika sekta mbalimbali za Serikali.
Kati ya nafasi hizo, nafasi 3,018 zimepangwa mahsusi kwa kada ya Mwalimu Daraja la IIIA, zikiwa ni sehemu ya ajira mpya zinazolenga kuimarisha utoaji wa elimu katika shule za msingi nchini Tanzania.
Tangazo hili limekuja kama sehemu ya utekelezaji wa mpango wa Serikali wa kuajiri watumishi wapya kwa mwaka wa fedha 2025/2026, ili kuongeza nguvu kazi katika taasisi za umma, hasa katika sekta nyeti za elimu, afya na utawala wa Serikali za Mitaa.
Kupitia ajira hizi, Serikali inalenga kuboresha uwiano wa walimu kwa wanafunzi, kuongeza ubora wa elimu na kutoa fursa kwa wahitimu wa vyuo vya ualimu kujiunga na utumishi wa umma kwa mara ya kwanza.
Kuhusu Nafasi za Mwalimu Daraja la IIIA
Nafasi hizi zimeandaliwa mahsusi kwa walimu waliohitimu mafunzo ya ualimu wa miaka miwili kutoka vyuo vinavyotambulika na Serikali, na ambao wamepata Cheti cha Ualimu Daraja la A. Wajibu wa walimu hawa ni kuhakikisha kuwa elimu bora inatolewa kwa wanafunzi katika shule za msingi kupitia ufundishaji, ushauri nasaha na usimamizi wa malezi ya kitaaluma na kijamii.
Majukumu ya Kazi ya Mwalimu Daraja la IIIA
Walimu watakaopata nafasi hizi watawajibika kutekeleza majukumu mbalimbali ya kitaaluma na kiutendaji kama ifuatavyo:
- Kuandaa mpango wa kazi, maandalio ya masomo, na nukuu za masomo kulingana na mtaala uliopo.
- Kutengeneza na kutumia zana za kufundishia na kujifunzia ili kuongeza ufanisi wa somo darasani.
- Kufundisha, kufanya tathmini za maendeleo ya wanafunzi, na kutunza kumbukumbu zao kitaaluma.
- Kusimamia mahudhurio ya wanafunzi darasani na kuhakikisha nidhamu na utaratibu vinafuatwa.
- Kutoa malezi na ushauri nasaha wa kiakili, kimwili na kiroho kwa wanafunzi ili kukuza maendeleo yao ya kijamii na kitabia.
- Kusimamia utunzaji wa vifaa na mali za shule kwa uadilifu.
- Kushiriki katika kufundisha Elimu ya Watu Wazima pale inapohitajika.
- Kufanya kazi nyingine zote zitakazopangwa na Mkuu wa Shule kulingana na majukumu ya taasisi husika.
Sifa za Muombaji wa Nafasi ya Mwalimu Daraja la IIIA
Waombaji wote wanapaswa kuwa na sifa zifuatazo:
- Awe Raia wa Tanzania mwenye umri usiozidi miaka 45.
- Awe amehitimu mafunzo ya ualimu kwa miaka miwili (2) kutoka chuo kinachotambulika na Serikali.
- Awe na Cheti cha Ualimu Daraja la A kinachotolewa na mamlaka husika.
- Awe na Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) kilichoidhinishwa na NECTA.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kuomba na wanatakiwa kueleza aina ya ulemavu wao kwenye mfumo wa maombi.
Nyaraka Muhimu za Kuambatisha Wakati wa Kuomba
Wakati wa kujaza fomu ya maombi kupitia mfumo wa kielektroniki wa Sekretarieti ya Ajira, waombaji wanapaswa kuambatisha nyaraka zifuatazo:
- CV ya kina (Detailed C.V) yenye anwani, namba za simu na majina ya wadhamini watatu (Referees).
- Cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
- Vyeti vya taaluma vilivyothibitishwa (Cheti cha Kidato cha Nne/Sita, Cheti cha Ualimu Daraja la A, n.k).
- Vyeti vya kitaaluma kutoka bodi husika (Professional Certificates).
- Waombaji waliomaliza masomo nje ya nchi lazima wawe wamehakikisha vyeti vyao na TCU, NECTA, au NACTE.
Kumbuka: Testmonials, Statement of Results, au Result Slips hazitakubalika kwa maombi haya.
Jinsi ya Kutuma Maombi ya Ajira Mpya za Walimu MDAs & LGAs 2025
Waombaji wote wanatakiwa kuwasilisha maombi yao kwa njia ya mtandao pekee kupitia mfumo wa kielektroniki wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kupitia tovuti:
Hakuna maombi yatakayopokelewa nje ya mfumo huu, na wale watakaotuma kwa njia nyingine hawatafanyiwa uchambuzi.
Barua ya maombi ya kazi inapaswa kuelekezwa kwa:
KATIBU,
Ofisi ya Rais,
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma,
S.L.P. 2320,
Mtaa wa Mahakama, Tambukareli,
DODOMA.
Masharti Muhimu ya Kazi
- Waombaji waliostaafishwa serikalini hawaruhusiwi kuomba, isipokuwa kama wana kibali maalum cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Wale walio kwenye utumishi wa umma kwa sasa hawapaswi kuomba nafasi hizi.
- Uwasilishaji wa taarifa za kughushi utasababisha hatua kali za kisheria.
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 29 Oktoba 2025.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Majina ya Waliochaguliwa Kusimamia Uchaguzi 2025
- Majina ya Waliochaguliwa Kusimamia Uchaguzi 2025 Kigamboni
- Nafasi Mpya za Kazi MDAs & LGAs October 2025
- Mfano Wa Barua Ya Kuomba Kazi Mwalimu Daraja La IIIA
- Mfano Wa Barua Ya Kuomba Kazi Afisa Muuguzi Msaidizi II
- Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili INEC 2025
- Posho na Malipo ya Wasimamizi wa Uchaguzi 2025
Leave a Reply