Al Al Ahly Vs Yanga Leo 23/01/2026 Saa Ngapi?
Timu ya Wananchi Yanga SC leo Ijumaa, Januari 23, wanashuka dimbani katika uwanja wa Cairo International Stadium, Misri, kuivaa miamba wa soka la Afrika Al Ahly SC katika mchezo wa tatu wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League). Hii ni moja ya mechi zinazovuta hisia kubwa barani Afrika kutokana na historia, hadhi na nafasi ya timu hizi katika michuano ya CAF.
Katika Kundi B, Yanga na Al Ahly wote wana alama nne baada ya kila mmoja kucheza mechi mbili, kushinda mchezo mmoja na kutoka sare moja. Hali hiyo imeifanya mechi ya leo kuwa ya ushindani mkubwa, kwani matokeo yake yataathiri moja kwa moja mwelekeo wa kundi hilo kuelekea hatua ya robo fainali.
Al Al Ahly Vs Yanga Leo 23/01/2026 Saa Ngapi?
Kwa mashabiki wengi wanatazamia kufuatilia mtanange huu wa Al Al Ahly Vs Yanga leo 23/01/2026 hapa chini ni taarifa kamili za mchezo
- Muda wa mechi: Saa 1:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki
- Uwanja: Cairo International Stadium, Misri
- Mashindano: Ligi ya Mabingwa Afrika – Hatua ya Makundi
- Matangazo ya moja kwa moja: Azam Sports 2 HD
Msimamo wa Kundi B Kabla ya Mechi
Baada ya raundi mbili za mwanzo:
- Yanga SC: pointi 4 (ushindi 1, sare 1)
- Al Ahly SC: pointi 4 (ushindi 1, sare 1)
Hii ina maana kuwa mshindi wa leo atajitengenezea mazingira mazuri kuelekea robo fainali, huku sare ikiacha ushindani wazi zaidi kwa mechi zijazo.
Yanga SC: Morali na Matokeo ya Awali
Yanga inaingia katika mchezo huu ikiwa na morali nzuri baada ya:
- Kushinda 1-0 nyumbani dhidi ya AS FAR Rabat ya Morocco
- Kutoka sare ya bila kufungana ugenini dhidi ya JS Kabylie ya Algeria
Matokeo hayo yamewapa wachezaji na benchi la ufundi imani ya kuendelea kupambana hata dhidi ya wapinzani wakubwa kama Al Ahly. Ingawa kihistoria Yanga haijawahi kupata ushindi ugenini dhidi ya Al Ahly, mchezo wa leo unaonekana kuwa fursa muhimu ya kuthibitisha ubora wa kikosi chao.
Al Ahly SC: Wababe wa Afrika Wakiwa Nyumbani
Al Ahly ni moja ya klabu zenye mafanikio makubwa zaidi barani Afrika. Kucheza nyumbani Cairo ni faida kubwa kwao, lakini ukweli kwamba Yanga ina pointi sawa nao unaongeza presha kwa wenyeji. Al Ahly wanajua kuwa kupoteza pointi nyumbani kunaweza kuwagharimu katika mbio za kusonga mbele.
Mapendekezo ya Mhariri:








Leave a Reply