Al Hilal VS Yanga Leo 12/01/2025 Saa Ngapi? | Muda wa Mechi ya Yanga na Al Hilal Leo Klabu Bingwa
Al Hilal VS Yanga Leo 12/01/2025 Saa Ngapi?
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania, Yanga SC, leo watashuka dimbani kuendelea kuisaka tiketi ya kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika (TotalEnergies CAF Champions League). Timu hiyo itakuwa wageni wa Al Hilal Omdurman ya Sudani kwenye Uwanja wa Cheikha Ould Boïdiya uliopo Nouakchott, Mauritania, mechi itakayoanza saa 1:00 usiku kwa saa za Mauritania (sawa na saa 4:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki).
Taarifa za Mechi ya AL Hilal VS Yanga Leo
- Michuano: TotalEnergies CAF Champions League (Raundi ya Tano – Hatua ya Makundi)
- Timu: Al Hilal vs Young Africans SC
- Tarehe: Jumapili, 12 Januari 2025
- Uwanja: Cheikha Ould Boïdiya, Nouakchott, Mauritania
- Muda: Saa 1:00 usiku (Mauritania), Saa 4:00 usiku (Tanzania)
Msimamo wa Kundi A
Yanga SC kwa sasa inashika nafasi ya tatu kwenye Kundi A, ikiwa na pointi nne baada ya mechi nne. Timu hiyo ilianza kwa kupoteza mechi mbili za mwanzo dhidi ya Al Hilal (2-0) na MC Alger (2-0), kabla ya kuzinduka na kupata sare ya 1-1 ugenini dhidi ya TP Mazembe na baadaye kuifunga TP Mazembe 3-1 jijini Dar es Salaam. Ushindi katika mechi ya leo ni muhimu kwa Yanga ili kufikisha pointi saba na kujiweka katika nafasi nzuri ya kuwania kufuzu hatua ya robo fainali.
Kwa upande wa Al Hilal, tayari wamefuzu hatua ya robo fainali wakiwa na pointi 10. Hata hivyo, bado wanahitaji ushindi ili kumaliza wakiwa vinara wa kundi na kujihakikishia faida ya kucheza na mshindi wa pili wa makundi mengine kwenye hatua ya robo fainali.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Rachid Taoussi Apania Kushusha Nyota Zaidi Dirisha Dogo
- Timu Zilizofuzu Robo Fainali Klabu Bingwa Afrika 2024/2025
- AS Vita Yamnyakua Dennis Modzaka Kutoka Coastal Union
- Rabbin Sanga Ajiunga na Tanzania Prisons Kwa Mkopo
- Robert Matano Ateuliwa Kuwa Kocha Mkuu wa Fountain Gate FC
- Msimamo wa Kundi la Yanga Klabu Bingwa Afrika CAF 2024/2025
- Mazembe Yaondolewa Ligi ya Mabingwa na MC Alger Baada ya Kipigo cha 1-0
- Bao la Inzaghi Laipa Zanzibar Heroes Tiketi ya Fainali Kombe la Mapinduzi
- CV ya Jonathan Djogo Kapela: Winga Mpya wa Yanga SC
Leave a Reply