Al Hilal ya Ibenge Yabeba Kombe la Ligi Kuu Mauritania 2024/25

Al Hilal ya Ibenge Yabeba Kombe la Ligi Kuu Mauritania 2024/25

Timu ya Al Hilal kutoka Sudan chini ya kocha Florent Ibenge, iliyoshiriki Ligi Kuu ya Mauritania kwa msimu wa 2024/25 kama mgeni, imetangazwa mabingwa wa heshima (honorary champions) wa ligi hiyo ikiwa bado na mechi mbili mkononi. Ushiriki huu ulitokana na hali ya kutokuwa na usalama nchini Sudan, hali iliyosababisha kusimamishwa kwa mashindano ya ndani.

Al Hilal ya Ibenge Yabeba Kombe la Ligi Kuu Mauritania 2024/25

Sababu ya Al Hilal kucheza Ligi Kuu ya Mauritania

Kutokana na mzozo unaoendelea Sudan na kusitishwa kwa michezo ya ndani, Shirikisho la Soka la Mauritania liliwasilisha ombi maalum kwa FIFA na CAF kuruhusu klabu za Al Hilal na Al Merrikh kushiriki Ligi Kuu ya Mauritania. Ombi hilo lilikubaliwa kwa misingi ya kipekee, na vilabu hivyo viwili kutoka Sudan vikaanza kushiriki ligi hiyo kwa msimu mmoja ili kuendelea kuwa katika hali ya ushindani.

Al Hilal imecheza jumla ya mechi 28 kati ya 30 zilizopangwa msimu huu, ikishinda michezo 18, kutoa sare 8 na kupoteza 2. Klabu hiyo imekusanya jumla ya pointi 62. Katika mchezo wa mwisho waliocheza hadi sasa, walipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya ASC Gendrim. Mabao hayo yalifungwa na Ahmed Salem pamoja na Aime Tendeng.

Ushindani na FC Nouadhibou

Licha ya mafanikio ya Al Hilal, mabingwa rasmi wa Ligi Kuu ya Mauritania msimu wa 2024 ni FC Nouadhibou. Timu hiyo ilishinda mechi yake ya 29 dhidi ya Inter Nouakchott kwa mabao 2-0, na kufikisha pointi 58. Hata hivyo, hata ikishinda mchezo wake wa mwisho, haitafikia pointi 62 za Al Hilal. Hii ndiyo sababu Al Hilal imetambuliwa kama mabingwa wa heshima wa ligi hiyo.

Al Merrikh ya Sudan katika nafasi ya sita

Klabu ya Al Merrikh, ambayo pia ilialikwa kushiriki Ligi Kuu ya Mauritania, inashikilia nafasi ya sita katika msimamo wa ligi kwa sasa. Imecheza mechi 29 na kuvuna pointi 44, huku ikiwa na mchezo mmoja wa mwisho kusalia. Ingawa haijashinda taji, bado itawakilisha Sudan katika mashindano ya klabu ya CAF msimu ujao.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Kevin De Bruyne Atajwa Kujiunga na Mabingwa wa Serie A Napoli
  2. Mac Allister Awindwa Kuziba Pengo la Modric Real Madrid
  3. Mbappé Ashinda Tuzo ya Mfungaji Bora Ulaya na La Liga kwa Mwaka 2024/25
  4. Simba Yapokewa Dar kwa Shangwe Kubwa Baada ya Mtanange Mkali Zanzibar
  5. Rs Berkane Yabeba Ubingwa Kombe la Shirikisho Afrika 2024/2025
  6. Ndoto ya Ubingwa Shirikisho ya Simba Yazimwa Baada ya Sare Amaan Complex
  7. Rais Mwinyi Aahidi Mamilioni Kwa Simba Wakishinda Kombe la Shirikisho
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo