Awesu na Onana Watua Misri Kujiunga na Kambi ya Mazoezi ya Simba
Msimu mpya wa soka Tanzania unakaribia kwa kasi, na klabu kongwe ya Simba SC ipo katika kambi maalumu kwa ajili ya maandalizi ya Msimu mpya. Huku gumzo la usajili wa kiungo Awesu Ali Awesu likiendelea kutawala vichwa vya habari, nyota huyo mwenye uwezo wa hali ya juu ametua rasmi nchini Misri kujiunga na kambi ya mazoezi ya Wekundu wa Msimbazi.
Awesu, kiungo mshambuliaji aliyejizolea umaarufu mkubwa akiwa na Madini FC, amewasili Misri akiwa ameambatana na kiungo mshambuliaji, Willy Essomba Onana. Wawili hawa wanatarajiwa kuongeza nguvu na ubunifu katika safu ya kiungo ya Simba, na kuwapa mashabiki matumaini ya msimu wenye mafanikio makubwa.
Usajili wa Awesu umeambatana na utata fulani, huku klabu ya KMC FC ikidai kuwa bado ina mkataba halali na mchezaji huyo. Hata hivyo, Simba SC imeonekana kutojali malalamiko hayo na inaendelea kuweka nguvu zake katika maandalizi ya msimu mpya.
Kambi ya mazoezi ya Simba SC mjini Ismailia, Misri, ni sehemu ya mkakati wa klabu hiyo kujenga timu imara na yenye ushindani. Wachezaji wanapata mazoezi ya hali ya juu, mikakati mipya, na fursa ya kuimarisha umoja wao kama timu.
Awesu Awesu akizungumzia siku yake ya kwanza ya mazoezi akiwa Msimbazi.
Taarifa zaidi tumia Simba App na Simba Bando inayokupa dakika za kupiga, sms, data na mastori ya Simba bure. Kujiunga Simba Bando piga *149*01# > 7 > 1. #WenyeNchi #NguvuMoja pic.twitter.com/Z662DlQiM6
— Simba Sports Club (@SimbaSCTanzania) July 19, 2024
Mapendekezo ya Mhariri:
Weka Komenti