Bei ya Iphone 16 Tanzania ( Iphone 16 Price in Tanzania)
Kampuni ya Apple imetangaza rasmi toleo jipya la simu zake maarufu iPhone 16, ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa bidhaa zake zenye teknolojia ya hali ya juu. Simu hii imefanyiwa maboresho kadhaa ambayo yanatarajiwa kuhamasisha wapenzi wa simu janja kununua toleo hili jipya la simu, hasa kwa wale ambao wamekuwa wakitumia toleo la zamani kwa muda mrefu. Nchini Tanzania, bei ya iPhone 16 itategemea mambo kadhaa kama vile gharama za usafirishaji, kodi, na mtandao wa maduka yanayouza bidhaa za Apple.
Bei ya iPhone 16 Tanzania
Kwa mujibu wa uzinduzi rasmi wa Apple, bei ya iPhone 16 inaanzia $799, ambayo ni takriban TZS 2,000,000 kulingana na kiwango cha ubadilishaji wa fedha hii leo tarehe 10 septemba 2024.
Hata hivyo, bei hii inaweza kupanda zaidi kutokana na gharama za kuagiza bidhaa nje na kodi za forodha. Watumiaji wa iPhone 16 Plus, ambayo ina ukubwa mkubwa wa skrini, watahitaji kulipa zaidi, kwani inauzwa kwa bei ya kuanzia $899, sawa na takriban TZS 2,250,000.
Kwa upande wa toleo la iPhone 16 Pro, bei inaanzia $999 (karibu TZS 2,500,000), wakati toleo la juu kabisa, iPhone 16 Pro Max, linauzwa kwa bei ya kuanzia $1,199 (karibu TZS 3,000,000).
Tofauti ya bei kati ya matoleo haya inatokana na maboresho ya teknolojia na vipengele vilivyoongezwa katika kila toleo.
Mapendekezo ya Mhariri:
Weka Komenti