Chelsea Yajipanga Kuzima Moto wa Di Maria Katika Mechi ya Usiku Dhidi ya Benfica
Chelsea imemtaja mshambuliaji matata wa Benfica, Angel Di Maria, kama tishio kubwa katika pambano lao la hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia la Klabu linalotarajiwa kupigwa leo usiku katika Uwanja wa Bank of America, Charlotte, Marekani.
Mchezo huo mkubwa unatarajiwa kuanza saa 5:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki, huku mshindi akitarajiwa kuvaana na atakayeshinda kati ya Palmeiras dhidi ya Botafogo kwenye robo fainali.
Licha ya Di Maria kuwa na umri wa miaka 37, Chelsea imesisitiza kuwa bado ni miongoni mwa wachezaji wenye ushawishi mkubwa uwanjani. Meneja wa klabu hiyo, Enzo Maresca, amefichua kuwa wamekuwa wakifuatilia kwa ukaribu uwezo wa Di Maria, hasa katika mechi ya Benfica dhidi ya Bayern Munich, ambapo alionyesha kiwango cha juu mno.
“Di Maria anaonyesha namna gani alivyo mchezaji mkubwa. Ni mchezaji wa daraja la juu. Nimeona mechi zake katika mashindano haya… nahisi alikuwa mchezaji bora wa mechi dhidi ya Bayern. Tunatakiwa kuwa na angalizo kwake,” amesema Maresca.
Levi Colwill: Di Maria Hatakiwi Kuachiwa Nafasi
Katika kuhakikisha Chelsea yajipanga kuzima moto wa Di Maria, beki wa kati Levi Colwill amesema kwa uwazi kuwa mchezaji huyo wa Argentina ni hatari na hatakiwi kuachiwa nafasi hata kidogo. Colwill, ambaye amekuwa nguzo muhimu katika safu ya ulinzi ya Chelsea, amesisitiza kuwa wanapaswa kuwa makini zaidi na mguu wa kushoto wa Di Maria.
“Hapana shaka ni mchezaji wa kipekee ambaye wakati nakua nilikuwa namtazama. Uwezo wake wa kiufundi ni wa kushangaza. Natumaini tutaudhibiti mguu wake wa kushoto na tunatumaini hatofunga bao lolote dhidi yetu,” amesema Colwill.
Kauli hiyo inaonyesha namna ambavyo Chelsea imejiandaa kwa kina kumdhibiti Di Maria, ambaye tayari ameshapachika mabao matatu kwenye mashindano haya moja dhidi ya Boca Juniors na mengine mawili dhidi ya Auckland City.
Pamoja na umri wake mkubwa, Di Maria bado anaonesha kiwango cha juu, akitumia uzoefu wake na ustadi wa kiufundi kuwasumbua walinzi wa timu pinzani. Uwepo wake ndani ya kikosi cha Benfica umeleta msisimko mkubwa katika mashindano haya, na Chelsea haitaki kurudia makosa ya timu zilizotangulia.
Meneja Maresca na safu yake ya benchi la ufundi wameweka mikakati mahsusi kuhakikisha wanamzuia mshambuliaji huyo mwenye sifa za kipekee – ikiwa ni pamoja na kumwekea ulinzi wa karibu, kuzuia pasi zinazomfikia, na kudhibiti mipira ya hatari.
Matarajio Kabla ya Mchezo
Mashabiki wa soka duniani wanaisubiri kwa hamu mechi hii kali kati ya Chelsea na Benfica. Huku Chelsea ikijipanga kuzima moto wa Di Maria, upande wa Benfica nao utakuwa ukimtegemea kwa kiwango kikubwa kuleta ushindi.
Kwa mujibu wa takwimu za awali, mechi hii inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa hasa ikizingatiwa kuwa mshindi atasonga mbele kwenye hatua ya robo fainali ambapo ushindani huwa mkali zaidi.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Timu Zilizofuzu Hatua ya 16 Bora Kombe la Dunia la Vilabu 2025
- Wydad Casablanca Yafungashiwa Virago Kombe la Dunia Bila Pointi
- Asante Kotoko Yachukua Nafasi ya Yanga Kombe la Toyota Afrika Kusini
- Milos Kerkez Ajiunga Rasmi na Liverpool kwa Ada ya Pauni Milioni 40
- Christian Eriksen Aondoka Man United Baada ya Utumishi wa Miaka Mitatu
- Kikosi cha Tanzania CHAN 2024: Wachezaji Kuingia Kambini Julai 7, 2025
- Yanga Yailaza Simba 2-0 na Kutwaa Kombe la Ligi Kuu Kwa Mara ya 31
- Vituo Vya Tiketi Mechi ya Yanga Vs Simba 25/06/2025
Leave a Reply