Timu Iliyopangwa na Yanga Klabu Bingwa CAF 2024/2025 | Timu Iliyopangiwa Yanga CAF Champions LeagueÂ
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limefanya droo ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika kwa msimu wa 2024/2025. Tanzania imewakilishwa na timu kadhaa zenye uwezo mkubwa, zikiwemo Yanga SC, Azam FC, Simba SC, na Coastal Union. Makala hii itajadili kwa kina jinsi droo ilivyopangwa na matarajio ya Yanga SC katika michuano hii.
Timu Iliyopangwa na Yanga Klabu Bingwa CAF 2024/2025; Klabu Bingwa Afrika
Katika hatua ya awali ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika, Yanga SC imepangwa kucheza dhidi ya Vital’O ya Burundi. Mechi ya kwanza itachezwa ugenini, ambapo Yanga itasafiri kwenda Burundi, kabla ya kurudi nyumbani kwa mechi ya marudiano.
Kama mabingwa wa soka Tanzania Yanga SC watafanikiwa kuvuka hatua hii ya ufunguzi wa michuano ya mechi za awali za klabu bingwa, watakutana na mshindi kati ya SC Villa ya Uganda na Commercial Bank ya Ethiopia katika hatua ya pili.
Maandalizi ya Yanga SC
Kuelekea michuano hii, Timu ya wananchi Yanga SC imeweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha wanapata matokeo mazuri. Timu imejipanga kwa mazoezi ya nguvu na mikakati kabambe ili kuhakikisha wanapambana vilivyo katika kila mechi. Kocha wa Yanga SC amesisitiza umuhimu wa kuanza vyema katika mechi za ugenini ili kujipa nafasi nzuri ya kusonga mbele.
Ratiba ya Mechi Za Awali Klabu Bingwa Afrika
Mechi za mkondo wa kwanza wa hatua ya awali zitapigwa kati ya Agosti 16 na 18, 2024, huku marudiano yakitarajiwa kufanyika kati ya Agosti 22 na 25, 2024. Hii inatoa muda wa kutosha kwa timu kujiandaa na kurekebisha makosa yatakayojitokeza katika mechi za mwanzo.
Katika hatua ya pili, mechi za mkondo wa kwanza zitapigwa kati ya Septemba 13 na 15, 2024, na marudiano yatapigwa kati ya Septemba 20 na 22, 2024. Yanga SC inatarajia kufika mbali katika michuano hii kwa kuonyesha kiwango bora cha soka.
Mapendekezo Ya Mhariri:
- Matokeo Mechi za CECAFA Dar Port Kagame Cup 2024
- Makundi ya Dar Port Kagame CECAFA Cup 2024
- Stephane Aziz Ki Asaini Mkataba Mpya na Yanga SC
- Rasmi: Simba SC Yamtema Sadio Kanoute
- Yanga Yamsajili Rasmi Aziz Andabwile: Mkataba wa Miaka miwili, Kiungo Mpya Jangwani
- Wachezaji Wapya Yanga | Wachezaji Waliosajiliwa Yanga 2024/2025
Weka Komenti