CV ya Naby Camara Beki Mpya Simba 2025/26
Klabu ya Simba SC imekamilisha usajili wa mchezaji kiraka, Naby Camara, raia wa Guinea. Camara anasifika kwa uwezo mkubwa wa kucheza nafasi nyingi uwanjani ikiwemo beki wa kushoto, kiungo wa kati (namba 6), namba 10 pamoja na winga wa kushoto.
Usajili huu umeongeza nguvu mpya kwenye kikosi cha Wekundu wa Msimbazi kuelekea msimu wa mashindano ya Ligi Kuu NBC 2025/26 na michuano ya kimataifa ya CAF. Naby Camara amejipatia jina la utani “Messi” kutokana na uchezaji wake wa kiufundi, ubunifu na uwezo wa kudhibiti mchezo. Sifa hii imewafanya mashabiki wengi kuamini kuwa ataongeza ladha ya kipekee kwenye kikosi cha Simba.
Taarifa Binafsi za Naby Camara
- Jina kamili: Naby Camara
- Tarehe ya kuzaliwa: 03 Desemba 2001
- Umri: Miaka 23 (2025)
- Urefu: 1.77m
- Raia: Guinea
- Mguu anaotumia zaidi: Kushoto
- Nafasi anazocheza: Kiungo wa kati, beki wa kushoto, namba 10, na winga wa kushoto
- Klabu ya sasa: Simba SC (alijiunga Agosti 14, 2025)
Safari ya Kimpira na Historia ya Usajili
Kabla ya kujiunga na Simba SC, Naby Camara alicheza kwenye klabu kadhaa barani Afrika na Kati ya Mashariki:
- 2019/20 – Alihudumu katika kikosi cha vijana cha CS Sfaxien U21 (Tunisia).
- 2020/21 – Aliendelea kuonesha kiwango kizuri na kupandishwa kwenye kikosi cha wakubwa cha CS Sfaxien.
- 2023/24 – Aliondoka CS Sfaxien na kujiunga na Al-Waab SC ya Qatar.
- 2025/26 – Baada ya kuachana na Al-Waab SC, Camara alikuwa bila klabu kwa muda mfupi kabla ya kusajiliwa na Simba SC.
Kulingana na takwimu za thamani ya soko, wakati anaondoka Al-Waab SC thamani yake ilikuwa karibu €350k, ishara kuwa bado ni mchezaji mwenye thamani kubwa katika soka la kimataifa.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Ratiba ya Mechi za Leo 16/08/2025 CHAN
- Sifa za Kujiunga na Jeshi la Magereza Tanzania 2025
- Rayon Sports vs Yanga Leo 15/08/2025 Saa Ngapi?
- Kikosi cha Yanga vs Rayon Sports Leo 15/08/2025 Mechi ya Kirafiki
- Matokeo ya CHAN 2025 Kundi La Tanzania (Kundi B)
- Azam FC Yamwaga Mamilioni Ili Kumbakiza Nyota Wake Fei Toto
- Ratiba ya Mechi za Leo 14/08/2025 CHAN
- Ifahamu Gaborone United Wapinzani wa Simba Ligi ya Mabingwa CAF 2025/2026
- Makundi ya CHAN 2025 Yatangazwa
Leave a Reply