Vilabu Bora Afrika 2024/2025 (CAF Club Ranking)

Vilabu Bora Afrika 2024/2025 (CAF Club Ranking) | Rank za vilabu Afrika 2024

Wakati mashabiki wa vilabu vya soka barani Afrika wakisubiri kuanza kwa msimu mpya wa 2024/2025, klabu ya Al Ahly kutoka Misri imeendelea kushikilia nafasi ya kwanza kwenye orodha ya vilabu bora Afrika. Al Ahly, ambao wana historia ndefu ya mafanikio katika ulimwengu wa soka la Afrika, wameweza kushikiria nafasi yao kama klabu bora zaidi barani Afrika kutokana na mafanikio yao ya mara kwa mara katika michuano ya klaby bingwa ya CAF (CAF Champions league).

Klabu ya Esperance ya Tunisia imepanda hadi nafasi ya pili, ikipita Wydad Athletic Club ya Morocco baada ya kufanikiwa kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) msimu wa 2023/2024. Wydad, ambao walikuwa kwenye nafasi ya pili, wameporomoka hadi nafasi ya tatu baada ya kushindwa kufuzu kutoka kwenye hatua ya makundi ya michuano ya CAF kwa msimu huo.

Mamelodi Sundowns kutoka Afrika Kusini imeendelea kushikilia nafasi ya nne, lakini inatarajiwa kushuka zaidi katika msimamo wa CAF kutokana na kushindwa kufuzu kwa michuano ya 2024/2025. Hii inaweza kuwa na matokeo kama yale yaliyoikumba klabu ya Raja Club Athletic ya Morocco, ambayo ilishuka kutoka nafasi ya tano hadi nafasi ya 12 baada ya kukosa kushiriki michuano ya CAF msimu uliopita.

Vilabu vingine vilivyo kwenye nafasi za juu katika msimamo wa Vilabu Bora Afrika 2024/2025 (CAF Club Ranking) ni pamoja na Zamalek ya Misri, RS Berkane ya Morocco, wekundu wa msimbazi Simba SC kutoka Tanzania, Petro de Luanda ya Angola, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DR Congo), na CR Belouizdad ya Algeria.

Vilabu Bora Afrika 2024/2025 (CAF Club Ranking)
Rank za vilabu afrika 2024

Orodha ya Vilabu Bora Afrika kwa Msimu wa 2024/2025

NafasiClub2020–212021–222022–232023–242024–25Jumla
(× 1)(× 2)(× 3)(× 4)(× 5)
1Al Ahly6566≥158
2Tunisia Espérance4345≥147
3South Africa3344≥142
4Wydad AC4652039
5Zamalek2225≥0.534.5
6CR Belouizdad3332≥131
7Democratic Republic230.54≥130.5
8RS Berkane1504≥0.529.5
9Simba3233≥0.530.5
10Young Africans0043≥129
11USM Alger0053027
11Angola Petro1423027
13Raja CA5330≥125
14Ivory Coast0133023
15Pyramids3221≥122
16Al-Hilal1122017
17South Africa2400≥115
18Rivers United0022014
19JS Kabylie4030013
20Dreams FC0003012
21Stade Malien0002≥0.510.5
22Horoya2120010
23Future000.5209.5
24Tunisia Étoile120109
24ES Sétif140009
24South Africa003009
27FC Nouadhibou000208.5
27Abu Salim000208
27MC Alger3000≥18
30CS Sfaxien2100≥0.56.5
31Coton Sport30.51007
32Jwaneng Galaxy010106
32Sagrada Esperança010106
32Al-Merrikh111006
32Libya Al030006
32ASFAR Rabat002006
32US Monastir002006
38Republic of0010.505
38Democratic Republic201005
38Kaizer Chiefs500005

Simba na Yanga Kwenye Viwango Vya Ubora CAF

Simba na Yanga Kwenye Viwango Vya Ubora CAF

Jinsi Ambavyo Viwango Hivi Vimepangwa

Kwa msimu wa 2024/2025, alama zilizotumika kupangilia vilabu bora barani Afrika zimekusanywa kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, yaani kuanzia 2019 hadi 2024. Alama zilizokusanywa kwa msimu wa 2023/2024 zimepewa uzito mkubwa zaidi, zikiwa zimezidishwa mara tano, wakati msimu wa 2022/2023 alama zake zimezidishwa mara nne, na msimu wa 2021/2022 mara tatu, msimu wa 2020/2021 mara mbili, na msimu wa 2019/2020 mara moja.

Mshindi wa Ligi ya Mabingwa Afrika hupata alama sita, ambapo Al Ahly wamepata alama 30 (6×5) kwa msimu wa 2023/2024. ES Tunis waliomaliza kama washindi wa pili walipata alama tano na hivyo kupata jumla ya alama 25 (5×5). Vile vile, vilabu vilivyofika hatua ya nusu fainali kama ASEC Mimosas na Mamelodi Sundowns vilipata alama nne, huku robo fainali zikipatiwa alama tatu, na timu zilizomaliza nafasi ya tatu kwenye makundi zikipewa alama mbili, na nafasi ya nne zikipata alama moja.

Kwa upande wa Kombe la Shirikisho la CAF, mshindi hupata alama tano, ambapo Zamalek walipata alama 25 (5×5). Washindi wa pili RS Berkane walipata alama nne na hivyo kufikisha alama 20 (4×5).

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Vilabu Bora Afrika 2023/2024 (IFFHS Club Ranking)
  2. Ratiba Kamili ya UEFA Euro 2024 Hatua Ya 16 Bora
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo