Dodoma Jiji Fc vs Tabora United Leo 02/10/2024 Saa Ngapi?
Leo tarehe 02 Oktoba 2024, mashabiki wa soka nchini watashuhudia mechi kali ya soka kati ya Dodoma Jiji FC na Tabora United. Mchezo huu wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara (NBC Premier League) unatarajiwa kutimua vumbi katika viunga vya Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, makao makuu ya nchi. Je, mechi hii itachezwa saa ngapi na ni nini cha kutarajia?
Saa na Mahali pa Mechi
- Tabora Unitedπ Dodoma Jiji Fc
- π Ligi Kuu ya NBC (#NBCPL)
- π Uwanja wa Jamuhuri, Dodoma.
- π 02.10.2024
- π 01:00 Usiku
- πΊ Itaoneshwa na #AzamSports1HD
- π» Itatangazwa na #TBCFM
Mchezo huu utaanza rasmi majira ya saa 1:00 usiku (19:00 EAT), kwenye Uwanja wa Jamhuri, ambao unatumiwa kama uwanja wa nyumbani wa Dodoma Jiji FC. Kwa wapenzi wa soka ambao hawatakuwa na nafasi ya kufika uwanjani, hakikisha unafuatilia matangazo ya moja kwa moja kwenye televisheni au kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kwa matokeo ya papo kwa papo.
Dodoma Jiji FC inakutana na Tabora United ikiwa na kumbukumbu ya mchezo wa msimu uliopita ambapo walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0, bao hilo likifungwa na mshambuliaji wao Hassan Mwaterema. Hali hii inawapa matumaini ya kuendelea kudumisha ubora wao nyumbani, hasa kwenye uwanja wa Jamhuri.
Kwa upande mwingine, Tabora United inaingia katika mchezo huu baada ya kupoteza mchezo wao wa hivi karibuni dhidi ya Fountain Gate kwa mabao 3-1. Hali hii inaweza kuwa changamoto kwao, lakini pia motisha ya kurekebisha makosa yao na kurudi kwa nguvu zaidi katika mechi hii ya ugenini.
Hali ya Timu Kabla ya Mechi
Katika michezo mitano ya hivi karibuni, Dodoma Jiji na Tabora United zote zimepoteza mara moja tu kwenye michezo yao ya ligi. Dodoma Jiji ilifungwa na Simba SC kwa bao 1-0, wakati Tabora United wakipoteza dhidi ya Fountain Gate. Ingawa timu zote zimekuwa na matokeo mchanganyiko, mechi hii inatoa fursa kwa kila moja kujiimarisha zaidi kwenye msimamo wa ligi.
Matarajio ya Mashabiki na Uchambuzi
Mashabiki wa Dodoma Jiji FC wana matumaini kuwa timu yao itatumia vyema faida ya kucheza nyumbani na kurekebisha makosa ya mchezo uliopita dhidi ya Simba. Wengi wanategemea kuona mchezo wa kasi, mbinu za hali ya juu, na ulinzi imara ili kuhakikisha ushindi unapatikana.
Tabora United kwa upande wao watakuwa na kazi ya kujibu mashambulizi na kutafuta matokeo mazuri kwenye uwanja wa ugenini, jambo ambalo si rahisi lakini linawezekana. Kwa kuzingatia kuwa ligi bado ipo katika hatua za awali, kila pointi ina umuhimu mkubwa kwa timu zote mbili.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Acheni Kulewa Sifa β Kocha Coastal Union Awachana Chipukizi
- Bado Niponipo Sana tu- Jibu la Tshabalala Kuhusu Kustaafu
- Kikosi cha Fountain Gate FC 2024/2025
- Kikosi cha Tanzania Prisons 2024/2025
- Wachezaji Wa Yanga Walioitwa Timu ya Taifa October 2024
- Wachezaji Wa Simba Walioitwa Timu ya Taifa October 2024
Weka Komenti