Droo ya Klabu Bingwa Afrika 2025/2026 CAF: Timu & Ratiba Ya Round ya Awali
Mashindano ya Klabu Bingwa Afrika (CAF Champions League) msimu wa 2025/2026 yamezinduliwa rasmi kwa kufanyika kwa droo ya Raundi ya Awali, ikifungua ukurasa wa kwanza wa safari ya kusaka taji kubwa zaidi la soka la vilabu barani Afrika.
Droo hiyo imeweka wazi wapinzani wa timu 60 zilizofuzu hatua ya awali, huku mechi zikitarajiwa kuchezwa kwa mikondo miwili kuanzia tarehe 19–21 Septemba na marudiano tarehe 26–28 Septemba 2025.
Timu zitakazoshinda katika hatua hii zitapiga hatua kwenda Raundi ya Pili ya Mchujo itakayofanyika katikati ya mwezi Oktoba, hatua ambayo itakaribisha vigogo wawili wa soka barani Al Ahly ya Misri na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini ambao wamepatiwa mapumziko ya hatua ya kwanza kutokana na nafasi zao za juu kwenye viwango vya CAF.
Wapeperusha Bendera ya Tanzania na Ratiba Zao
Katika droo hii, Tanzania imewakilishwa na miamba miwili ya soka ambayo ni timu ya wananchi Yanga SC na wekundu wa msimbazi Simba SC, ambao wote wamepangwa kuanzia Raundi ya Awali kwa mechi za kwanza ugenini.
- Yanga SC watakabiliana na Wiliete Benguela ya Angola.
- Simba SC wao watavaana na Gaborone United ya Botswana.
Kwa upande wa Kombe la Shirikisho Afrika, Azam FC imepangwa kuanza dhidi ya Al Merriekh ya Sudan, huku Singida Black Stars wakikabiliana na Rayon Sports ya Rwanda inayoongozwa na kocha wa zamani wa Simba, Robertinho Oliveira.
Msimu uliopita, Yanga iliishia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, huku Azam FC ikijikuta ikitolewa mapema kwenye hatua ya awali ya Kombe la Shirikisho. Simba, licha ya historia yao nzuri katika michuano ya CAF, walimaliza kama washindi wa pili kwenye Kombe la Shirikisho baada ya kuchechezea kichapo kutoka kwa RS Berkane.
Kwa Singida Black Stars, hii ni mara yao ya kwanza kushiriki mashindano ya kimataifa, wakiendeleza nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Coastal Union. Wamekuwa wakitarajiwa kufanya vyema kutokana na uwekezaji mkubwa walioufanya, pamoja na uongozi wa Kocha Miguel Gamondi ambaye aliifikisha Yanga hatua ya makundi msimu uliopita.
Orodha ya Mechi Zote za Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika 2025/2026
- Ethiopian Insurance (Ethiopia) vs Mlandege (Zanzibar)
- APR FC (Rwanda) vs Pyramids FC (Egypt)
- Mogadishu City (Somalia) vs Kenya Police (Kenya)
- Jamus FC (South Sudan) vs Al Hilal (Sudan)
- Rahimo FC (Burkina Faso) vs Mangasport (Gabon)
- AS FAN (Niger) vs Espérance (Tunisia)
- Dadje FC (Benin) vs Libya 1 (Libya)
- ASCK (Togo) vs RS Berkane (Morocco)
- East End Lions (Sierra Leone) vs US Monastir (Tunisia)
- Goldstars (Ghana) vs JS Kabylie (Algeria)
- Fundacion Bata (Equatorial Guinea) vs Nouadhibou (Mauritania)
- AS Tempete (CAR) vs Stade Malien (Mali)
- Libya 2 (Libya) vs Horoya AC (Guinea)
- DR Congo 2 (DR Congo) vs Al Merriekh (Sudan)
- Colombe Sportive (Cameroon) vs ASC Jaraaf (Senegal)
- FC Fassell (Liberia) vs MC Alger (Algeria)
- Remo Stars (Nigeria) vs Zilimadjou (Comoros)
- Simba Bhora (Zimbabwe) vs Nsingizini Hotspurs (Eswatini)
- Gaborone United (Botswana) vs Simba SC (Tanzania)
- Elgeco Plus (Madagascar) vs Silver Strikers (Malawi)
- Wiliete Benguela (Angola) vs Yanga SC (Tanzania)
- Cote d’Or (Seychelles) vs Stade d’Abidjan (Ivory Coast)
- Cercle Joachim (Mauritius) vs Petro Atletico (Angola)
- AC Leopards (Congo) vs Black Bulls (Mozambique)
- DR Congo 1 (DR Congo) vs Rivers United (Nigeria)
- African Stars (Namibia) vs Vipers SC (Uganda)
- Power Dynamos (Zambia) vs ASEC Mimosas (Ivory Coast)
- Lioli FC (Lesotho) vs Orlando Pirates (South Africa)
Mapendekezo ya Mhariri:
- Mshahara wa Celestin Ecua Yanga 2025/2026
- Msimamo Kundi la Tanzania CHAN 2024
- Mohamed Hussein Shabalala Ajiunga na Yanga SC Baada ya Miaka 11 Simba
- Ratiba ya CHAN 2025 Mechi za Makundi
- Orodha ya Wachezaji Wazawa Yanga Sc 2025/2026
- CV Ya Mohamed Doumbia Kiungo Mpya wa Yanga 2025/2026
- Cv ya Mohammed Bajaber Kiungo Mshambuliaji Mpya Simba Sc 2025/2026
Leave a Reply