Kikosi Cha Yanga VS Vitalo Leo 17/08/2024 CAF Champions League | Kikosi Cha Yanga Leo Dhidi ya Vital’o Klabu Bingwa Afrika.
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya NBC Tanzania na Ngao ya Jamii Yanga SC leo wanatarajia kuanza rasmi safari yao ya michuano ya kimataifa CAF, ambapo watachuana na klabu ya Vital’O kutoka Burundi.
Mchezo huu utaanza majira ya kumi jioni katika uwanja wa Azam Complex, Chamanzi. Michuano hii ni muhimu sana kwa Yanga SC, kwani inafungua ukurasa mpya wa kufukuzia mafanikio zaidi katika ngazi ya kimataifa.
Kuelekea mchezo huu, Yanga SC imejipanga kwa hali ya juu, huku kocha Miguel Gamondi akiwataka wachezaji wake kudumisha nidhamu ya kiufundi na umakini mkubwa katika kila dakika ya mchezo.
Kocha Gamondi, akiwa na kikosi kamili baada ya ushindi mnono wa 4-1 dhidi ya Azam FC kwenye Ngao ya Jamii, ameweka wazi kuwa lengo lake ni kupata ushindi wa kwanza nyumbani ili kuweka mazingira mazuri kwa mchezo wa marudiano.
Katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kabla ya mchezo, Kocha Mkuu wa Vital’O FC, Sahabo Parris, alikiri kuwa anakiheshimu kikosi cha Yanga SC kwa kuwa na wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu na morali ya ushindi. Hata hivyo, alisisitiza kuwa hakuna mechi rahisi katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika na kwamba wamejipanga kutoa upinzani mkali kwa Yanga.
Vital’O FC ni moja ya klabu zenye historia kubwa katika soka la Burundi. Timu hii imefanikiwa kutwaa mataji 21 ya Ligi Kuu Burundi na iliwahi kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika mwaka 1992. Msimu huu, Vital’O walitawazwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Burundi baada ya kumaliza msimu kwa alama 72 katika michezo 30, jambo linaloashiria kuwa ni timu yenye uwezo mkubwa wa ushindani.
Kikosi Cha Yanga VS Vitalo Leo 17/08/2024 CAF
Kikosi cha Yanga SC kwa sasa kipo katika hali nzuri, wachezaji kama Clatous Chama, Jean Baleke, na Farid Mussa wanatarajiwa kuleta changamoto kubwa kwa wapinzani. Aidha, wachezaji wapya kama Duke Abuya na Prince Dube wameonyesha kiwango cha juu tangu walipojiunga na timu hiyo, jambo linaloongeza matumaini ya Yanga kufanya vizuri katika michuano hii.
Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga, ametoa wito kwa mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Azam Complex ili kuwapa sapoti wachezaji na kuwatia morali. “Tumekuwa tukisema mara kwa mara kuwa hakuna mchezo mwepesi katika Ligi ya Mabingwa Afrika. Tunawaomba mashabiki wetu waje kwa wingi na kujenga mazingira ya ushindi,” alisema Kamwe.
Hiki apa ndicho kikosi rasmi cha Yanga leo
- 59 Diarra
- 21 Yad
- 30 Kibabage
- Mwamnyeto
- 4 Bagga
- Augho
- Maxi
- Mudathir
- 24 Dube
- 10 A212 Ki
- 12 Chama
Fuatilia Matokeo Ya Mhacho Huu APa
Mapendekezo ya Mhariri:
- Ifahamu Timu ya Vital’O Mpinzani wa Yanga CAF Champions league
- KMC na Simba Wafikia Makubaliano ya Uhamisho wa Kiungo Awesu Awesu
- Ahmed Arajiga Ateuliwa na CAF Kuchezesha Mechi ya Klabu Bingwa Afrika
- Dirisha la usajili Tanzania 2024/2025 Kufungwa Leo Agosti 15
- Viingilio Mechi ya Vital O FC Vs Yanga Klabu Bingwa 17/08/2024
- Jezi Mpya Za Yanga 2024/2025
- Yanga Yapata Mserereko CAF: Mechi Zote za Klabu Bingwa Kupigwa Dar es Salaam
Weka Komenti