Droo ya Robo Fainali Klabu Bingwa Afrika 2025/2026

Droo ya Robo Fainali Klabu Bingwa Afrika 2025/2026

Droo ya Robo Fainali ya Klabu Bingwa barani Afrika imekamilika rasmi leo majira ya saa 9:00 alasiri jijini Cairo, katika hafla iliyofanyika kwenye makao makuu ya Shirikisho la Soka la Misri, huku wawakilishi wa vilabu pamoja na maafisa wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) wakishuhudia upangaji wa mechi utakaoamua timu zitakazofuzu hatua ya nusu fainali ya msimu wa 2025/2026.

Hatua hiyo imewakutanisha mabingwa wanane waliovuka hatua ya makundi na sasa wanajiandaa kwa michezo ya mtoano ya kukata na shoka itakayochezwa mwezi Machi kabla ya kufuatiwa na nusu fainali mwezi Aprili.

Soma Pia: Droo ya Robo Fainali Kombe la Shirikisho Afrika 2025/2026

Droo ya Robo Fainali Klabu Bingwa Afrika 2025/2026

Timu Zilizofuzu Robo Fainali

Vilabu nane vilivyofanikiwa kufika hatua hii ya mashindano ni:

  1. Al Ahly (Misri)
  2. Pyramids (Misri)
  3. Al Hilal (Sudan)
  4. Stade Malien
  5. Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini)
  6. Royal Army (Morocco)
  7. Renaissance Berkane (Morocco)
  8. Esperance (Tunisia)

Al Ahly walifuzu baada ya kuongoza Kundi B kwa alama 10, huku mabingwa watetezi Pyramids wakiongoza Kundi A kwa alama 16, jambo linaloendeleza ushindani mkali wa vilabu vya Misri katika michuano hiyo msimu huu.

Matokeo ya Droo ya Robo Fainali Klabu Bingwa Afrika 2025/2026

Droo imepanga michezo minne mikubwa kama ifuatavyo:

  • Renaissance Berkane vs Al Hilal
  • Esperance vs Al Ahly
  • Mamelodi Sundowns vs Stade Malien
  • Pyramids vs Royal Army

Michezo ya mkondo wa kwanza itachezwa kati ya Machi 13–14, 2026, huku marudiano yakipangwa kufanyika Machi 20–21, 2026.

Ratiba ya Nusu Fainali

Washindi wa robo fainali watakutana mwezi Aprili kuwania nafasi ya kucheza fainali. Ratiba ni:

Nusu fainali ya kwanza
Mshindi wa Al Ahly vs Esperance atakutana na mshindi wa Mamelodi Sundowns vs Stade Malien.

Nusu fainali ya pili
Mshindi wa Renaissance Berkane vs Al Hilal atamenyana na mshindi wa Pyramids vs Royal Army.

Michezo ya kwanza ya nusu fainali itachezwa Aprili 10–11, 2026 na marudiano Aprili 17–18, 2026.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Droo Robo Fainali CAF 2025/26: Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Kupangwa Leo Cairo
  2. CAF Yalaani Vurugu Mechi ya Al Ahly vs AS FAR Ligi ya Mabingwa Afrika 2026
  3. Simba Sc vs Greenland Fc Leo 17/02/2026 Saa Ngapi?
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo