Wachezaji Wa Simba Walioitwa Timu ya Taifa October 2024 | Wachezaji wa Simba Walioitwa Taifa Stars
Katika maandalizi ya michezo miwili muhimu ya michuano ya kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2025), Kaimu Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Hemed Morocco, amechagua kikosi imara cha wachezaji 23 kitakacho ipambania bendera ya Tanzania.
Miongoni mwa wachezaji hao, Simba Sports Club imetoa jumla ya wachezaji wanne ambao wameitwa kuwakilisha timu ya taifa ya Tanzania mwezi Oktoba 2024. Wachezaji wa Simba walioteuliwa ni wale walioonyesha uwezo wa hali ya juu katika ligi ya ndani na ya kimataifa, na kuchaguliwa kwao kunadhihirisha umuhimu wa klabu yao kwenye soka la Tanzania.
Wachezaji Wa Simba Walioitwa Timu ya Taifa October 2024
Katika orodha ya wachezaji 23 waliochaguliwa, wachezaji wa Simba SC wamejumuishwa katika nafasi mbalimbali, kuanzia ulinzi hadi ushambuliaji. Wafuatao ni wachezaji wa Simba waliopo kwenye kikosi cha Taifa Stars kwa michezo ya kufuzu AFCON 2025 dhidi ya DR Congo:
- Ally Salim (Kipa)
- Mohammed Hussein (Beki)
- Abdulrazack Hamza (Beki)
- Kibu Denis (Mshambuliaji)
Maandalizi ya Taifa Stars Dhidi ya DR Congo
Tanzania inakutana na DR Congo, timu inayoongoza kundi H katika mbio za kutafuta tiketi za kufuzu AFCON 2025. Mchezo wa kwanza utafanyika Oktoba 10, 2024, ugenini, huku mchezo wa pili ukiwa nyumbani Oktoba 15. Katika michezo hii, wachezaji wa Simba wana nafasi muhimu ya kuhakikisha Tanzania inapata matokeo mazuri.
Simba SC imekuwa na historia ya kutoa wachezaji wenye viwango vya kimataifa, na waliochaguliwa kwa timu ya taifa Oktoba 2024 wamepewa jukumu la kuonyesha uwezo wao kwa nchi nzima. Ushiriki wao katika timu ya taifa utasaidia kuimarisha nafasi ya Tanzania kufuzu kwenye mashindano hayo makubwa barani Afrika.
Mapendekezo ya Mhariri:
Weka Komenti