eRITA Portal: Uhakiki wa Cheti cha Kuzaliwa 2024 (Njia Rahisi) | Jinsi ya Kuhakiki Cheti cha Kuzaliwa RITA Online 2024
Katika karne hii yenye ukuaji mkubwa na matumizi makubwa wa vifaa vya kidijitali, urahisi na ufanisi katika upatikanaji wa huduma muhimu za kijamii ni jambo lililoleta haueni kubwa kwa watoa huduma mbalimbali.
Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) umechukua hatua kubwa katika kurahisisha uhakiki wa vyeti vya kuzaliwa kwa kuanzisha huduma mpya kupitia mtandao inayojulikana kama eRITA Portal.
Huduma hii mpya ya kielektroniki inalenga kuondoa usumbufu, kuongeza ufanisi na kuokoa muda kwa watanzania wanaohitaji kuhakiki vyeti vyao vya kuzaliwa kwa ajili ya kutimiza mambo mbalimbali. Badala ya safari ndefu na foleni katika ofisi za RITA, sasa inawezekana kuhakiki cheti cha kuzaliwa kwa urahisi na haraka muda wowote na ukiwa mahali popote pale.
Kupitia huduma ya eRITA Portal, muombaji anaweza kuwasilisha ombi la uhakiki wa cheti cha kuzaliwa kwa kuskani cheti halisi na kukituma kwa njia ya kielektroniki. Hii inaondoa hitaji la kuwasilisha nakala halisi na hivyo basi kuokoa gharama na muda wa usafiri.
Baada ya uhakiki kukamilika, majibu yatatumwa moja kwa moja kwenye akaunti ya muombaji katika sehemu ya “Maelezo” (Details) ambapo pia ataweza kupakua cheti kilichohakikiwa. Huduma hii inaifanya RITA kuwa kinara katika kuweka mifumo ya kisasa inayomrahisishia mtanzania kupata huduma muhimu kwa wakati na kwa ufanisi mkubwa.
eRITA Portal: Uhakiki wa Cheti cha Kuzaliwa 2024 (Njia Rahisi)
Jinsi ya Kuhakiki Cheti cha Kuzaliwa RITA Online 2024
- Tembelea Tovuti ya RITA: Anza kwa kutembelea tovuti rasmi ya RITA kupitia anwani www.rita.go.tz.
- Fikia Lango la eRITA: Kwenye tovuti, bofya kitufe cha “eRITA” ili kuingia kwenye lango la huduma za kielektroniki.
- Chagua Huduma ya Kuhakiki Vizazi na Vifo: Katika lango la eRITA, chagua kategoria ya “Huduma Za Vizazi Na Vifo” ili kuendelea.
- Fungua Akaunti (Usajili): Kama wewe ni mtumiaji mpya, bofya “REGISTER” na ujaze taarifa zinazohitajika kwa usahihi ili kufungua akaunti. Hakikisha nenosiri lako lina herufi zaidi ya nane, ikijumuisha herufi kubwa, ndogo, namba, na alama. Baada ya kujisajili, fuata maelekezo katika barua pepe yako ili kuamilisha akaunti.
- Ingia Kwenye Akaunti Yako: Baada ya kuamilisha akaunti, bofya “SIGN IN” na uweke taarifa zako sahihi (jina la mtumiaji na nenosiri) ili kuingia kwenye mfumo.
- Chagua Huduma ya Kuzaliwa: Katika menyu ya huduma, chagua “BIRTH SERVICES” ili kuendelea na uhakiki wa cheti cha kuzaliwa.
- Omba Uhakiki: Chagua “REQUEST VERIFICATION” na ujaze taarifa zote zinazohitajika kwa usahihi, ikiwa ni pamoja na jina, tarehe ya kuzaliwa, na namba ya cheti cha kuzaliwa.
- Chagua Sababu ya Uhakiki: Bainisha taasisi inayohitaji uhakiki (kwa mfano, benki, chuo, mwajiri) katika sehemu ya “VERIFICATION REASON”.
- Ambatanisha Cheti cha Kuzaliwa: Changanua (scan) cheti chako cha kuzaliwa na ukiambatanishe katika fomu ya maombi. Hakikisha cheti kiko katika mfumo wa PDF na taarifa zote zinasomeka vizuri.
- Omba Namba ya Malipo: Bofya “REQUEST CONTROL NUMBER” ili kupata namba ya malipo.
- Fanya Malipo: Lipa ada ya uhakiki kwa kutumia namba ya malipo uliyopatiwa.
- Subiri Majibu: Majibu ya uhakiki yatatumwa kupitia akaunti yako ya eRITA.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Jinsi ya Kupata Cheti cha Kuzaliwa Tanzania
- Jinsi Ya kukata Tiketi Ya Treni Online (eticketing.trc.co.tz) 2024
- Jinsi Ya Kupata Namba Ya NIDA Kwa Simu 2024
- Jinsi ya Kuangalia Namba ya NIDA Online 2024
- Jinsi Ya Kukopa Salio Nipige Tafu Vodacom (Menu Ya Kukopa Salio Vodacom) 2024
- Jinsi ya Kukopa Salio Airtel (Menu Ya Kukopa Salio Airtel)
- Jinsi Ya Kupata Leseni Ya Biashara Ya Duka La Rejareja
- Jinsi Ya Kuangalia Taarifa Zangu Za NIDA 2024
Weka Komenti