Jezi Mpya Za Azam Fc 2024/2025: HATIMAYE Azam FC imefungua milango ya utambulishi wa Jezi mpya za msimu wa 2024/2025 kwa kuanza kwa kuonyesha jezi zake za mazoezi ambazo zimeanza kutumika Morocco ilipo kambi ya mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya. Jezi hizo ambao zimesifiwa na mashabiki wengi kwa kua na muonekano mzuri zimetangazwa rasmi leo tarehe 17 julai 2024.
Uzinduzi huu wa jezi umefanyika huku kukiwa na shauku kubwa kutoka kwa mashabiki wa Azam FC, ambao wamekuwa wakisubiri kwa hamu kuona nini kipya kimeandaliwa kwa msimu ujao. Jezi za mazoezi, zikiwa zimevaliwa na wachezaji nyota wa timu hiyo wakati wa mazoezi yao nchini Morocco, zimeonesha muundo wa kisasa na rangi zinazovutia.
Wakati jezi mpya za mazoezi zikiwa zimewekwa wazi, mashabiki wa Azam FC sasa wanasubiri kwa hamu kubwa uzinduzi wa jezi za nyumbani na ugenini. Je, zitakuwa na rangi gani? Je, zitakuwa na muundo wa aina gani? Maswali haya yameibua mijadala mingi miongoni mwa mashabiki, huku kila mmoja akijaribu kubashiri nini kipya kitakuja.
Muonekano & Picha Jezi Mpya Za Azam Fc 2024/2025
Jezi Mpya Za Azam Za Mazoezi
Jezi Mpya Za Azam Fc 2024/2025 (Jezi ya NYumbani & Ugenini)
Baada ya kuonesha mashabiki wake jezi mpya za mazoezi ambazo zilionekana kutumika katika kambi ya mazoezi huko Morocco, Klabu ya Azam inatarajia kuzindua jezi zake mpya ambazo watazitumia kwa michezo ya mashindano yote msimu wa 2024/2025. Jezi mpya za Azam zimepangwa kuzinduliwa kesho Agosti 01 2024 kwa staili ya aina yake.
Klabu ya Azam FC itafanya uzinduzi wa jezi mpya katika boti ya Kilimanjaro VIII ‘The Falcon Sea’ jijini Dar es Salaam saa 3:00 asubuhi. Baadaye, saa 9:00 alasiri, uzinduzi utaendelea katika jengo la Michenzani Mall, Unguja. Uzinduzi huu wa kipekee unatarajiwa kuvutia mashabiki na wanachama wa klabu hiyo.
Azam FC inatarajia kuanza msimu mpya kwa kushiriki katika mchezo wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Coastal Union ya Tanga mnamo Agosti 8, Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar. Aidha, klabu hiyo itashiriki pia Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao, na pia imepanga kucheza mchezo wa kirafiki na Rayon Sports ya Rwanda.
Hizi Apa Jezi Mpya za Azam Fc 2024/20225
Mapendekezo ya Mhariri:
Weka Komenti