Jezi Mpya za Simba 2024/25 | Muonekano w Jezi mpya za Simba 2024
Wakati usajili wa wachezaji watakaoongeza nguvu katika kikosi cha Simba Msimu wa 2024/2024 kuendelea kufanyika, Klabu ya Simba inakalibia kutangaza jezi mpya ambazo watavaa msimu wa 2024/2025. Uzinduzi huu wa jezi za wekundu wa msimbazi Simba Sc unasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa Simba pamoja na wafanyabiashara nchini Tanzania.
Mashabiki wa Simba Sc wamekuwa wakisubiri kwa hamu kubwa kuona jinsi jezi hizi zitakavyoonekana, zikiwa ni ishara ya matumaini mapya na ari ya ushindi kwa timu yao pendwa katika msimu mpya wa 2024-2025. Wafanyabiashara nao wanasubili uzinduzi wa jezi za Simba kwa hamu kubwa sababu kwao ni fursa kubwa ya kibiashara, wakitarajia kuuza kwa wingi na kuongeza mapato yao.
Jezi Mpya za Simba 2024/25
Habari za Hivi Punde: Klabu ya Simba Sc imetangaza rasmi jezi zao mpya kwa ajili ya msimu wa 2024/2025. Jezi hizo ambayo zimepewa jina la jezi za Ubaya Ubwela zitaanza kupatikana rasmi katika maduka mbalimbali mara tu baada ya kutangazwa.
Uzinduzi wa Jezo mpya za simba 2024/2025 umefanyika katika mbuga ya wanyama ya Mikumi mkoani Morogoro ambapo mashabiki na viongozi pamoja na kikosi kazi cha uzinduzi wa jezi mpya wamekutana kwa ajili ya zoez la utangazaji wa jezi.
Picha, Muonekano wa Jezi Mpya Za Simba
Kibegi chenye jezi ya Ubaya Ubwela kimewasili kesho kuzinduliwa ndani ya mbuga ya Mikumi.
Endelea kufatilia safari ya kibegi cha jezi ya Ubaya Ubwela usikae mbali na kurasa zetu.
Jezi za Ubaya Ubwela zitaanza kuuzwa rasmi baada ya kuzinduliwa kesho.
Taarifa zaidi tumia Simba… pic.twitter.com/OJj3dwBjX1
— Simba Sports Club (@SimbaSCTanzania) July 23, 2024
Tetesi zinasema kuwa jezi za nyumbani zitakuwa na rangi nyekundu na nyeupe, zikiwa na michoro ya kisasa inayowakilisha historia na utamaduni wa klabu. Jezi za ugenini, kwa upande mwingine, zinatajwa kuwa na rangi nyeupe na michoro ya kipekee.
Gharama na Upatikanaji wa Jezi
Jezi mpya za Simba zitauzwa kwa gharama ya shilingi 32,000 kwa kila moja. Mashabiki na wafanyabiashara wanaweza kununua jezi hizi kuanzia matawi yote ya Simba SC na kwa wauzaji wa jumla wa Simba nchini kote. Upatikanaji wa jezi hizi umewekwa vizuri ili kuhakikisha kila shabiki anaweza kupata jezi kwa urahisi.
Namna ya Kupata Jezi Mpya
Kwa wale ambao wangependa kununua jezi mpya za Simba, wanaweza kutumia namba za simu zilizoainishwa kwa ajili ya mawasiliano na kufanya oda. Namba za mawasiliano ni +255675500000 na +255718431948. Jezi hizi pia zitapatikana kwenye maduka ya michezo na maeneo mengine yaliyosajiliwa kuuza bidhaa za Simba SC.
Mapendekezo ya mhariri:
Weka Komenti