Jinsi ya Kulipia King’amuzi Cha Azam 2024 Kwa Airtel Money, M-pesa, Halopesa And Tigo pesa kwa Urahisi
Je, wewe ni mpenzi wa burudani za Azam TV? Unatamani kufurahia mechi za Ligi Kuu Tanzania, tamthilia kali, habari mpya motomoto, na makala mbalimbali za kielimu? Huna haja ya kusumbuka tena! Mwongozo huu utakuelekeza jinsi ya kulipia king’amuzi cha Azam kwa haraka na urahisi mwaka huu wa 2024.
Azam TV imejiimarisha kama chaguo bora kwa Watanzania wengi. Vifurushi vyake vinatoa mchanganyiko wa kipekee wa burudani, habari, michezo, na elimu ili kukidhi mapenzi ya familia mbalimbali. Lakini kabla ya kufurahia uhondo muvi kali au mecha kali za ligi kuu Tanzania kupitia Azam Tv, unahitaji kulipia kifurushi chako. Hapa Tutakuonyesha njia mbalimbali rahisi za kufanya hivyo.
Vifurushi vya Azam TV 2024: Chagua Kinachokufaa
Azam TV inatoa vifurushi tofauti ili kukidhi mahitaji ya wateja tofauti tofauti:
- Azam Lite: Kwa shilingi 8,000 tu, pata burudani ya kutosha
- Azam Pure: Furahia chaneli zaidi kwa shilingi 13,000
- Azam Plus: Pata uhondo kamili kwa shilingi 20,000
- Azam Play: Fikia kiwango cha juu cha burudani kwa shilingi 35,000
- DTT packages: Saadani, Mikumi, Ngorongoro, na Serengeti zinapatikana kwa bei sawa na vifurushi vya kawaida
Jinsi ya Kulipia King’amuzi cha Azam kwa Urahisi Mwaka 2024
Moja kati ya vitu rahisi kufanya katika zama hizi za teknolojia ni pamoja na kufanya malipo mbalimbali kupitia simu za mkononi. Shukrani ziende kwa maendeleo ya kiteknolojia, sasa sio lazima kutoka nyumbani na kwenda kutafuta mawakala ili kulipia Azam TV. Mtu yeyote na wakati wowote anaweza kutumia simu ya mkononi kulipia kifurushi cha Azam kwa urahisi zaidi akiwa ameketi kwenye kochi sebuleni. Kama ni mgeni katika zoezi hili, basi fuata muongozo huu rahisi:
1. Jinsi ya Kulipia King’amuzi cha Azam kwa M-Pesa
- Piga *150*00#
- Chagua “Lipa kwa M-Pesa”
- Chagua Namba 4 – Malipo Ya Kampuni
- Chagua Namba 3 – Chagua Kwenye Orodha
- Chagua Namba 1 – King’amuzi
- Chagua Namba 5 – Azam Tv – Ok
- Ingiza Namba Ya Kumbukumbu: Tz1000xxxx – Ok
- Weka Kiasi
- Weka Namba Ya Siri
- Bonyeza 1 Kuthibitisha
2. Jinsi ya Kulipia King’amuzi cha Azam kwa Airtel Money:
- Piga *150*60#
- Chagua Lipa Bili
- Chagua chagua biashara
- Chagua Vin’gamuzi vya TV
- Chagua Azam Pay TV
- Weka kiasi
- Weka Nambari ya Marejeleo (Nambari ya Akaunti ya Azam TV)
- Weka Pini
- Bonyeza 1 ili kuthibitisha‚ 2 ili kukataa.
3. Jinsi ya Kulipia King’amuzi cha Azam kwa Tigo Pesa:
- Piga *150*01#
- Chagua “Lipa Bili”
- Chagua “Pata Namba ya Biashara”
- Chagua “5 Kin’gamuzi”
- Chagua “Azam Pay Tv”
- Fuata hatua kama za M-Pesa
Mapendekezo Ya Mhariri:
- Jinsi Ya Kuangalia Salio La Vifurushi Airtel 2024
- Jinsi Ya Kuangalia Usajili Wa Namba ya Simu
- Code Za Mitandao Ya Simu Tanzania | Namba Za Simu Tanzania 2024
- Jinsi Ya Kuangalia Namba Ya Simu Airtel, Vodacom, TTCL, Tigo & Halotel
- Menu ya Kukopa Salio Halotel & Jinsi ya Kukopa Muda wa Maongezi
- Hizi Apa Code za Haloteli: Namba Muhimu Za Haloteli 2024
- Jinsi ya Kukopa Salio Airtel (Menu Ya Kukopa Salio Airtel)
- Jinsi ya Kukopa Salio Tigo (Menu Ya Kukopa Salio Tigo) 2024
Weka Komenti