JKU Yanyakua Ubingwa Ligi Kuu Zanzibar 2023/2024: Ligi Kuu Zanzibar (ZPL) msimu wa 2023/2024 bila shaka utaandikwa kwenye historia kama miongoni mwa misimu bora ya soka Zanzibar. Msimu wa 2023/2024 ulikua na ushindani wakipekee, huku JKU wakitawazwa mabingwa wapya baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Kipanga siku ya Ijumaa ya tareh 21. Ushindi huu wa kihistoria umekuja baada ya mchuano mkali na Zimamoto, ambao walimaliza katika nafasi ya pili baada ya kipigo cha 2-0 dhidi ya New City.
JKU Yanyakua Ubingwa Ligi Kuu Zanzibar 2023/2024
Safari ya JKU Kuelekea Ubingwa Ligi Kuu Zanzibar 2023/2024
JKU walianza msimu kwa kusuasua, lakini walionyesha uthabiti na azma ya ushindi katika mechi za mwisho. Sare yao dhidi ya Kipanga iliwafikisha pointi 66, wakizidi Zimamoto kwa pointi nne.
Mafanikio haya ni ushuhuda wa juhudi za pamoja za wachezaji, makocha, na mashabiki wa JKU. Zimamoto walikuwa na matumaini makubwa ya kutwaa ubingwa, lakini kipigo chao dhidi ya New City kiliwaacha wakiwa na pointi 62.
Licha ya juhudi zao za kupambana hadi mwisho, hawakuweza kuzuia JKU kunyakua taji hilo.
Msimu huu pia umeshuhudia mabadiliko makubwa katika msimamo wa ligi. Kundemba, licha ya ushindi wao wa 2-1 dhidi ya Malindi, walishushwa daraja pamoja na Ngome, Jamhuri, na Maendeleo. Matokeo haya yanaonyesha ushindani mkali katika ZPL na umuhimu wa kudumisha kiwango cha juu katika kila mechi.
Mapendekezo Ya Mhariri:
- Yanga Yafanikiwa Kutetea Ubingwa wa Kombe la Shirikisho la CRDB 2024
- Timu za Tanzania Zilizofuzu Klabu Bingwa Afrika 2024/2025
- Timu Zilizofuzu Klabu Bingwa Afrika 2024/2025
- Picha Za Parade ya Yanga SC Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2023/24
- Yanga SC Kusherehekea Ubingwa wa Ligi kwa Parade Kubwa Mei 25
- Yanga SC Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania 2023/24: Ushindi wa Mara ya 30 Kihistoria
- Orodha Ya Mabingwa Wa UEFA Champions League
Weka Komenti