Kikosi cha Azam Vs JKT Tanzania Leo 28/08/2024 | Kikosi cha Azam Leo Dhidi ya JKT Tanzania Agosti 28 2024 Ligi kuu
Klabu ya JKT Tanzania leo watawakalibisha wana rambaramba Azam FC katika mchezo wao wa kwanza ligi kuu ya NBC Tanzania msimu wa 2024/2025 utakaochezeka majira ya saa 10 jioni katika dimba la Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni. Mchezo huu unatarajiwa kuwa wa kusisimua sana, huku timu zote zikiwa na malengo makubwa katika msimu huu wa 2024/2025.
Baada ya kupoteza nafasi ya kushiriki katika michuano ya kimataifa dhidi ya APR ya Rwanda, Azam FC wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa na ari ya kurekebisha makosa yao waliyoyafanya katika michezo ya klabu bingwa na kuanza ligi kwa ushindi.
Kocha wa Azam, Youssouph Dabo, ameweka wazi kuwa licha ya changamoto zilizowakuta katika michuano ya awali, malengo ya timu bado yako palepale – kuhakikisha wanapambana hadi mwisho wa msimu kwa mafanikio.
Kwa upande mwingine, JKT Tanzania wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa na matumaini makubwa. Timu hii ilinusurika kushuka daraja msimu uliopita baada ya kushinda katika mechi za mchujo (play-off), na sasa wakiwa na kikosi kipya, wanataka kuanza ligi kwa ushindi. Kocha wa JKT, Hamady Ally, anafahamu vizuri ubora wa Azam FC na amesisitiza kuwa wamejiandaa kikamilifu kwa ajili ya mchezo huu.
Kikosi cha Azam Vs JKT Tanzania Leo 28/08/2024
Kikosi cha Azam dhidi ya JKT Tanzania leo katika mchezo wa ligi kuu kinatarajiwa kutangazwa majira ya saa 9 alasiri. Hapa tutakuletea orodha ya wachezaji wote wa Azam watakao anza katika mtanange huu mara tuu baada ya kutangazwa rasmi na kocha.
Fuatilia Hapa Matokeo JKT Tanzania Vs Azam Leo 28/08/2024
Kocha Youssouph Dabo wa Azam FC ana matumaini kuwa kikosi chake kitarudia ubora wa msimu uliopita. Amekuwa akiwasisitiza wachezaji wake kutonunja moyo licha ya matokeo mabaya katika Ligi ya Mabingwa Afrika. Kwa mujibu wa Dabo, mchezo wa leo utakuwa kipimo cha maandalizi yao ya msimu mpya, na anaamini kuwa kikosi chake kinaweza kufanya vizuri ikiwa watacheza kwa umakini na nidhamu kubwa.
Kwa upande wa JKT, kocha Hamady Ally anaamini kwamba maandalizi waliyoyafanya yatazaa matunda. Amewahimiza wachezaji wake kucheza kwa kujituma na kuwa makini katika kujilinda dhidi ya mashambulizi ya Azam, ambao wana washambuliaji wenye uwezo mkubwa.
Historia ya Mikutano ya JKT Tanzania vs Azam Fc Hivi Karibuni
Azam FC imekuwa na rekodi nzuri dhidi ya JKT Tanzania katika misimu iliyopita. Katika msimu uliopita wa 2023/2024, Azam ilishinda mechi zote mbili walizokutana. Mechi ya kwanza ilichezwa Desemba 11, 2023, ambapo Azam ilishinda kwa mabao 2-1, huku mechi ya marudiano ikipigwa Mei 21, 2024, ambapo Azam walishinda tena kwa mabao 2-0. Hata hivyo, hali ya mchezo wa leo ni tofauti, kwa sababu timu zote zimefanya usajili mkubwa ambao unatarajiwa kuleta ushindani zaidi.
Katika mikutano ya nyuma, Azam haijawahi kupoteza dhidi ya JKT Tanzania tangu mwaka 2018, wakishinda mechi sita na kutoka sare mara mbili. Ushindi wao mkubwa dhidi ya JKT Tanzania ulitokea Machi 8, 2019, walipoibuka na ushindi wa mabao 6-1.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Matokeo ya Mashujaa Vs Dodoma Jiji Leo 17/08/2024
- Matokeo ya Pamba Jiji Vs Tanzania Prisons Leo 16/08/2024
- Viingilio Mechi ya Pamba Jiji Vs Tanzania Prisons 16/08/2024
- Vikosi Mechi ya Pamba Jiji Vs Tanzania Prisons 16/08/2024
- Viingilio Mechi ya Pamba Jiji Vs Tanzania Prisons 16/08/2024
- Vikosi Mechi ya Pamba Jiji Vs Tanzania Prisons 16/08/2024
Weka Komenti