Kikosi cha Simba SC VS Nsingizini Leo 26/10/2025

Kikosi cha Simba SC VS Nsingizini Leo 26/10/2025

Leo jioni, timu ya Simba SC itashuka dimbani katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam, kuivaa Nsingizini Hotspurs kutoka Eswatini katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League). Mchezo huo wa kiporo unatarajiwa kuanza saa 10:00 jioni na kuruka moja kwa moja kupitia Azam Sports 1 HD.

Mnyama anaingia katika mtanange huu akiwa na mtaji wa mabao 3–0, ushindi uliopatikana katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliochezwa Oktoba 19, 2025 huko Eswatini. Hata hivyo, benchi la ufundi limeweka wazi kuwa pamoja na matokeo hayo mazuri, Simba SC haitabweteka, bali itashambulia zaidi ili kuhakikisha inatinga hatua ya makundi kwa kishindo.

Kikosi cha Simba SC VS Nsingizini Leo 26/10/2025

MUHTASARI: KIKOSI CHA SIMBA SC VS NSINGIZINI LEO 26/10/2025

  • Tarehe: Jumapili, 26 Oktoba 2025
  • Uwanja: Benjamin Mkapa, Dar es Salaam
  • Muda: Saa 10:00 jioni (AzamSports1HD)
  • Matokeo ya kwanza: Nsingizini 0–3 Simba SC

MATOLA: “TUNAHITAJI KUJITUMA ZAIDI – HUU NI MCHEZO MWINGINE”

Kocha msaidizi wa Simba SC, Selemani Matola, amesema timu yake imejipanga vizuri kwa mchezo wa leo licha ya kuwa na faida ya mabao matatu. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Matola alisisitiza kuwa wanatambua umuhimu wa mchezo huu na hawataki kurudia makosa ya misimu iliyopita.

“Ni kweli tuna uzoefu mkubwa katika hii michuano, lakini hatutaki kurudia kile kilichowahi kutukuta misimu kadhaa nyuma. Hii ni mechi nyingine yenye uhitaji mkubwa kama ilivyokuwa ile ya mwanzoni ugenini,” alisema Matola.

Matola pia alizungumzia motisha mpya kwa kikosi hicho, kufuatia Simba kuteuliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuwania tuzo ya Klabu Bora ya Afrika kwa mwaka 2025.

“Sio kwa bahati mbaya tumepata nafasi hiyo. Ni kutokana na mafanikio ya kimataifa tuliyoyapata. Hii inatupa morali ya kupambana zaidi katika michuano mikubwa kama hii,” aliongeza.

Hali ya Wachezaji wa Simba SC Kabla ya Mechi

Katika upande wa wachezaji, taarifa njema kutoka benchi la ufundi ni kwamba beki Wilson Nangu ambaye alipata majeraha kwenye mchezo wa kwanza yupo fiti na anatarajiwa kuanza. Aidha, kiungo mshambuliaji Mohamed Bajaber naye anaendelea vizuri baada ya kufanyiwa programu maalumu ya mazoezi ili kuhakikisha yupo tayari kikamilifu.

Kapombe: “Tunataka kuandika historia mpya”

Nahodha wa Simba SC, Shomari Kapombe, amesema kikosi chao hakina mpango wa kuridhika na matokeo ya awali, bali kimejipanga kuonyesha ubora zaidi mbele ya mashabiki wake.

“Niwaombe mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi kwa sababu mechi ya kwanza hawakupata nafasi hiyo. Hii ni fursa nyingine nzuri ya kuendelea kuandika historia mpya kwa umoja wetu,” alisema Kapombe.

Aidha, Kapombe aliongeza kuwa jukumu lake kama nahodha ni kuhakikisha Simba inaendelea kusonga mbele kimataifa.

“Nina majukumu mazito kama nahodha ya kuipeleka Simba mbali zaidi ya hapa. Naamini kwa umoja na ushirikiano wetu tutafikia malengo tuliyodhamiria kwa msimu huu,” aliongeza kwa kujiamini.

Nsingizini Hotspurs: “Tunajua ugumu upo, lakini tutapambana”

Kwa upande wa wapinzani wao kutoka Eswatini, Kocha Mkuu wa Nsingizini Hotspurs, Mandla Qhogi, amesema licha ya kupoteza mchezo wa kwanza kwa mabao 3-0, kikosi chake kimejipanga kupambana kwa ajili ya taifa lao na mashabiki wa Eswatini.

“Kabla ya mechi yetu ya kwanza hakuna aliyetarajia kama Simba ingeshinda kwa idadi kubwa ya mabao. Hii ni mechi nyingine ngumu, ila tutapambana kadri ya uwezo wetu,” alisema Mandla.

Ameongeza kuwa wanatambua ugumu wa kucheza katika Uwanja wa Benjamin Mkapa wenye uwezo wa kubeba zaidi ya mashabiki 60,000, lakini bado wana matumaini ya kutoa upinzani.

“Tunatambua Simba ni miongoni mwa timu tano bora barani Afrika, hivyo tunajua tunakutana na changamoto kubwa. Hata hivyo, tutapambana hadi dakika ya mwisho,” alisisitiza kocha huyo.

Kikosi cha Simba SC VS Nsingizini Leo 26/10/2025

Kikosi cha Simba kinatarajiwa kuongozwa na nyota wake wa kimataifa wakiwa na lengo la kuendeleza ubabe wao na kumaliza mchezo wakiwa na matokeo chanya mbele ya mashabiki wao, jijini Dar es Salaam.

Kama Simba Sc wataweza kuibuka mabingwa wa mchezo basi watafuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika 2025/2026. Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo, wachezaji wapo katika hali nzuri ya kiafya na morali iko juu.

Hapa chini Tutakuletea kikosi cha Simba Sc kitakachoanza dhidi ya Nsingizini Hotspurs mara tu baada ya Kutangazwa.

Kikosi cha Simba SC VS Nsingizini Leo 26/10/2025

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Singida BS VS Flambeau Leo 25/10/2025 Saa Ngapi?
  2. Yanga Vs Silver Strikers Leo 25/10/2025 Saa Ngapi?
  3. Matokeo ya Azam vs KMKM Leo 24/10/2025
  4. Yanga SC Yatangaza Kuachana na Kocha Wake Romain Folz
  5. Timu Zilizofuzu Kombe la Dunia 2026
  6. Msimamo wa Ligi Kuu Zanzibar PBZ 2025/2026
  7. Matokeo ya Azam vs KMKM Leo 24/10/2025
  8. Pacome Anukia Kombe la Dunia Baada ya Ushindi 7-0 Dhidi ya Shelisheli
  9. Kaizer Chiefs Ya Thibitisha Kuachana na Kocha Nasreddine Nabi
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo