Kikosi cha Simba vs Azam Leo 08/01/2026 Mapinduzi Cup

Kikosi cha Simba vs Azam Leo 08/01/2026 Mapinduzi Cup

Wana rambaramba wa Azam FC leo wanakutana na Simba SC katika moja ya mechi zinazosubiriwa kwa hamu kubwa, nusu fainali ya NMB Mapinduzi Cup 2026, pambano linalobeba heshima, historia na kisasi cha wazi kati ya wapinzani hawa wakubwa wa soka la Tanzania. Mchezo huu utapigwa leo Januari 08, 2026, kuanzia saa 2:15 usiku, katika Uwanja wa New Amaan Complex, Unguja, huku macho na masikio ya mashabiki yakielekezwa kwenye kikosi cha Simba vs Azam leo 08/01/2026 Mapinduzi Cup.

Taarifa Muhimu za Mchezo

  • Mashindano: NMB Mapinduzi Cup 2026
  • Hatua: Nusu Fainali
  • Tarehe: 08 Januari 2026
  • Muda: Saa 2:15 usiku
  • Uwanja: New Amaan Complex, Unguja

Viingilio:

  • Orbit & Saa – 3,000/=
  • Urusi – 5,000/=
  • VIP – 10,000/=

Kikosi cha Simba vs Azam Leo 08/01/2026 Mapinduzi Cup

Historia Fupi ya Dabi ya Mzizima

Ni takribani mwezi mmoja tu umepita tangu Simba SC na Azam FC zilipokutana kwenye Dabi ya Mzizima ya Ligi Kuu Bara, ambapo Azam iliibuka na ushindi wa mabao 2-0. Leo, dabi hiyo inarudi tena lakini safari hii ikiwa ni kwenye jukwaa la nusu fainali ya Mapinduzi Cup, mashindano ambayo yamekuwa na kumbukumbu nyingi kwa timu hizi mbili.

Kwa ujumla, Simba na Azam zimekutana mara saba kwenye Kombe la Mapinduzi tangu Azam FC ilipoanza kushiriki mwaka 2011. Takwimu zinaonyesha Azam kushinda mechi tano huku Simba ikishinda mbili, hali inayoongeza uzito na presha kwenye kikosi cha Simba vs Azam leo 08/01/2026 Mapinduzi Cup.

Safari ya Azam FC Hadi Nusu Fainali

Azam FC imefuzu hatua hii baada ya kumaliza kama kinara wa Kundi A kwa pointi saba. Walipata ushindi dhidi ya:

  • Mlandege (2-0)
  • URA (2-1)
  • na sare ya bao 1-1 dhidi ya Singida Black Stars.

Matokeo haya yameonesha uimara wa kikosi chao na uthabiti katika mashindano haya.

Safari ya Simba SC Kwenye Mapinduzi Cup 2026

Kwa upande wa Simba SC, walimaliza juu ya Kundi B baada ya kushinda mechi zote mbili walizocheza:

  • Muembe Makumbi City (1-0)
  • Fufuni (2-1)

Ushindi huo uliihakikishia Simba tiketi ya nusu fainali na kuifanya iwe tayari kwa mtihani mkubwa dhidi ya Azam.

Kikosi cha Simba vs Azam Leo 08/01/2026 Mapinduzi Cup

Hapa tutakuletea kikosi kamili cha Simba SC kitakachoshuka dimbani kuikabili Azam FC katika mchezo wa nusu fainali ya NMB Mapinduzi Cup 2026. Orodha hii itajumuisha wachezaji wa kuanza pamoja na waliopo benchi la akiba, kulingana na tangazo rasmi la benchi la ufundi la Simba SC.

Kwa mujibu wa ratiba ya mchezo, kikosi cha Simba kinatarajiwa kutangazwa majira ya saa moja usiku, muda mfupi kabla ya mpira wa kuanza. Mara tu taarifa hizo zitakapotolewa rasmi, sehemu hii itasasishwa papo hapo ili kuwapatia wasomaji taarifa sahihi, za kuaminika na zilizothibitishwa kuhusu kikosi cha Simba vs Azam leo 08/01/2026 Mapinduzi Cup.

Endelea kufuatilia ukurasa huu kwa taarifa kamili za kikosi, mabadiliko ya dakika za mwisho na maelezo muhimu kuelekea mchezo huu mkubwa wa Mapinduzi Cup 2026.

Hiki Apa Kikosi cha Simba

Kikosi cha Simba vs Azam Leo 08/01/2026 Mapinduzi Cup

Rekodi za Simba vs Azam Kwenye Mapinduzi Cup

Katika historia ya Mapinduzi Cup, timu hizi zimekutana mara kadhaa katika hatua tofauti, ikiwemo nusu fainali na fainali. Baadhi ya matokeo muhimu ni pamoja na:

  • Azam 2-0 Simba (Nusu fainali 2012)
  • Azam 2-2 Simba, Azam ikashinda penalti 5-4 (Nusu fainali 2013)
  • Azam 1-0 Simba (Fainali 2017)
  • Azam 2-1 Simba (Fainali 2019)
  • Simba kushinda kwa penalti 3-2 baada ya sare ya 0-0 (Nusu fainali 2020)
  • Simba 1-0 Azam (Fainali 2022)

Mara ya mwisho walipokutana ilikuwa Desemba 7, 2025 katika Ligi Kuu Bara, ambapo Azam iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Mapednekezo ya Mhariri:

  1. Timu Zilizofuzu Robo Fainali AFCON 2025
  2. Msimamo wa Kundi C La Tanzania AFCON 2025
  3. Haaland Aipiku Rekodi ya Magoli ya Cristiano Ronaldo EPL
  4. Bingwa wa AFCON 2025 Kubeba Zaidi ya Bilioni 24 za Kitanzania
  5. Chelsea Yanusurika Kupigika Nyumbani Kwa Newcastle United
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo