Kikosi Cha Yanga Vs Azam Fc Fainali Ngao ya Jamii 11/08/2024 | Kikosi cha Yanga Dhidi ya Azam Fc Fainali
Mtanange wa kukata na shoka unatarajiwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Agosti 11, 2024, wakati Yanga na Azam FC zitakapokabiliana katika fainali ya Ngao ya Jamii msimu wa 2024. Mechi hii inakuja baada ya Azam FC kujikatia tiketi kwa ushindi mnono wa 5-2 dhidi ya Coastal Union, huku Yanga wakionyesha ubabe wao kwa kuwatoa mahasimu wao Simba kwa 1-0.
Fainali hii itakuwa ni mkutano wa 38 kati ya timu hizi mbili katika mashindano yote, ikiwa ni pamoja na Ligi Kuu Tanzania Bara, Kombe la Shirikisho la CRDB, na Kombe la Kagame la Cecafa. Yanga wanaongoza kwa ushindi katika mechi 17, huku Azam FC wakiwa wameshinda 10, na mechi 10 zikiisha kwa sare. Hata hivyo, historia haitakuwa na maana sana uwanjani Jumapili hii. Azam FC, wakiongozwa na kocha wao Bruno Ferry, wanatafuta kisasi baada ya kupoteza fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB kwa Yanga msimu uliopita.
Kocha mkuu wa Azam FC, Bruno Ferry, raia wa Ufaransa, ameweka wazi kwamba timu yake ipo tayari kwa vita, na lengo lao kuu ni kulipiza kisasi baada ya kupoteza fainali ya mwisho walipokutana na Yanga kwenye Kombe la Shirikisho la CRDB huko Zanzibar. Ferry amesema kuwa licha ya kuheshimu Yanga, hawana hofu na wanajiamini kuwa wataibuka na ushindi.
Kwa upande mwingine, kocha wa Yanga, Miguel Gamondi kutoka Argentina, amejipanga vyema kwa ajili ya fainali hii. Gamondi amesisitiza kuwa lengo lao ni moja tu, ambalo ni kuongeza taji jingine kwenye kabati lao la vikombe na kuwaridhisha mashabiki wao ambao wamekuwa nguzo muhimu katika safari yao.
Kikosi Cha Yanga Vs Azam Fc Fainali Ngao ya Jamii 2024
Kikosi cha Azam Dhidi ya Yanga Fainali
Mlinda Mlango
- 16 Mohamed Mustafa
Walinzi
- C5 Lusajo Mwaikenda
- 14 Cheikh Sidibe
- 24 Yeison Fuentes
- Ayannick Bangala
- 3 Yoro Diaby
Viungo
- 26 Adolf Mtasingwa
- 2 James Akaminko
- 15 Jhonier Blanco
Washambuliaji
- 6 Fei Toto
- 19 Gibril Sillah
Wachezaji Wa Akiba: Foba, Msindo, Chilambo, Meza, Samake, Diakite, Tiesse, Saadun na Adam
Fuatilia Hapa Matokeo Yanga VS Azam Leo Fainali Ngao ya Jamii 2024
Mapendekezo ya Mhariri:
- Kikosi Cha Simba VS Coastal union Ngao ya Jamii 11/08/2024
- Hizi apa Picha za Jezi Mpya ya KMC Fc 2024/2025
- Viingilio Mechi ya Fainali ya Yanga Vs Azam Fc Ngao Ya Jamii 2024
- Waamuzi Watakao chezesha Yanga SC vs Azam Ngao ya Jamii 2024: Hawa Hapa!
- Waamuzi Watakao chezesha Simba SC vs Coastal Union Ngao ya Jamii 2024: Hawa Hapa!
- Ratiba ya Simba Sc Ligi Kuu Ya NBC 2024/2025
- Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/2025 (NBC Premier league)
Weka Komenti