Kikosi Cha Simba VS Coastal union Ngao ya Jamii 11/08/2024 | Kikosi cha Simba dhidi ya Coastal Union
Simba Sc itaingia dimbani kesho, tarehe 11 Agosti 2024, kuwakabili Coastal Union Sc katika mchezo wa kuwania nafasi ya tatu katika michuano ya Ngao ya Jamii 2024. Pambano hili litapigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa majira ya saa tisa alasiri.
Simba Sc inajikuta katika nafasi hii ya kuwania ushindi wa tatu baada ya kupoteza mchezo wao wa nusu fainali dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Yanga Sc. Mchezo huo ulimalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi mwembamba wa 1-0, goli likifungwa na Max Nzegeli katika dakika za lala salama za kipindi cha kwanza. Simba, licha ya kufanya mashambulizi kadhaa, walishindwa kupenya ngome ya ulinzi ya Yanga iliyokuwa imara chini ya Bacca.
Coastal Union nao wanacheza mechi hii ya kuwania nafasi ya tatu baada ya kuchapwa 5-2 na Azam Fc katika mchezo wa nusu fainali.
Mechi ya Simba VS Coastal union inatarajiwa kuwa ya kusisimua, huku Simba wakitafuta faraja baada ya kupoteza nafasi ya kucheza fainali. Wekundu wa Msimbazi watataka kuonyesha ubora wao na kujihakikishia ushindi ili kumaliza michuano hii kwa heshima. Coastal Union, kwa upande wao, watataka kutumia fursa hii kujenga morali yao baada ya kipigo kikali kutoka kwa Azam Fc.
Kikosi Cha Simba VS Coastal union Ngao ya Jamii 11/08/2024
Kikosi Cha Simba kitakachoanza dhidi ya Coastal union katika mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu wa Ngao ya Jamii 11/08/2024 kimetangazwa rasmi na kocha mkuu wa simba. Hapa tumekuletea orodha ya wachezaji wote ambao wataunda wataanza katika mchezo huu
- 26 Camara
- 33 Kijili
- 15 Hussein C
- 14 Hamza
- 20 Che Malone
- 25 Okejepha
- Sinda
- 16 Karabaka
- 17 Fernandes
- 11 Mukwala
- 10 Ahoua
- 7 Mutale
Wachezaji wa Ziada; Ally, Kapombe, Nouma, Kazi, Ngoma, Mzamiru, Kagoma, Mashaka, Balua, Kibu.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Hizi apa Picha za Jezi Mpya ya KMC Fc 2024/2025
- Viingilio Mechi ya Fainali ya Yanga Vs Azam Fc Ngao Ya Jamii 2024
- Waamuzi Watakao chezesha Yanga SC vs Azam Ngao ya Jamii 2024: Hawa Hapa!
- Waamuzi Watakao chezesha Simba SC vs Coastal Union Ngao ya Jamii 2024: Hawa Hapa!
- Ratiba ya Simba Sc Ligi Kuu Ya NBC 2024/2025
- Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/2025 (NBC Premier league)
Weka Komenti