Kikosi cha Yanga vs Al Ahly Leo 23/01/2026

Kikosi cha Yanga vs Al Ahly Leo 23/01/2026

Wananchi wa Yanga SC leo Ijumaa Januari 23, wanashuka dimbani katika Uwanja wa Borg El Arab, Alexandria Misri, kuivaa klabu bingwa wa Afrika Al Ahly, katika mchezo wa tatu wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Mechi hii ya Kundi B itaanza saa 1:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki na itarushwa mbashara kupitia AzamSports2HD.

Katika msimamo wa kundi hilo, Yanga na Al Ahly wote wana pointi nne baada ya kila timu kushinda mechi moja na kutoka sare moja katika michezo miwili iliyopita. Tofauti ipo kwenye mabao, ambapo Al Ahly amefunga mabao matano na kuruhusu mawili, huku Yanga akifunga bao moja bila kufungwa. Ushindi kwa upande wowote leo unaweza kubadilisha kabisa mwelekeo wa uongozi wa kundi.

Kikosi cha Yanga vs Al Ahly Leo 23/01/2026

Yanga yaja na dhamira ya kushambulia

Yanga imetangaza wazi kuwa haina mpango wa kujilinda licha ya ukubwa na historia ya Al Ahly barani Afrika. Lengo la timu hiyo ya Tanzania ni kupata ushindi, na kama haitowezekana basi kupata sare, lakini sio kupoteza.

Akizungumza wakati msafara wa timu unaondoka kuelekea Misri, Kocha Mkuu wa Yanga, Pedro Goncalves, alieleza kuwa usajili uliofanywa kwenye dirisha dogo la usajili umeipa timu uwiano sahihi na imani ya kupambana na klabu yoyote Afrika.

“Tupo tayari kukutana na Al Ahly. Ni timu ngumu na yenye rekodi kubwa Afrika, lakini jambo zuri ni kwamba tuna timu imara. Hatutacheza kwa kujilinda; tutatumia ubora wa kikosi chetu kutafuta matokeo,” alisema Pedro.

Nguvu ya kikosi baada ya dirisha dogo la usajili

Kwa mujibu wa kocha huyo, mchanganyiko wa wachezaji wapya na waliokuwepo umeongeza ushindani mkubwa ndani ya kikosi, hali inayoongeza ari na umakini kwenye mazoezi pamoja na siku ya mechi.

Katika dirisha dogo la usajili, Yanga imefanikiwa kuwanasa:

  • Hussein Masalanga (kipa),
  • Mohammed Damaro na Allan Okello (viungo),
  • Emmanuel Mwanengo na Laurindo Aurélio ‘Depu’ (washambuliaji).

Wakati huo huo, Denis Nkane, Selestin Ecua na Mamadou Doumbia wametolewa kwa mkopo, huku Andy Boyeli aliyekuwa kwa mkopo akirejeshwa klabu yake ya Sekhukhune ya Afrika Kusini.

Pedro alisisitiza kuwa mabadiliko hayo yameifanya Yanga kuwa na kikosi pana, kinachompa uhuru wa kuchagua mifumo bora na kuwapumzisha wachezaji kutokana na ratiba ya mashindano mengi.

Kikosi cha Yanga vs Al Ahly Leo 23/01/2026

Kikosi cha kwanza cha Yanga SC kitakachoanza katika mchezo wa leo dhidi ya Al Ahly kinatarajiwa kutangazwa rasmi na benchi la ufundi majira ya saa 12:00 jioni, kuelekea kwenye pambano la hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Mashabiki wa Yanga wanasubiri kwa hamasa kuona orodha ya wachezaji watakaopewa dhamana ya kuanza, hasa wale walioonyesha kiwango bora katika michezo iliyopita.

Miongoni mwa majina yanayotajwa kwa matarajio makubwa ni Pacome Zouzoua, Maxi Nzengeli, Mudathir Yahaya na Diarra, wachezaji ambao wamekuwa na mchango muhimu katika uimara na ushindani wa kikosi cha Yanga katika mechi za hivi karibuni. Uamuzi wa benchi la ufundi kuhusu kikosi cha kuanza unatarajiwa kuakisi falsafa ya timu ya kucheza kwa ushindani na kutafuta matokeo chanya ugenini.

Hiki Apa Kikosi kilichotangazwa

Kikosi cha Yanga vs Al Ahly Leo 23/01/2026

Umuhimu wa matokeo ya leo

Ushindi dhidi ya Al Ahly utaifanya Yanga kufikisha pointi saba na kujiweka katika nafasi nzuri ya kuongoza Kundi B. Hii ni mechi yenye uzito mkubwa kwani timu nyingine za kundi hilo, FAR Rabat ya Morocco na JS Kabylie ya Algeria, zina pointi moja kila moja, hivyo ushindi wa leo unaweza kuwa hatua muhimu kuelekea kufuzu hatua inayofuata.

Muhtasari wa mechi

  • Mechi: Yanga SC vs Al Ahly
  • Mashindano: Ligi ya Mabingwa Afrika – Hatua ya Makundi (Kundi B)
  • Tarehe: Ijumaa, 23/01/2026
  • Uwanja: Borg El Arab, Alexandria – Misri
  • Muda: Saa 1:00 usiku (EAT)
  • Matangazo: AzamSports2HD

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Yanga Yarejea Ligi Kuu Kwa Kishindo Baada ya Kuicharaza Mashujaa 6-0
  2. Cv ya Allan Okello Kiungo Mpya wa Yanga Sc 2025/2026
  3. Matokeo ya Yanga VS Mashujaa Leo 19/01/2026
  4. Kikosi cha Yanga Vs Mashujaa Leo 19/01/2026
  5. Ratiba ya Nusu Fainali AFCON 2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo