Kikosi cha Yanga Vs Namungo FC Leo 13/05/2025

Yanga Vs Namungo FC Leo 13 05 2025 Saa Ngapi

Kikosi cha Yanga Vs Namungo FC Leo 13/05/2025 | Kikosi cha Yanga leo dhidi ya Namungo Fc Ligi Kuu

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC, Yanga SC, leo Jumanne, Mei 13, 2025, watashuka dimbani kwa mara nyingine kuendeleza safari yao ya kutetea taji la ubingwa, kwa kuwakaribisha Namungo FC katika mchezo wa raundi ya pili utakaopigwa kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam. Mchezo huo utaanza saa 10:15 jioni na kurushwa moja kwa moja kupitia Azam Sports 1 HD.

Kwa sasa, Young Africans wanaongoza msimamo wa ligi kwa alama 70 baada ya mechi 26, wakijivunia ushindi katika michezo 23, sare moja, na kupoteza michezo miwili pekee. Mchezo wa leo dhidi ya Namungo FC unakuwa wa muhimu sana kwa Kocha Mkuu Miloud Hamdi na kikosi chake, hasa kwa kuzingatia umuhimu wa kuendelea kuimarisha nafasi yao kileleni mwa jedwali la NBC Premier League.

Kikosi cha Yanga Vs Namungo FC Leo 13/05/2025

Kikosi cha Yanga Vs Namungo FC Leo 13/05/2025

Kikosi rasmi cha Yanga kitakacho anza leo dhidi ya Namungo Fc kinatarajiwa kutangazwa majira ya saa 9 alasiri. Hapa tutakuletea orodha kamili ya wachezaji wote watakaounda kikosi hicho mara tu kitakapotangazwa na kocha mkuu wa Yanga Miloud Hamdi.

Kikosi cha Yanga Vs Namungo FC Leo 13/05/2025

Historia ya Mikutano ya Hivi Karibuni

Katika michezo mitano ya mwisho baina ya Yanga SC na Namungo FC, Wananchi wameonyesha ubora wa hali ya juu kwa kuibuka na ushindi katika kila mechi. Takwimu zinaonesha:

  • Namungo FC 0-2 Yanga SC
  • Namungo FC 1-3 Yanga SC
  • Yanga SC 1-0 Namungo FC
  • Yanga SC 2-0 Namungo FC
  • Namungo FC 0-2 Yanga SC

Kwa jumla, Yanga SC imeshinda mechi 5 mfululizo dhidi ya Namungo, ikifunga mabao 9 na kuruhusu mabao 2 pekee. Hii inaipa klabu hiyo ya Jangwani rekodi ya kuvutia kuelekea mchezo wa leo.

Kauli ya Kocha Miloud Hamdi Kabla ya Mchezo

Akizungumza kuelekea mchezo huu muhimu, Kocha Miloud Hamdi amesisitiza kuwa maandalizi yamekamilika na timu iko katika hali nzuri ya kiakili na kimwili. Ameweka wazi kuwa malengo yao ni kushinda kila mechi iliyopo mbele yao, huku akitambua uwezo wa wapinzani wao.

“Tumejiandaa vizuri sana kuelekea mchezo wetu wa kesho, wachezaji wote wana morali ya kutosha kukabiliana na Namungo. Tuna muda mrefu bila mechi ya ushindani hivyo kesho tutacheza kwa umakini mkubwa sana,” alisema Hamdi.

Aidha, kocha huyo amefurahishwa na kurejea kwa baadhi ya wachezaji muhimu katika kikosi, jambo linaloimarisha zaidi safu yake ya ushambuliaji na ulinzi.

“Lengo letu kuu ni moja tu, kushinda kila mechi ambayo ipo mbele yetu. Tunahitaji kuwa mabingwa msimu huu na hilo lipo wazi. Nawaheshimu Namungo, nafahamu wana timu nzuri lakini kwetu sisi kesho ni mchezo muhimu wa kushinda, hatupaswi kabisa kudondosha alama tena ukizingatia tupo nyumbani,” aliongeza Hamdi.

Hali ya Namungo FC

Namungo FC, inayonolewa na kocha Juma Mgunda, ipo nafasi ya 9 katika msimamo wa ligi ikiwa na alama 31 baada ya kucheza mechi 27. Wamejikusanyia ushindi katika michezo 8, sare 7, na kupoteza michezo 12. Ingawa wanapambana kuhakikisha wanamaliza msimu katika nafasi salama, wanakutana na timu ambayo ina rekodi bora dhidi yao.

Kwa mujibu wa historia ya hivi karibuni, Namungo FC haijapata ushindi wowote dhidi ya Yanga SC katika michezo yao mitano ya mwisho, hali inayoifanya kuwa na mtihani mgumu mbele ya Wananchi wenye kiu ya kutetea ubingwa.

Mahali na Saa ya Mchezo

📍 Uwanja: KMC Complex, Dar es Salaam

⏰ Muda: Saa 10:15 jioni (13/05/2025)

📺 Matangazo: Azam Sports 1 HD

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Yanga Vs Namungo FC Leo 13/05/2025 Saa Ngapi?
  2. Xabi Alonso Atangazwa Kuwa Kocha Mpya wa Real Madrid Hadi 2028
  3. Simba Yapewa Vitisho Vikali na KMC Kuelekea Mechi ya Kesho Mei 11, 2025
  4. Napoli Yajipanga Kumsajili Jack Grealish Kutoka Man City
  5. KENGOLD Yapanga Kuipeleka Simba Ruvuma Juni 18
  6. Simba SC Yakata Tiketi Ligi ya Mabingwa Afrika 2025-2026 Baada ya Kufikisha Pointi 66
  7. Yanga Yashikilia Msimamo wa Kutocheza Dabi Licha Ya Majibu ya CAS
  8. Simba Yaitandika JKT na Kujiweka Kwenye Njia ya Ligi ya Mabingwa
  9. Matokeo JKT Tanzania vs Simba Leo 05/05/2025
  10. Sababu 3 Zilizofanya CAS Kuitupilia Mbali Kesi ya Yanga
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo