Kikosi cha Yanga vs Zimamoto Leo 29/04/2025

Matokeo ya Zimamoto VS Yanga Leo 29 04 2025

Kikosi cha Yanga vs Zimamoto Leo 29/04/2025 | Kikosi cha Yanga Leo Dhidi ya Zimamoto

KIKOSI cha Yanga usiku wa leo kinatarajiwa kushuka tena dimbani katika Uwanja wa Gombani, Pemba, kuumana na Zimamoto FC katika nusu fainali ya michuano ya Kombe la Muungano—maarufu pia kama Mapinduzi Cup. Mechi hiyo inakuja wakati klabu hiyo ya Jangwani ikisaka rekodi mpya katika mashindano hayo yaliyorejeshwa rasmi mwaka jana baada ya kusimama kwa zaidi ya miaka 20 tangu 2003.

Mechi hiyo itapigwa saa 1:15 usiku, ikiwa ni ya pili ya hatua ya nusu fainali, kufuatia pambano la jana kati ya JKU na Azam FC. Mshindi wa Yanga dhidi ya Zimamoto ataungana na mshindi wa jana kwa ajili ya fainali itakayochezwa Mei Mosi, huku kila timu ikipambana kwa nguvu zote kufikia hatua ya mwisho ya mashindano haya ya kihistoria.

Kikosi cha Yanga vs Zimamoto Leo 29/04/2025

Kikosi cha Yanga vs Zimamoto Leo 29/04/2025

Kikosi rasmi cha Yanga kitakacho anza leo dhidi ya Zimamoto Fc kinatarajiwa kutangazwa majira ya saa 12 jioni. Hapa tutakuletea orodha kamili ya wachezaji wote watakaounda kikosi hicho mara tu kitakapotangazwa na kocha mkuu wa Yanga Miloud Hamdi.

Kikosi cha Yanga vs Zimamoto Leo 29/04/2025

Yanga inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na lengo moja kuu—kulirejesha taji la Kombe la Muungano katika mikono yao na kuvunja rekodi ya kuwa na mataji sita sawa na Simba. Hadi sasa, Yanga imetwaa taji hilo katika miaka ya 1983, 1987, 1991, 1996, 1997, na 2000.

Ikiwa inaongoza Ligi Kuu Tanzania Bara kwa pointi 70 baada ya mechi 26, Yanga inalenga kuendeleza ubora wake mbele ya wapinzani kutoka Zanzibar. Katika hatua ya robo fainali, Yanga iliifunga KVZ mabao 2-0, ikionyesha uwezo mkubwa wa safu ya ushambuliaji na uimara wa benchi la ufundi linaloongozwa na kocha Miloud Hamdi. Licha ya changamoto, Hamdi anaweka msisitizo kwa kikosi chake kuhakikisha wanarudi Dar es Salaam na ubingwa wa mashindano hayo.

Kwa upande wa Zimamoto, kikosi hicho kinachonolewa na kocha Mohamed Ali kimekuwa na msimu mzuri katika Ligi Kuu Zanzibar, ambapo kimejikusanyia pointi 36 katika mechi 22, na kushika nafasi ya sita. Katika robo fainali, Zimamoto waliiondoa Coastal Union kwa ushindi wa bao 1-0, ushindi ambao umeongeza morali kikosini kuelekea mechi ya leo.

Zimamoto haijawahi kutwaa taji la Kombe la Muungano, na ushindi dhidi ya Yanga utakuwa hatua kubwa kuelekea kwenye fainali na uwezekano wa kuandika historia. Timu chache kutoka Zanzibar ndizo zilizowahi kutwaa taji hilo—KMKM mwaka 1984 na Malindi miaka ya 1989 na 1992. Kocha Mohamed Ali anasisitiza kuwa licha ya hadhi ya Yanga, mchezo unaamuliwa ndani ya uwanja, na kikosi chake kipo tayari kupambana mpaka dakika ya mwisho.

Mapendekezo ya Mhariri

  1. Zimamoto VS Yanga Leo 29/04/2025 Saa Ngapi?
  2. Matokeo ya Zimamoto VS Yanga Leo 29/04/2025
  3. Ratiba ya Kombe la Muungano 2025
  4. Liverpool Wafanikiwa Kuwa Mabingwa EPL 2024/2025
  5. Ratiba ya Fainali Kombe La Shirikisho Afrika CAF 2024/2025
  6. Simba SC Yatinga Fainali Kombe la Shirikisho Afrika Baada ya Sare na Stellenbosch
  7. Matokeo ya Stellenbosch VS Simba SC Leo 27 April 2025
  8. Kikosi cha Simba SC vs Stellenbosch Leo 27 April 2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo