Real Madrid Yatinga Fainali ya Klabu Bingwa 2024 | Waichapa Bayer Munich Jumla ya Magoli 3-4
Fainali ya UEFA Champions League 2024 ni Real Madrid dhidi ya Borussia Dortmund
Baada ya mchezo wa pili wa nusu fainali ya kombe la klabu bingwa Ulaya linalojulikana kama UEFA, sasa macho na masikio ya mashabiki wa mpira duniani kote yamemia katika michuano ya fainali ambayo itamkutanisha bingwa wa nusu fainali ya kwanza Borussia Dortmund dhidi ya Real Madrid. Mchezo wa fainali ya klabu bingwa mwaka huu wa 2024 unatarajiwa kuchezeka Jumamosi, Juni 1 saa 9 mchana. ET.
Real Madrid Yatinga Fainali Ya Klabu Bingwa 2024 Ikimtoa Bayern
Borussia Dortmund – ambayo kwa sasa iko katika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi ya Ujerumani Bundesliga – ilifika fainali baada ya kuiondoa Paris Saint-Germain, ambayo ilinyakua taji la Ligue 1 ya Ufaransa kwa msimu wa tatu mfululizo.
Real Madrid walifunga mabao mawili dakika za jioni kabisa – huku Joselu aliyetokea benchi kipindi cha pili akifunga mabao yote mawili yalio hakikishia Real madrid tiketi ya kufuzu hatua ya fainali kwa mara ya 18 katika historia ya mabingwa hao wa Uispania.
Kikosi cha Thomas Tuchel kilikuwa kinacheza kwa kujilinda, kilinusurika mara kadhaa na mbali ya hapo kiliweza hadi kufunga goli la kutangulia, Alphonso Davies akipiga shuti zuri na kuwapa uongozi wa 1-0, 3-2 kwa jumla ya mabao, na kuongeza ndoto ya fainali.
Kushindwa kwa bayern kuongeza goli ambalo lingewapa uongozi mkubwa dhidi ya Real Madrid ambao wamekua wabishi kukubali kutoka ndio ilikua mwisho wa ndoto ya mabingwa hao wa ujerumani na Harry Kane kufuzu hatua ya fainali ya UEFA baada ya Madrid kupindua meza katika dakika za mwishoni.
Jinsi Borussia Dortmund walivyofika fainali ya Klabu bingwa ulaya UEFA Champions 2024
- Hatua ya Makundi: Imeshinda Kundi F, ambalo pia lilijumuisha Paris Saint-Germain, AC Milan na Newcastle United
- Awamu ya 16: PSV Eindhoven ilishindwa
- Robo Fainali: Waliwashinda Atlético Madrid
- Nusu fainali: Ilishinda Paris Saint-Germain
Jinsi Real Madrid walivyofika fainali ya Klabu Bingwa 2024
- Hatua ya Makundi: Imeshinda Kundi C, ambalo pia lilijumuisha Napoli, Braga na Union Berlin
- Raundi ya 16: RB Leipzig ilishindwa
- Robo Fainali: Iliishinda Manchester City
- Nusu fainali: Waliwashinda Bayern Munich
Mapendekezo Ya Mhariri:
Weka Komenti