Kiungo Mghana Enock Aingia Kwenye Radar ya Singida BS

Kiungo Mghana Enock Aingia Kwenye Radar ya Singida BS

MABOSI wa Singida Black Stars wameanza kumfuatilia kwa karibu kiungo mshambuliaji wa klabu ya Gor Mahia ya Kenya, Mghana Enock Morrison, wakati hatma ya mkataba wake na timu hiyo ikibaki kuwa haijafahamika.

Morrison, ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu, hajaanza mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya na klabu hiyo, hali inayofanya baadhi ya timu kuanza kuonyesha nia ya kumtaka.

Taarifa kutoka ndani ya Singida Black Stars zinaeleza kuwa kiungo Mghana Enock Aingia Kwenye Radar ya Singida BS baada ya kuingia kwenye orodha ya wachezaji wanaofuatiliwa na klabu hiyo kwa ajili ya mipango ya kuimarisha kikosi.

Chanzo kutoka ndani ya timu hiyo kilieleza kuwa Morrison ni miongoni mwa wachezaji wanaofuatiliwa kwa ukaribu, huku mawasiliano ya awali kuhusu uwezekano wa kumpata yakianza kujadiliwa tangu dirisha dogo la usajili la Januari 2026.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, mmoja wa viongozi wa Singida Black Stars aliyeshiriki kufanikisha usajili wa mshambuliaji Elvis Rupia ndiye anayeshughulikia mchakato huo. Inaelezwa kuwa kiongozi huyo ana ushirikiano mzuri na mchezaji huyo pamoja na baadhi ya viongozi wa Gor Mahia, jambo linalorahisisha mawasiliano ya awali.

Kiungo Mghana Enock Aingia Kwenye Radar ya Singida BS

Hata hivyo, chanzo hicho kinasema bado ni mapema kutoa kauli ya mwisho kuhusu hatma ya usajili huo kutokana na muda uliobaki kabla ya mwisho wa msimu.

“Ni mapema sana kuzungumzia hilo kwa sababu miezi mitatu iliyobakia lolote linaweza kutokea. Sisi tunamsajili mchezaji mzuri kutokana na ripoti na mapendekezo ya benchi letu la ufundi, hivyo acha tuone mwisho wake,” kilisema chanzo hicho.

Mbali na Singida Black Stars, taarifa kutoka Ghana zinaeleza kuwa Simba pia imekuwa ikimfuatilia Morrison kwa ukaribu, ingawa hadi sasa hakuna makubaliano rasmi yaliyowasilishwa mezani.

Morrison, aliyezaliwa Januari 18, 2000, ana uwezo wa kucheza kama kiungo wa kati huku pia akitokea upande wa kulia na kushoto. Kabla ya kucheza Gor Mahia, aliwahi kuzichezea klabu za King Faisal FC na Asante Kotoko zote za nchini Ghana.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Yanga Yashindwa Kulenga Lango Dhidi ya Azam FC Licha ya Uwepo wa Depu na Dube
  2. Bilioni 388.8 Kujenga AFCON City Unguja
  3. Tanzania Yatoa Zaidi ya Sh80 Bilioni CAF Ili Kuwa Mwenyeji wa AFCON 2027
  4. Depu Aibuka Shujaa Yanga Ikiichapa Tanzania Prisons Kwa Bao Pekee
  5. Azam FC Yavunja Ukame wa Ushindi Ugenini Kwa Kuichapa Dodoma Jiji 3-0
  6. Mpanzu Aipa Simba Pointi Tatu dhidi ya Singida Black Stars Uwanja wa Airtel
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo